Moja ya sababu inaweza kuwa gari lako limetembea saana (lina km nyingi) na maintenance haikuwa nzuri saana, au at some point, lilikaa muda mrefu bila kutumika. So inawezekana kuna oil leak kutokana na kwamba oil seals zimezeeka (maana gari lako lina zaidi ya miaka 20), japo hii ungeweza kuigundua kirahisi sababu asubuhi ungekuta kuna oil imemwagika chini, pia linaweza kuwa linachoma oil. Hii inasababishwa na shida ya valves, au piston rings au cylinders zimechoka na zimetanuka.
Huwa unaona moshi wa blue kwenye exhaust? Mafundi wengi watakushauri kufanya overhaul ya engine, ila mie nitakushauri kununua engine used ufunge, itakuwa gharama na usumbufu kidogo kuliko kufanya overhaul, unless wakute ni tatizo tofauti. Kama ni seals, hizo zinapatiakana, unabadilisha tu na unasonga mbele. Pia jenga mazoea ya kuweka oil filter na oil nzuri na kuepuka kujaza oil kupita kipimo cha mtengenezaji wa engine.