Eng Hersi Said Simamia Misingi ya Kanuni na Sheria za Mpira. Mshauri Rais Samia asivuke Mipaka

Mama yeye hajaingilia katoa '' OMBI" Sasa kama mnaoubavu Wa kukataa la Rais fanyeni hivyo. Kifupi mbwa anatakiwa kula mbwa. Kichwa kiko GSM mama Kasema hatambinya binya. Sasa Hersi achague kumvimbia Rais au kuheshimu. Over
 
Hivi kweli dogo kawa huru na ni msimu wa usajili [emoji3][emoji3] Ubwabwa umewagharimu Uto
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ubwabwaa una balaaa lale mjinii.
Famchezo nn, uwiiiih
 
Mbna walirudisha zile 112M baada ya kuingiziwa kwa ACC yao?? Au huna kumbu kumbu??

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] imeishaaaa hiyooooo
Shidaa ya yanga roho mbayaaaaaaaa
Wana uchawi mwingi sana
 
Siku nyingine wakiitiwa ubwabwa tena Ikulu hawaendi,wamejifunza vya bure ni gharama pia [emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hivi unajua mama mjanjaa sanaa, akasisitiza anasubiri mrejeshoo wa suala la Fei toto. Woyoooooooo
 
Feisali yuko huruu kuanzia jana usiku, bado kuweka wazi kwa umma tyuuh. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Utashangaa simba watakavyomdaka fastaaaaaa. Yanga wamepoteza mchezaji kizembe kweli alafu mambo ya chuki zisizo na msingi ukimuangalia herisi anavyojifanya mpole nyoooo kumbe kashetani tu
 
Wakati mnafakamia pilau mliona raha? Rais wa Tanzania ni kama sheria. Halafu kama mmiliki wa sasa wa Yanga GSM anaweza binywa na akatoa mlio je huyo Hersi mwajiriwa wa Yanga ni takataka gani kum-challenge Rais? Halafu hata Rais alishaona upumbavu wa Yanga kutaka kumkomoa kijana bila sababu za msingi. Yanga ni makatili sana kutaka kuua kipaji kinachotegemewa na nchi nzima. Nampongeza sana Mama Samia kwa kuwaamrisha Yanga waache upuuzi.
 
Ndiyo muelewe kwa nini FIFA inakataza serikali kuingilia mambo ya mpira wa miguu. Mlikata miuno kupewa ndege,mamilioni ya magoli na kualikwa kwenda kufakamia pilau la ikulu. There is no free dinner.
Kula chuma hicho
 
Sisi lengo ni yeye atoke hapo Utopoloni iwe kwa sheria au kinguvu.

Nyinyi ndio mkajidai wasiamamia misingi eti mnalinda brand.

Haya sasa Raisi katoa amri hakuna cha brand wala brandina hapo ni utekelezaji tu.
Ningekuwa mimi nisingetaka mbeleko maana wanaotafuta mlango tofauti na mamlaka husika basi huyo hana haki na ni tapeli hivyo madai yake ya kimkataba ni batili.

Mfano wewe upewe kesi ya kubaka au Wizi na ushahidi unao kuwa wewe si mhusika sasa utakubali vipi ionekane umesamehewa kimagumashi kea shinikizo na sio kisheria hapo hamuoni dosari ?
 
Watu wisely washaelewa kuwa nyinyi ndio wenye matatizo na ndio maana Raisi hajamfata Feisali kumuambia arudi Yanga kama ambavyo TFF waliamua.

Kwanza unatakiwa ujue lengo ni nini na sio niia gani iliyotumika kufikia lengo.

Lengo ni Feisali aondoke Yanga, njia yeyote itayotumika kwetu sisi ni malengo
 
Kwani wana akili sasa hapo utopoloni?
 
Reactions: Tsh
Kuwaambia wakae wamalize hiyo issue ni kupeleka pressure?
Kwani yeye hana uhuru wa kutoa maoni yake?
 
Kama Yanga ndio wenye matatizo mamlaka ingeamua kwa vile ni jambo la kisheria , sasa wewe unaweka personal views kuamua jambo la kisheria kitu kama hiko hakipo kwa watu wenye busara zao.
 
Kama Yanga ndio wenye matatizo mamlaka ingeamua kwa vile ni jambo la kisheria , sasa wewe unaweka personal views kuamua jambo la kisheria kitu kama hiko hakipo kwa watu wenye busara zao.
Kama ni jambo la kisheria na Hersi anaifata basi angemuambia Raisi kuwa lile ni jambo la kisheria tuone inakuwaje.

Usizungumzie kitu kuhusu busara ambazo huko nyuma zilijatibu kutumika na hazikuweza kuleta matunda yeyote.

Tuone hiyo sheria yenu ina nguvu kiasi gani kwenye agizo la Raisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…