Eng. Hersi ateuliwa na FIFA kufundisha mfumo wa mabadiliko ya klabu Doha, Qatar

Eng. Hersi ateuliwa na FIFA kufundisha mfumo wa mabadiliko ya klabu Doha, Qatar

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani [FIFA], Limemchagua Rais wa Klabu ya Yanga SC na Mwenyekiti wa Umoja wa vilabu Afrika [ACA], Eng. Hersi Said kuwa miongoni mwa Wataalam watakaofundisha kwenye Kongamano kubwa la Mpira litakalofanyika Doha, Qatar, siku ya kesho, Desemba 14,2025.

1765620201981.png
Eng. Hersi, amepangiwa na FIFA kufundisha kwenye mada ya KEY ELEMENTS FOR CLUB SUCCESSFUL TRANFORMATION [ MFUMO WA MABADILIKO YA KLABU].

Miongoni mwa Wataalam wengine wa mpira Duniani watakaozungumza kwenye Kongamano hili ni Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, Roberto Di Mateo, Dennis Wise, Alexander Pato, Eric Abidal na wengine kibao

Eng Hersi Said ndiye mtaalamu pekee wa Mpira kutoka Afrika aliyepata nafasi ya kufundisha Kwenye Kongamano hilo.

1765620367492.png

1765620379247.png
 
Hersi anachokera ni kuingia au kujihusisha kwenye TZ politics. Komaa hukuhuku kunakufaa jamaa yangu
 
Mangungu wangu na Try Again vipi hawakuteuliwa?
 
Simba tunapambana na aggy Simba mamaeh kila mtu atakula alipoacha mboga mamaeh ..
 
Hersi Said keshapenya kuingia kwenye mtandao wa FIFA.
Alitaka kujiharibia kuingia kwenye siasa za bongoland.
FIFA ni mojawapo ya taasisi ya hovyo, iliyo na double standards na yenye ufisadi mkubwa duniani . Pia huwa inashirikiana kwa karibu sana na watawala wa hovyo wa kila aina.
 
Back
Top Bottom