Generation Z wamefanya jambo lao.
Manara anatafutiwa nafasi Yanga baada ya Ally Kamwe "kujaa" katika idara ya habari.
Kijana huyo ambaye ni "genius" katika mambo ya habari, ameimudu nafasi hiyo kwa kiasi kwamba amemfuta Haji Manara katika ulingo huo.
Moja ya mafanikio yake makubwa ni kuondoa u-afisa habari wenye asili ya uadui na kufitinisha, badala yake amekuja na mfumo ambao haujengi chuki, lakini wenye hamasa ya hali ya juu.
Ally Kamwe pia amekuwa na mvuto kwa vijana, ambao ndio kizazi kipya cha " wanazi" wa Yanga ikiashiria kwamba Yanga wanaunga generation iliyopita na ya sasa.
Kuna tetesi kwamba Haji Manara anaweza kupewa usemaji wa Baraza la Wazee kutokana na umri wake kufanana na Mzee Magoma, na pia kuna vimaneno kwamba atahamia Azam FC.
Manara anakuwa mzito kuhamia Azam FC kwa sababu ni vigumu kukutana na Mzee Bakhresa kila wakati na kumpiga shoti (mizinga) kama ilivyo rahisi kwa GSM