JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Uchafu huo unakusanywa kama dampo maeneo yanayozunguka sehemu walipo Wafanyabiashara kwa lengo la wahusika kuja kuubeba, lakini kinachosikitisha unarudikwa eneo ambalo linatumika kwa matumizi ya vyombo vya moto huku ukihatarisha usalama wa afya za Wananchi hususani kupindi hiki ambacho mlipuko wa kipindupindu umekuwa ukitajwa kuwepo kwa baadhi ya maeneo.
Licha hivyo uchafu huo ambao umekuwa ukitundikwa kwenye maeneo ya barabara, imekuwa sehemu ya vyanzo vinavyosababisha uwepo wa foleni wakati magari ya taka yanaposimamishwa kupakia uchafu huo eneo la barabara hasa majira ya asubuhi au jioni
Nitoe wito wangu kwa mamlaka zinazosimamia usafi wa mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuwajibika ipasavyo ikiwemo kuweka miundombinu rafiki kwa wafanyabiashara wa eneo hilo kwa ajili ya kumwaga taka badala ya utaratibu wa sasa wa kuzirundika katika eneo la barabara huku zikibaki kuzagaa na kuleta kero zaidi.
Ni vyema kuzingatia suala la usalama wa afya za Wananchi hususani kwenye eneo hilo lenye mkusanyiko wa Watu wengi, wahusika watambue wanahatarisha maisha ya wengi hasa ikitokea kukaibuka magonjwa ya mlipuko.
Pia soma:
~ Magari yanayobeba taka eneo la Tegeta-kwa Ndevu yanaleta kero ya foleni, wahusika wameshindwa kuliona hilo?
~ Taka zilizorundikwa barabarani eneo la Tegeta Kwandevu zimezolewa, sasa iwekwe mifumo rafiki ya kuhifadhi taka