BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Lakini katika hali ya kushangaza katika eneo hilo biashara ya vyakula hususani matunda inaendelea ikiwa majitaka ya chemba inayopita maeneo ya karibu.
Wafanyabiashara hususani wa magenge ufika eneo hilo kila siku kuchukua bidhaa mbalimbali ikiwemo nyanya, karoti, nyanya chungu na matunda, lakini kwa hali inavyoendelea naona afya za Wananchi zikiwa hatarini kutoka na bidhaa kupangwa kwenye maeneo machafu huku magari yanayopita maeneo hayo yakiwa yanatimua hayo maji kutokana na barabara kujaa mashimo.
Licha ya changamoto za kiafya njia hiyo ni kero kwa watumiaji wa magari hususani daladala ambazo zinapita kwenye njia hiyo, ambapo mashimo hayo yanaleta foleni pamoja na kupelekea magari kuaribika kutokana na ubovu wa kipande hicho cha daladala.
Nashangaa kwanini mamlaka hazichukui hatua za haraka kuiweka barabara hiyo katika mazingira rafiki pamoja na kuondoa kero ya majitaka yanoyotokea kwenye chemba hasa kipindi mvua zikinyesha.
Rai yangu kwa mamlaka ikiwemo Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ambao wapo karibu na eneo hilo wafuatilie changamoto hiyo na kuipatia ufumbuzi wa haraka.