Eng. Hersi: Kombe la Ngao ya Jamii 2025 limeibwa wakati tunasherehekea parade

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said anasikitika kuwatangazia kuwa Ngao ya Jamii 2025 imeibiwa wakati wa kusherehekea Parade Yao na ameomba Kwa aliyechukua Ngao hiyo anaombwa airejeshe Makao makuu ya Klabu hiyo.

Ameyasema hayo akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu ya Yanga ambapo ameeleza kuwa wametoa taarifa sehemu husika Ili waweze kutengenezewa Ngao ya Jamii nyengine kwakuwa aliyetengeneza ni Mtanzania.

Your browser is not able to display this video.
 
Hawa jamaa wanachekesha kama sio viongozi wa timu yako...

Kombe linaibiwaje likiwa garini?

Wewe huwajui wabongo? Wanajifanya wanashanguria mwishowe wanasepa nalo.

Kuna kipindi Kitaa kulikua na Ligi Ya Kata, Ikizaminiwa na Diwani.

Siku ya Finally, baada ta Diwani kugawa zawadi kwa Mshindi, Wakati wa kushangilia wananchi wakambeba Diwani juu juu uwanja mzima.

Kumbe kuna msenge ana msearch mfukoni akasepa na simu na Pochi ๐Ÿคฃ

Kesho yake jioni wananchi wakamkamata mpaka kwa Diwani
 
Kweli bongo mmeshindikana๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œ๐Ÿพ๐Ÿ™Œ๐Ÿพ

Ila siyo mbaya aliyeiba ni mwanayanga mwenzao. Kaamua akaitunze nyumbani kwake
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 

Watanzania Njaa Kali Sana. GSM weka dau la Bilioni 10 watu wakuletee Kombe mlangoni kwako kesho asubuhi

Mbona Mzee GSM aliweka mzigo CCM wa Bilioni 10 na YANGA wakaweka Milioni 100

KWANINI YANGA msiweke Milioni 100 Kombe liweze rudi Jangwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ