Endapo majina ya walioambukizwa Corona yatatangazwa hadharani patakuwa na ubaya gani?

Endapo majina ya walioambukizwa Corona yatatangazwa hadharani patakuwa na ubaya gani?

Corona ni janga la kimataifa.

Prince Charles katangazwa, PM Boris katangazwa na PM Netanyahu katangazwa.

Sasa, najiuliza hapa Tanzania kuna ubaya gani kuwatangaza wenye dalili na wenye maambukizi?

Anayeweza kunijibu Tafadhali!
Ndugu yangu hao wametangazwa kwa kuwa wameruhusu watangazwe...ugonjwa wowote ule ni Siri ya mgonjwa na familia yake...Kuna privacy...hata daktari haruhusiwi kutangaza publicly ni Nini mgonjwa wake anaumwa...yaani hata Kama anaumwa malaria haruhusiwi kutangaza mpaka mgonjwa aruhusu...labda kwa issue maalum za mahakamani pengine on special cases labda inaweza kutangazwa Kama labda kutoa ushahidi..nasema labda..Kuna watu wanna ukimwi lakini hawatangazwi...Kama wewe una ugonjwa Fulani na unataka utangazwe ili usiwaambukize watu unaweza kufanya hivyo...
 
Hahahaha chadema wata ua mtu

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kibongo bongo ukishakubali kujitangaza hiyo itakuwa nongwa hata kwenye siasa huwezi pata wadhifa tena. Mara tutakuja kusikia watu wakiambiwa kwa maneno ya kejeli kuhusu ugonjwa huu. Huku kwetu bongo ukituhumiwa na kashfa fulani wakati haijathibitika mahakamani na ww ukaamua kuachia ngazi kupisha uchunguzi hiyo itakuwa imekula kwako kila mtu atakunyooshea kidole kuwa fulani amekula rushwa mbona kaachia madara mwenyewe kama asingekula navyojua angekataa tu. Hivyo kwa muktadha wetu waache hivo hivo waendelee kutangaza idadi bila kutaja majina ya wahusika ili wasije chafuliwa future yao

DUMU KUBWA
 
Wakitangazwa itasaidia nini? Duniani hakuna nchi inayotangaza majina ya wagonjwa wanaokwenda hospitalini na magonjwa wanayougua . Hao kina waziri mkuu wa Uingereza ni public figures ndiyo maana wamejitangaza wenyewe. Hata hapa kwetu kama kuna kiongozi ameambukizwa na kuamua kuwajulisha wananchi hazuiwi. Ila huwezi kutangaza ugonjwa wa mtu.
Kwani Mtoto wa Mh.Mbowe nae ni public figure ..maana rahisi wa pili alimtangaza
 
PM Netanyahu hajapatikana na corona. Aliyetest positive ni aide wake.
 
Kwani Mtoto wa Mh.Mbowe nae ni public figure ..maana rahisi wa pili alimtangaza
Kwanza lazima ujue hata hao public figures ni wao wenyewe hujitangaza au huwaambia wasaidizi wao wawatangaze na siyo mtu mwingine anakurupuka tu na kutangaza! Kuhusu huyo mtoto, Makonda alifanya kosa kusa kubwa sana na angetakiwa awajibishwe kwa ujinga aliofanya. Familia ya Mbowe ikitaka inaweza kumshtaki ila serikali ilitakiwa kumwajibisha pia.
 
Corona ni janga la kimataifa.

Prince Charles katangazwa, PM Boris katangazwa na PM Netanyahu katangazwa.

Sasa, najiuliza hapa Tanzania kuna ubaya gani kuwatangaza wenye dalili na wenye maambukizi?

Anayeweza kunijibu Tafadhali!
Nenda Lumumba kawaulize wana CCM wenzako, chini ya serikali ya kipumbavu ya CCM unayoishabikia kila jambo ni la kipumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo wanaoshuka pale JNIA na kuwekwa karantini hawatendewi haki?!
Wanatendewa haki kabisa. Kuwawekea karantini ni kuzuia wasisambaze ugonjwa. Kama mtu akiwekwa karantini na wakati yuko karantini akakutwa na vurus lakini akakataa matibabu yoyote, basi ana haki ili mradi tu hadai kuachiwa.
 
tena watuwekee na picha zao kabisa.
ili tujuane
Mambo mengine ni busara ,kwa magonjwa ya mlipuko ni busara kutangaza ili waliokutana na mhusika karibuni wachukue tahadhari na kuanza tiba japo hata doz za limao.Japo mimi nipo na JPM hili si gojwa letu litapita tuchape kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona ni janga la kimataifa.

Prince Charles katangazwa, PM Boris katangazwa na PM Netanyahu katangazwa.

Sasa, najiuliza hapa Tanzania kuna ubaya gani kuwatangaza wenye dalili na wenye maambukizi?

Anayeweza kunijibu Tafadhali!
Kenya mtu alipigwa mpaka kufa kisa tu anahisiwa ana korona.

Halafu hakunaga utaratibu hospitalini wa kumtangaza mgonjwa
 
Corona ni janga la kimataifa.

Prince Charles katangazwa, PM Boris katangazwa na PM Netanyahu katangazwa.

Sasa, najiuliza hapa Tanzania kuna ubaya gani kuwatangaza wenye dalili na wenye maambukizi?

Anayeweza kunijibu Tafadhali!
Halafu mtu mwenyewe ndio anaridhia kutangazwa au kutotangazwa.

Siyo mambo kqma yale aliyofanya Bashite...
 
Ukiacha Mambo ya kujitangaza kuwa na Corona ni mambo gani mengine ungependa tuyaige kutoka kwa PM Boris?

Back
Top Bottom