Huyu muanzisha thread hana hoja, hata wahandisi ambao sio direct kutoka UDSM waliopo kwenye soko la Tanzania indirect wametoka UDSM, hii ni kwa sababu wengi wa walimu waliowafundisha kama sio wote wamesoma na kupitia UDSM.
Vyuo vyenye course za Engineering hapa Tanzania ambavyo wahandisi wake wako sokoni ni UDSM wenyewe, DIT, MIST kwa kiwango kidogo sana na St. Joseph, na ukitaka kujua hili kuwa majority ya walimu wa wahandisi hawa ni UDSM product tafuta prospectus za vyuo nilivyovitaja then angalia hao wahadhiri walisoma wapi.
UDSM/pCET/COET ina mchango mkubwa katika fani za uhandisi hapa Tanzania, huwezi kusimama kirahisi kwa maneno ya kulishwa pasipo kufikiri na kuanza kuihusisha na maovu yanaendelea hapa kwetu kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Kwa ujumla bado watalamu wetu kutoka vyuo tajwa hapo juu wanafanya vizuri sana, ila Tanzania ya sasa siasa, jeuri ya pesa, nk vitatupeleka pabaya.