Asante.
Halafu kwa kuwa na mimi najua najifunza bado, siwezi kuacha kuandika kiingereza changu cha kuunga unga kwa kuhofia watu watanisema vizuri au kwa kutaka sifa. Huko nyuma sikuwa hivyo, kwa nini nianze sasa?
Nikifanya hivyo nitajinyima nafasi yangu ya kujiendeleza zaidi.
Nakumbuka tukiwa shule Tambaza tulikuwa tunaongea kiingereza na rafiki zangu mpaka kwenye mabasi, kwa kuwa tulikuwa tunajifunza. Ilikuwa kama utani lakini tulikuwa tunapata mazoezi ya kuongeleshana kiingereza bila kujali watu wengine watafikiri vipi. Wengine wakatuona tunajidai, walioelewa wakaona vijana wanaweka jitihada ya ziada nje ya madarasa kujifunza kiingereza.
Hakukuwa na cha ajabu, after all hizi habari muda huo kwa vijana fulani wa mitaa fulani zilikuwa za kawaida kama jando kwa makabila fulani. Vijana waliozibukia hip hop, sitcoms, comedies, international news, novels, non fiction books etc kuongea Kiingereza, hata kama ni cha kujifunzafunza tu, haikuwa cha ajabu sehemu fulani.
Nakumbuka kuna siku tukakutana na mzee mmoja wa wizara ya elimu alikuwa impressed na maongezi yetu mpaka akajichanganya kwenye mazungumzo yetu, kiingeteza. Mzee anashangaa nimeshika kitabu cha Carl Sagan ananiuliza kama nakielewa. Nikamwambia nakielewa vizuri na hiki cha pili sasa nasoma. Akatuambia "kila mara nasikia mambo mabaya kuhusu shule yenu lakini nyinyi mnaonekana smart tu". Tukamwambia mambo ya samaki mmoja akioza yanatuharibia wote.
Najikuta kwamba kadiri ninavyozidi kujisomea, nakusanya msamiati mkubwa zaidi, na kadiri ninavyokuwa na msamiati mkubwa zaidi, nautumia zaidi. Mara nyingine bila ya kupanga.
Natoa historia zote hizi ili wanaofikiri kuna cha kuiga wajue kufika hapa - ambapo mimi.napaona bado chini sana, lakini.wengine wanaona panatamanika sana tu- haikuwa.kazi ya mara moja. Ni utamaduni uliojengeka tangu niko mdogo naangalia comics za Archie na Tintin, najaribu muelewa story kwa kuangalia picha, halafu ukweli kwamba sijui kusoma kiingereza na nashindwa kuelewa story yote ukaniuma sana na kunisukuma kujifunza kiingereza mwa njia zote, kuanzia kamusi.mpaka kujifua kwa maongezi.
There is a point when one has to decide to be a Bodhisattva or a Buddha.
One shouldn't be blamed for either decision.