Wakuu kwa muda mrefu nimekuwa na passion ya kuijua vizuri sana hii lugha ya kiingereza km hyu member wa humu anayeitwa kiranga nitumie njia gani niweze kui master vizur hii lugha????
Habari mkuu!! Mm ni mmoja kati ya watu wavivu sana katika kuchangia mada mbalimbali katika majukwaa mbalimbali kama jinsi nilivyo mvivu katika kusoma nyuzi katika katika majukwaa mbalimbali pia lakini hapa naomba nijitahidi japo kwa uchache!!
Ili kujifunza Lugha yeyote ile sio tu Kiingereza hata kimatumbi yapo mambo makuu ya Msingi ya kuanzia katika Kujifunza Lugha Husika!! Kwanza Jifunze SARUFI(Grammar/Syntax ya hiyo Lugha) hapo Utajifunza Kuhusu Sentensi na miundo anuai ya sentensi, maneno na usanifu/ufinyanzi wa Maneno mapya (Lexis), utasoma "Stylistics" ya Lugha hiyo yaani Matumizi ya maneno katika Muktadha(Contexts) mbalimbali na kadhalika, sarufi ni pana zaidi ya haya maelezo machache niliyoandika hapa!!
Vivyo hivyo utajifunza kuhusu Matamshi (Phenology) ya Lugha husika katika muktadha huu ni Kiingereza kwa hiyo!! Hapa utajifunza Kiingereza kina vitamkwa vingapi (Phonemes) yaani Vowels na Consonants na utakisoma na kukitamka na utaangalia jinsi kinavyotamkwa!! Vowels ni phoneme zote ambazo mtu hutamka bila kuhitaji kugusanisha lips zake ili kuzitamka wakati Consonants mi phoneme zote ambazo mtu hawezi kuzitamka pasipo lipsi zake kugusana!!
Kwa kuongezea tu Utasoma Intonation na namna za Kuwekea Mkazo silabi, Katika Kiswahili huwa mkazo unawekwa kwenye Silabi moja kabla ya Mwisho kwa mfano neno chakula lina silabi tatu Cha+Ku+ la hapo silabi ambayo itatamkwa kwa mkazo ni KU na zilizobaki ni sauti ya kawaida tu!! Sasa hiyo inakwenda hivyo kwa maneno yote ya Lugha ya Kiswahili wakati katika LUgha ya Kiingereza ni vigumu kubashiri kwamba mkazo utakuwa katika silabi ipi hivyo mtu hulazimika kujifunza neno moja moja!! Kwa msingi huu ukiangalia maana ya neno la kiingereza kwenye kamusi utaangalia pia stress inakaa wapi na katika context ipi neno hilo hutumika!!
Wengi wetu tunaweza kujitahidi kwenye sarufi lakini huwa hatuyapi umuhimu matamshi!! Unapokuwa hautamki vizuri maneno unampa kazi sana Msikilizaji kuelewa maana yako na hivyo kuathiri hata Utamu wa mawasiliano maana kila kutakuwa na maneno kama " I beg your pardon" " Could u pls explain" "come again" etc
Kuhusu pa kujifunzia nadhani sehemu nyingi zipo moja kati ya Sehemu nzuri kama upo Dar ni British Council Samora avenue.mkabala na Mgahawa mashuhuri wa Steers!! Tatizo bei zao ni za juu kiasi unaweza kununulia garimoshi!!
Kuangilia kazi za sanaa za Kiingereza, kusoma vitabu na Ujasiri wa kutokuogopa Makosa ya Kisarufi na Kimatamsho wakati wa kuongea ni Moja kati ya vitu vitakavyokuongezea ubabe wa Lugha hii adhimu!!
Ukidhamiria Unaweza, anza kuchukua hatua sasa, inalipa kujua kiingereza vizuri!!! 😜😜😜