Nashangaa sana na watu, kama serikali imekaa kimya haikufanyi wewe usjichukue tahadhari wewe ndio kichwa cha family panga mambo yako na sheria zako ya serikali waachie wenye mamlaka. Hata kama serikali itasema ndio watu hawatakufa?? mbona jamii za ki asia hata wazungu wanavaa mask kwani wameambiwa na mtu? hakuna sheria imekataza mtu kuvaa mask au kuepuka mikusanyiko.
Tatizo labda ni ile hali ya serikali kuacha mikusanyiko mikubwa kama clubs watu wanahemeana na au matamasha ya muziki hilo jukumu lao. Wewe jiangalie kama wewe na family yako jikinge, sio kwamba huwezi kupata unaweza kupata ila umekuwa umefanya juhudi kujikinga mengine tumuachie Mungu.
Tatizo ni kuwa serikali imewaaminisha the illiterate mass kuwa ugonjwa haupo.
Unajilinda vipi wewe na wapendwa wako wote kwenye hilo rojo? Unajilinda vipi kwenye mwendo kasi, dala dala, mabasi, ferry, TRA kwenye makadirio ya nyongeza za kodi nk?
Tusidanganyane haipo namna ya kujikinga binafsi katika rojo hili tulilomo.