Tariq f
JF-Expert Member
- Dec 11, 2021
- 233
- 347
Habarini Wanajangwani wenzangu.
Tunajenga kikosi cha aina gani!?
Kwanini kimataifa kila siku iwe kilio kwetu!?
Hapana. Tunahitaji mabadiliko ndani ya klabu yetu, kuanzia uongozi, wachezaji mpaka benchi la ufundi. Tunahitaji kikosi kitakachotoa upinzani kwa timu za kimataifa na si kutamba Ligi Kuu peke yake.
Kuna muda najisikia wivu ninavyoona wenzetu Simba wanavyotinga mpaka hatua za robo fainali michuano ya Africa, lakini nabaki sina namna kwa sababu Yanga niliirithi mwenyewe kwa baba angu.
Ila ni mpaka lini tutaitwa majina ya kukera na wapinzani huko mitaani kama wamatopeni, utopolo, chura fc, wazee miamala n.k? Yaani kila siku yanga ndiyo iwe timu ya kubinuliwa na wapinzani kimataifa. Hapana, imetosha sasa!
Naanza kuamini viongozi mnafanya tabia chafu za kununua mechi za Ligi Kuu, maana haiwezekani michuano ya nje ndiyo tushindwe ila ya ndani tumudu.
Kwa pamoja tushirikiane kuutoa huu uongozi madarakani, ikiwezekana Wanajangwani tusiende uwanjani, maana ndiyo kunapowapa viburi.
Tunaomba mtuachie timu yetu,
Daima mbele nyuma mwiko