Eng. Hersi, Senzo na Kocha Nabi tunaomba mtuachie klabu yetu!

Tariq f

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2021
Posts
233
Reaction score
347
Habarini Wanajangwani wenzangu.

Tunajenga kikosi cha aina gani!?
Kwanini kimataifa kila siku iwe kilio kwetu!?

Hapana. Tunahitaji mabadiliko ndani ya klabu yetu, kuanzia uongozi, wachezaji mpaka benchi la ufundi. Tunahitaji kikosi kitakachotoa upinzani kwa timu za kimataifa na si kutamba Ligi Kuu peke yake.

Kuna muda najisikia wivu ninavyoona wenzetu Simba wanavyotinga mpaka hatua za robo fainali michuano ya Africa, lakini nabaki sina namna kwa sababu Yanga niliirithi mwenyewe kwa baba angu.

Ila ni mpaka lini tutaitwa majina ya kukera na wapinzani huko mitaani kama wamatopeni, utopolo, chura fc, wazee miamala n.k? Yaani kila siku yanga ndiyo iwe timu ya kubinuliwa na wapinzani kimataifa. Hapana, imetosha sasa!

Naanza kuamini viongozi mnafanya tabia chafu za kununua mechi za Ligi Kuu, maana haiwezekani michuano ya nje ndiyo tushindwe ila ya ndani tumudu.

Kwa pamoja tushirikiane kuutoa huu uongozi madarakani, ikiwezekana Wanajangwani tusiende uwanjani, maana ndiyo kunapowapa viburi.

Tunaomba mtuachie timu yetu,
Daima mbele nyuma mwiko
 
Pole sana Senzo mbona alishasepa!

Tatizo hamuishii kununua mechi tu,ila na wachambuzi kwa ajili ya propaganda na uongo uongo wa mwingi.

Ingekuwa leo ni mwamuzi wa hapa kwetu,angelaumiwa Karia sana.

Lakini hizi ndiyo mechi za kimataifa
 
Endeleeni kujifunza kwa Simba SC, na muache zile kelele za unbeaten hapa nyumbani, huko nje ndio kuna mpira wa mabingwa ambao Simba anajua kuucheza.
Samahan hv timu yetu ya simba inamakombe mangapi ya kimataifa
 
Kwani matokeo si suluhu ya 1 - 1?

Ligi ya bongo imenunuliwa mpaka hapo AGOSM atakapokatwa mkia kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.

Kimataifa, pengine nguvu ya shilingi yetu ndo inatuangusha, wakitaka $1,000,000 tukigeuza kwenye madafu tunaona mbona ndo kiasi hicho hicho tulichotumia kuwalipa tifutifu kutuuzia misimu miwili, wao wanatuchaji kwa mechi 2 tu, tunaona wakafie mbali, bora kumlipa Tola tupate heshima kwenye debi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…