Endelea kupambana mpaka uone matokeo

Endelea kupambana mpaka uone matokeo

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Kwa aina ya kazi na majukumu ninayofanya na pia kwa utashi wangu binafsi huwa naona na familia yangu hasa watoto kwa nadra sana.Pamoja na kwamba huwa tunaonana kwa nadra mimi na watoto wangu tumejifunza namna bora ya kutumia muda mchache tunaokuwa pamoja kikamilifu.Nipatapo nafasi huwa nawapigia simu na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali lakini jambo la muhimu ambalo huwa nahakikisha kwamba wanatambua ni kwamba Pamoja na kwamba sipo nao lakini ninafuatilia kwa ukaribu maisha yao na maendeleo yao.

Katika moja ya mazungumzo na mwanangu,nilimuuliza kuhusu maendeleo yake shule na akanieleza kuhusu hesabu mpya walizofundisha za kutoa kwa kukopa.Kwa jinsi alivonieleza nilielewa kuwa somo alilielewa lakini niliamua kumuuliza swali,Kwani unapokopa unakopa kutoka wapi?Akasema kwenye hiyo inayofuata ambayo ni kubwa, Nikamuuliza unajuaje kuwa ni kubwa?Akanieleza kuhusu makumi,mamoja etc.Mwisho nikamwambia ukishakopa unarudishaje?

Hapa alikaa kimya kidogokisha akasema Hurudishi kwa sababu anayo nyingi.Sikutaka kumchosha kichwa zaidi lakini nilifurahi kwamba somo la reasoning ambalo ndo somo kubwa ambalo nataka watoto wangu walipate shuleni linaendelea vizuri.Wakati mwingine nilimuuliza tofauti kati ya hetrufi kubwa na ndogo.Katika mjadala nikamuuliza tofauti kati ya Z kubwa na Ndogo na S kubwa na ndogo na akanijibu tu kwamba unapoandika inabidi iwe kubwa zaidi.Kila baada ya mjadal wetu nilihakikisha kwamba ninamuachia swali la kutafakar ambalo ni gumu kuliko upeo wake.

Nilichojifunza ni kwamba kadiri nilvokuwa nikimuuliza maswali magumu ndivo na yeye alivobadilika kiupeo akitaka kunionesha kwamba amepata jibu au suluhu au ameelewa jambo fulani.

Katika maisha muamko wa kutaka kuendelea kujifunza na kukua na kupata maendeleo na kuleta mabadiliko ni muhimu sana.Muamko huo unapopotea maisha hupoteza maana na mwamko huwa unapokuwa Juu au unapochochewa basi maisha huwa yenye maana zaidi.Katika biashara muamko huu nao ni muhimu sana.Haijalishi biashara yako ni kubwa kiasi gani au mtaji wako ni mkubwa kiasi gani kadiri unavochochea ubunifu na kufanya maboresho ndivo unavoendelea kuona umuhimu wa biashara yako na kupata muamko zaidi.

Wengi wetu hujikuta tunapoteza hamasa katika biashara zetu kwa sababu hatujipi muda wa kutafakari uelekeo wa biashara zetu na kuweka mikakati ya kukuza biashara yetu.Ni lazima ujitahidi kuongeza ubunifu na maarifa katika biashara yako.Tazama watu wengine wanafanya nini katika biashara zao na ukiweza fanya maboresho kidog😵ngeza ubunifu kidogo.Mabadiliko hayo ni muhimu sio tu kwa ajili ya biashara yako bali pia kwa ajili yako mwenyewe.

Hisia ya mafanikio utakayoipata itakufanya ujione mwenye faraja na amani moyoni.

Nakutakia Kila la heri katika ujenzi wa taifa.
 
Kwa aina ya kazi na majukumu ninayofanya na pia kwa utashi wangu binafsi huwa naona na familia yangu hasa watoto kwa nadra sana.Pamoja na kwamba huwa tunaonana kwa nadra mimi na watoto wangu tumejifunza namna bora ya kutumia muda mchache tunaokuwa pamoja kikamilifu.Nipatapo nafasi huwa nawapigia simu na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali lakini jambo la muhimu ambalo huwa nahakikisha kwamba wanatambua ni kwamba Pamoja na kwamba sipo nao lakini ninafuatilia kwa ukaribu maisha yao na maendeleo yao.

Katika moja ya mazungumzo na mwanangu,nilimuuliza kuhusu maendeleo yake shule na akanieleza kuhusu hesabu mpya walizofundisha za kutoa kwa kukopa.Kwa jinsi alivonieleza nilielewa kuwa somo alilielewa lakini niliamua kumuuliza swali,Kwani unapokopa unakopa kutoka wapi?Akasema kwenye hiyo inayofuata ambayo ni kubwa,Nikamuuliza unajuaje kuwa ni kubwa?Akanieleza kuhusu makumi,mamoja etc.Mwisho nikamwambia ukishakopa unarudishaje?Hapa alikaa kimya kidogokisha akasema Hurudishi kwa sababu anayo nyingi.Sikutaka kumchosha kichwa zaidi lakini nilifurahi kwamba somo la reasoning ambalo ndo somo kubwa ambalo nataka watoto wangu walipate shuleni linaendelea vizuri.Wakati mwingine nilimuuliza tofauti kati ya hetrufi kubwa na ndogo.Katika mjadala nikamuuliza tofauti kati ya Z kubwa na Ndogo na S kubwa na ndogo na akanijibu tu kwamba unapoandika inabidi iwe kubwa zaidi.Kila baada ya mjadal wetu nilihakikisha kwamba ninamuachia swali la kutafakar ambalo ni gumu kuliko upeo wake.

Nilichojifunza ni kwamba kadiri nilvokuwa nikimuuliza maswali magumu ndivo na yeye alivobadilika kiupeo akitaka kunionesha kwamba amepata jibu au suluhu au ameelewa jambo fulani.

Katika maisha muamko wa kutaka kuendelea kujifunza na kukua na kupata maendeleo na kuleta mabadiliko ni muhimu sana.Muamko huo unapopotea maisha hupoteza maana na mwamko huwa unapokuwa Juu au unapochochewa basi maisha huwa yenye maana zaidi.Katika biashara muamko huu nao ni muhimu sana.Haijalishi biashara yako ni kubwa kiasi gani au mtaji wako ni mkubwa kiasi gani kadiri unavochochea ubunifu na kufanya maboresho ndivo unavoendelea kuona umuhimu wa biashara yako na kupata muamko zaidi.

Wengi wetu hujikuta tunapoteza hamasa katika biashara zetu kwa sababu hatujipi muda wa kutafakari uelekeo wa biashara zetu na kuweka mikakati ya kukuza biashara yetu.Ni lazima ujitahidi kuongeza ubunifu na maarifa katika biashara yako.Tazama watu wengine wanafanya nini katika biashara zao na ukiweza fanya maboresho kidog😵ngeza ubunifu kidogo.Mabadiliko hayo ni muhimu sio tu kwa ajili ya biashara yako bali pia kwa ajili yako mwenyewe.

Hisia ya mafanikio utakayoipata itakufanya ujione mwenye faraja na amani moyoni.

Nakutakia Kila la heri katika ujenzi wa taifa.
Good mkuu, me pia namuomba Mungu anisaidie niishi hivyo na family yangu
 
Huku kwetu ushenzini ukiboresha tu, basi wanaona tayari umefanikiwa, wanasusa huduma yako, ama bidhaa yako.

Suluhisho endelea kuvaa madabwada, lialia hali ngumu basi mteja anafurahi kweli kweli! Ya hondohondo, mbayuwayu changanya na zako.
 
Back
Top Bottom