engineering gani ninzuri apa Tanzania?

shareef95nes

Senior Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
108
Reaction score
16
natambua kama kuna careers nyingi za engineering,je, kati ya hizo nyingi ipi ni nzuri kwa hapa Tz?
 
Engineer Zote ni Nzuri na zote ni Mbaya.. Zote zinaweza kumtoa Mtu Na zote zinaweza kumuadhiri Mtu vilevile. Hakuna laini.

Ukitaka kusoma, kufurahia Na kuwa mhandisi unayeipenda Kazi yako Na Kazi inakupenda lazima utambue wazi Kwamba Uhandisi ni Kipaji. Ni kipaji anachoanza nacho Mtu tokea anazaliwa, anakua nacho Na kukitumikia. Masomo Na elimu anazo kutana nazo Kwenye makuzi yake huimarisha(sharpens) na Kukuza ufaham wa kile kipaji alichonacho.

Wale ambao hawana vipaji Na hujiunga Na fani nguli ya uhandisi ndio hao kila kukicha wanalialia, wanalalamika ugumu wa Kozi, wanaibia paper mwanzo-mwisho Na Bado supplement exams zinawafuata all study years Na wakibahatika kumaliza Kozi Basi wanaruka Na Gpa mbaya Na kuishia Kuuza mafuta Kwenye vituo au kufanya Kazi NJE ya fani zao. Maneno haya yanaweza kuwa chungu sana Kwa wahandisi wengi wanaosoma Na waliosoma but ndio UKWELI WA MAMBO. Tusiwahadae vijana wakakimbili fani watazozijutia, UHANDISI NI KIPAJI.

Kama wewe unadhani una kipaji Chochote mwenyezi Mungu amekujaalia, labda unapenda sana ufundi, au mzuri wa kuchora, una kipaji Cha Hesabu(hesabu SIO elimu ya kawaida ni kipaji), au una kakipaji kokote unakodhani kanatikana Na uasili wako Basi unaweza kuchagua kusomea hii kitu. Fani ya Uhandisi ni Pana sana inategemea Na unachodhani ni kipaji chako. Sasa siwezi kujua Asili ya kipaji chako nikakushauri. But awali kulikuwa Na Major 3 engineering Course Baadae zikawa Nne Leo ziko nyingi hapa naongelea ilivyokuwa Faculty of Engineering -UDSM, Baadae CoET (College of Engineering and Technology) ambapo ziko Fani Tele zenye walimu makini waliobobea Kwenye hii makitu. Sina bahati ya kujua sana habari Za vyou vingine.. Ni hayo yangu
 
POLITICAL ENGINEERING!
inalipa sana hii!
2015 sio mbali mkuu!
 
nashukuru umejibu vizuri sana, kama unakipaji cha hisabati bora kasome umeme, ila inabidi ujipange sana, hata ukipata degree yako yote yanaweza kutokea, ukafanikiwa mapema au ukachelewa. lakini kama unamapenzi na fani huwezi kukata tamaa, mi ni mhandisi wa umeme, nimehitimu miaka kumi iliyo pita mpaka sasa bado sijayapatia vizuri, ila naelekea kwani nimefungua kampuni yangu nitumai ndani ya mwaka au miwili mambo yanaweza kwenda vizuri. bora ujue ukweli kabla ya kuamua



 
natambua kama kuna careers nyingi za engineering,je, kati ya hizo nyingi ipi ni nzuri kwa hapa Tz?
1)civil engineering
2)mechanical engineering
3)agricultural engineering and related fields
4)electrical engineering
5)computer engineering
 
Saivi ambayo ni deal ni petroleum engineering komaa upige hiyo saivi mafuta na gesi ndio big deal makampuni mengi yanakosa watanzania wa kuwaajiri course hii ipo pale UDOM jaribu kufuatilia.
 

wewe jamaa lazima utakuwa Muhaya tu!
 
civil engineering ndio mpango mzima kozi nyingine hizo za engineerin upuuzi mtupu
 
Eng.y.bihagaze kweli umeniwacha hoi
nakubali hesabu ni kipaji pia sio somo la kawaida asee:A S angel:
 
Last edited by a moderator:
ukisema kozi ya engineering ambayo ni nzuri hapa tanzania ..
swali lako binafsi ntalitazama kwa mapana kidogo kwa maana hii
uzuri kwenye kipato ..?
uzuri kwenye utendaji kazi ..?
uzuri kwa maana ya urahisi wa kupata ajira..?
uzuri kwa maana maono ya watu kwenye jamii ..?
binafsi mimi ni mhandisi wa umeme na kwa dhati ya moyo napenda sana hii fani yanu pamoja na changamoto zilizopo ndani ya nchi yetu .. ni kozi nzuri ina wigo mpana wa ajira na pia unaweza kufanya kazi kwenye nyanja nyingi sana (viwanda, makumpuni ya uzalishaji umeme na usambazaji(tanesco), wakandarasi wa umeme, wahandisi washauri, nk)
kuhusu kipato bado hii fani haithamini sana .
jambo jingine ni ubunifu kwa wahandisi wengi ni rai yangu kwako na kwa vijana wengine wanataka kusoma fani za uhandisi/engineering wajitahidi kuwa wabunifu pamoja na changamoto nyingi sana zilizopo nchini mwetu ambazo watakutana nazo.

pili kozi nyingine za uhandisi kwa binafsi yangu nazoona nzuri kwa mtazamo mpana ni CIVIL, MECHANICAL, TELECOMS , COMPUTER ENG(ingawa kwetu bado inakabiliwa na changamoto nyngi hasa kukua taratibu kwa teknolojia) MINING , PETROL ENG(ingawa ni changa hapa kwetu ila ni fursa kwa kuwa tuna rasimali ya mafuta na gesi )

ANGALIZO: UHANDISI/ENGINEERING NI FANI AMBAYO INAKUHITAJI KUKAZA BUTI PIA UWE MTU MWENYE NIA YA DHATI VINGINEVYO UTAISOMA NA UTAIPRACTISE UTAIHAMA NA KUWA UMEPOTEZA MUDA WAKO BURE
MTU MWENYE UWEZO MZURI WA PHYSICS NA MATHS ANAWEZA KUSOMA ENGINEERING YEYOTE..
 
Habari ya mujini sasa hivi ni Chemical Engineering... Km ni mwenyeji wa Mtwara umeshanisoma!
 
Petroleum Engineering ndio mpango mzima kwa Tanzania,Africa na Dunia ya sasa.Usichezee nafasi hii,make a better use of it!!!!
 
POLITICAL ENGINEERING!
inalipa sana hii!
2015 sio mbali mkuu!

Habari ya mujini sasa hivi ni Chemical Engineering... Km ni mwenyeji wa Mtwara umeshanisoma!

Petroleum Engineering ndio mpango mzima kwa Tanzania,Africa na Dunia ya sasa.Usichezee nafasi hii,make a better use of it!!!!
.
.

Mchezo mgumu Na hatari watu wengi huwa tunachagua baadae zetu masomoni Kwa kuangalia kioo Cha soko la ajira Leo.. Hii ni Hatari sana sana.. Hii humfanya mhandisi ajiandae kuajiriwa, hapo atafurukuta amalize kozi Kwa namna iwayo yote. Anajitengeneza kuwa job seeker . Hawa ma job seeker wengi ni Wahandisi wasiojiamini. Hana ubavu wa kufungua kampuni ya alichosomea. Ukimsikia mhandisi Wa namna hii ana kampuni Basi ni ya usafi au supplier, au nyingine ambayo iko masafa marefu mbali Na alichosomea. Narudia tena Uhandisi ni Kipaji, kama unacho nenda kikikomaze uwe mhandisi mwenye confidence Na Kazi yako.. Kusomea uhandisi tu ni zaidi ya Ajira. Kazi huzitafuti zinakutafuta.. I am happy to be an Engineer..

DUNIA yote watu wakiamka wanamtegemea Mhandisi awaanzishie siku Na kuimaliza.
 
Hakuna jambo la kipuuzi kama kuichagua elimu,

elimu haichaguliki.

Elimu ni kipaji/karama.

Elimu ni bidii.

Engineering kwa ujumla wake ni maarifa yanayotokana na juhudi,ushirikiano,nidhamu,ubunifu,uvumilivu na kupenda unachoamini katika mazingira yaliyopo pasipo kuwabughuzi wenzako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…