Eneo la kufugia samaki kwa njia ya vizimba (cage culture) linakodishwa

Eneo la kufugia samaki kwa njia ya vizimba (cage culture) linakodishwa

Wazungu walifanya hivyoo wakaharibu kwao sasa wanabanana huku kwetu
Hakuna mzungu anaefanya vizimba bado ni wizara inawapa hadi mikopo wazawa ,isitoshe hakuna kemikali zinazotumika ni vyakula vya kawaida vinasagwa
 
Wachina wanamaeneo yao na wale watanzania mradi wao uliozinduliwa na Mama ni mradi wa kimkakati

Hii post inahusu eneo linalokodishwa kwa watu binafsi wanaotaka kuwekeza kwenye ufugaji samaki ila wanapitia ugumu kwenye kupata vibali
Mkuu ni gharama kiasi gani ambazo zinatakiwa baada ya kukodisha mpaka kufikia kuanza kuvuna?
 
Hizi ndio uchafuzi wa mazingira,napia uharibifu wa ziwa nendeni mkatoe haya makitu yenu ziwani mkawekee sehemu ingine ambapo ni sahihi . Tatizo hamtaki kujituma nyie ni Yes sio no
Kufuga samaki sio kujituma?
 
Mkuu ni gharama kiasi gani ambazo zinatakiwa baada ya kukodisha mpaka kufikia kuanza kuvuna?
Gharama zinategemea na unataka kuvuna tani ngapi per each production cycle

Mfano utengenezaji wa cage moja yenye uwezo wa kuchukua samaki 12,000 ni Tsh 3,000,000

Hivyo basi nikijua unataka kuweka cage ngapi itakuwa rahisi kukufanyia upembuzi yakinifu na kukupa actual cost
 
Wazungu walifanya hivyoo wakaharibu kwao sasa wanabanana huku kwetu
Jaribu kujenga mtazamo chanya, sio kila kitu kinacholetwa na wazungu ni kibaya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba unaenda kupunguza fishing pressure, kwa sababu watu wanakuwa na njia mbadala na ya uhakika ya kupata samaki bila kutengemea samaki toka vyanzo vya hasiri (ziwani, wabwani au mitoni)
 
Hakuna mzungu anaefanya vizimba bado ni wizara inawapa hadi mikopo wazawa ,isitoshe hakuna kemikali zinazotumika ni vyakula vya kawaida vinasagwa
Hakuna mzungu anaefanya vizimba bado ni wizara inawapa hadi mikopo wazawa ,isitoshe hakuna kemikali zinazotumika ni vyakula vya kawaida vinasagwa

TAFIRI wameshafanya research na kujilizisha ufugaji wa aina hii ni salama kwa mazingira

Samaki wanakuwa under control hawainteract na samaki wa asili
UKIONA MTU ANAWEKA L BADALA YA R NI JUA WAMESHAHARIBU KITU LAZIMA MUOGOPE
 
Gharama zinategemea na unataka kuvuna tani ngapi per each production cycle

Mfano utengenezaji wa cage moja yenye uwezo wa kuchukua samaki 12,000 ni Tsh 3,000,000

Hivyo basi nikijua unataka kuweka cage ngapi itakuwa rahisi kukufanyia upembuzi yakinifu na kukupa actual cost
Naomba unipembulie ya cage moja ya samaki 12,000 mpaka kufikia mavuno unatumia sh. Ngapi?
 
Naomba unipembulie ya cage moja ya samaki 12,000 mpaka kufikia mavuno unatumia sh. Ngapi?
Kupata kilo moja ya samaki inatumia kilo moja ya chakula,on average kilo moja ya chakula ni 3600 per kg Kwa chakula imported,kuna gharama za vifaranga bei ni 150-300tshs Kwa kimoja,ongeza gharama zako zingine binafsi usafiri,kusafisha vifaranga,kusafisha chakula,kijana WA kulisha,etc... profit margin itakua Kwa around 40%(Kwa hesabu kamili weka hiyo figure yako ya 12000 fish)
 
Back
Top Bottom