Eneo Lenye nyumba ya Kuvunja Linauzwa Ubungo Kibangu

Eneo Lenye nyumba ya Kuvunja Linauzwa Ubungo Kibangu

Eneo lenye Nyumba ya Kuvunja Linauzwa.
Mahali: Ubungo Kibangu.

Eneo liko mita 100 kutoka barabara ya mandela, mita 2 kutoka barabara ya Makoka.
Nyumba iliyoko ndani ya eneo ina vyumba 26, mbele ina fremu 4 za biashara.

Ukubwa wa Eneo: SQM 626.
Bei: Tzs 450M. Mazungumzo yanaruhusiwa.
Nyaraka: Hatimiliki.

Kwa maelezo zaidi na kuweza kuona wasiliana nasi.
Mawasiliano: 0784 829565, 0767 833345, 0627 605807
@prathrealestate

450M ninu ue nyumba ubungo kibangu? aha ha ha ha 😂 😆 🤣 bora kuanzisha kiwanda kidogo huko pwani heka moja 10M eneo zuri kabisa

Wabongo tuache ujambazi
 
Ukimwambia aandike hapa hicho Kiwanja kwa Sqmtr moja anauza bei gani? yeye mwenyewe ataona aibu kuiandika hapa, ila haoni shida kutamka 450m. Hiyo hela ukienda nayo Bunju unamvua mtu mwenye 1600sqmtr na unatandaza Vila yako ya Maana. Unless labda uniambie umedhamiria kuisha karibu na mji, tena sehem yenyewe inambanano kama vile uko Kwa Mnyamani au Mchafuoge. Najaribu kupambanua tu.
 
Hahaha madalali wa bongo wanavunja sana mioyo ya watu kununua vitu kitu cha m 1 wao wanaweka m 7,5 yaan upigaji tu
 
Hizi sio biashara bwana,Ni Utapeli Utapeli Tu Mwingi.Hivi wewe unapoona mtu anataja BEI Milioni 450 kwa eneo ambalo ni sqm 650 inamaana kila sqm anauza 685,000.Hio thmani ya ardhi inatoka wapi?Kwamba Inatoka Hewani ama? Wizara ya Ardhi Eti Hawa Madalali wa Ardhi kodi mnazowatoza zinaendana na Bei wanazotaja huku au Ndio Ardhi inatumika kufanya utakatishaji wa fedha?
... ameamua kuweka bei ambayo mnunuzi hatokaa auze tena hata baada ya miaka 50!

Inasaidia kuzuia matapeli kuiacha baada ya muda mfupi miaka mitatu minne naye anauza tena kwa hela ndefu!

Bei iliyowekwa ni final hadi kiyama ya wafu ukinunua una nia kweli ya kuwekeza na sio "kuizungusha" 🤣🤣🤣 radhiya?
 
Back
Top Bottom