Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,081
- 2,325
Lile eneo la Ukonga Banana ambalo mwana-ubalozi wa Canada alimtemea trafiki mate lilianza kutengenezwa tangu Ijumaa (11.12.2009), siku moja tu baaba ya tukio. Sijui ni kwa sababu ya tukio hilo au ni matengenezo ya kawaida lakini panapotengenezwa ni pale kituoni Banana-ukonga tu (palipokuwa na tukio la kutemea mate). Maaskari pia wameongezwa sehemu ile. Sasa hivi foleni kubwa iliyokuwepo imepungua sana.