KWELI Eneo iliporekodiwa video hii ni makutano ya barabara Moshi mjini, Kilimanjaro

KWELI Eneo iliporekodiwa video hii ni makutano ya barabara Moshi mjini, Kilimanjaro

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau tumia nyenzo za kidigitali kubainisha eneo halisi iliporekodiwa video hii?

Screenshot 2025-12-04 195900.png
 
Tunachokijua
Uhakiki na uthibitishaji wa maudhui picha na video ni muhimu ili kudhibiti upotoshaji unaoweza kufanyika kupitia maudhui ya aina hiyo. Hivyo ni muhimu kujifunza namna ya kutumia nyenzo za kidijitali zinazotuwezesha kubaini uhalisia wa picha na video ili kuepuka upotoshaji wakati wote.

Uthibitishaji Picha kwa kutumia Google Reverse Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu video kwa kuchukua picha (screenshot) katika sehemu ya video husika.

JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha na video. Rejea kiungo hiki kufuata hatua zote.

Mfano tutumie video hii inaonesha mazingira ya mjini, sehemu ya makutano ya barabara (Round about). Je video hiyo ilirekodiwa eneo gani?

Wadau wa JamiiCheck wameshiriki kuthibitisha video hiyo kwa kutumia nyenzo za kidigitali ambapo wanabainisha kuwa eneo la video hiyo ni Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, makutano ya barabara kuelekea Arusha.


Ufuatiliaji wa JamiiCheck

JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search imebaini kuwa video hiyo iliwahi kuchapishwa katika ukurasa wa Instagram wa irickoo Agosti 16, 2024 akibainisha kuwa eneo hilo ni Makutano maarufu ya barabara Moshi Mjini kuelekea mkoani Arusha.

Aidha kupitia Google Earth inaonesha Moshi mjini picha za makutano hayo ya barabara ambapo zinafanana na video hiyo.
​
1765008426586-png.3512037
Baada ya kufanya image reverse majibu yanonesha hapo ni Moshi mjini, Kilimanjaro
 
Back
Top Bottom