English Premiership: 2010-2011

Abdulhalim

Platinum Member
Joined
Jul 20, 2007
Posts
17,215
Reaction score
3,076
Nduguzanguni, wapenzi wa kabumbu..

Karibu katika ukumbi wenu muupendao ikiwa leo tarehe 15 mwezi wa nane, mwaka 2010, ni siku ile ambapo twakata utepe wa hiki kinyang'anyiro cha ligi bora zaidi kwenye sayari hii kama sio kwenye galaxi tuliyomo.

Basi wale wapenzi wenye mahaba na thread za vilabu sio mbaya mkichangia na huku, wajameni!!


Ratiba ya ufunguzi ni kama ifuatavyo:

 
Kama kawaida ya thread za michezo, utabiri ni jadi, basi sina budi kusema ni wapi naweka shilingi yangu mapema.

Mwaka huu au kwa hakika zaidi msimu huu, bila ubishi ubingwa utaondoshwa kule darajani, na kazi kubwa ya ushindani itabakia ktk timu za Manchester, yaani United na City, lakini mwisho wa siku nataraji Mashetani Wekundu wataibuka kidedea. Nafasi ya 3 itakuwa ngumu kutabiri kwa sasa, lakini Chelsea ipo mbele ya Liverpool, Arsenal, Spurs na Everton, natumai hawatajivunga.

Natabiri kuwa na ligi ya msisimko mkali zaidi mwaka huu kuliko mwaka jana, na tuombeane uzima kwetu washabiki na wachezaji tuwaombee uzima na afya, haswa ikikumbwa hawa ndio wanatufanya tuwe na kitu cha kusimulia.
 
Kwasababu mpira unadunda....Karata yangu nairusha kwenye Bwawa La Maini.

Najua wengi wataniona kreze lakini ndio hivyo tena, kila mtu ana chembe chembe za Sheikh Yahya Hussein wake.

Kwa kuanzia na kwa msisitizo ; Kesho Arsene Wenger anapelekewa kilio...........Go Liverpool Go!
 

Bingwa,

Unatabiri kuhusu mechi au ubingwa?
 
Ubingwa mzee. Najua ntaonekana kreze lakini mpira unadunda na msimu huu lazima kombe litue Anfield!

Hapa tatizo sio kuenekana kreze.....ila tayari wewe ni kreze!
Wachambuzi wengi wanaipa ze bluz nafasi ya kutetea kombe....
Mi naina Man U ikiwa imebeba kombe lake hapo Mei 2011!:A S soccer:....Man U are going for # 19, remember?

BTW: Msimamo wa ligi ni huu kwa sasa...

1 Arsenal
2 Aston Villa
3 Birmingham
4 Blackburn
5 Blackpool
6 Bolton
7 Chelsea
8 Everton
9 Fulham
10 Liverpool
11 Man City
12 Man Utd
13 Newcastle
14 Stoke
15 Sunderland
16 Tottenham
17 West Brom
18 West Ham
19 Wigan
20 Wolves

Ze gunaz oyee...
 
Spurs na City wapo uwanjani hivi sasa, mpambano mkali kwelikweli.

Dk 14 bado 0:0
 
Ubingwa mzee. Najua ntaonekana kreze lakini mpira unadunda na msimu huu lazima kombe litue Anfield!
Liverpool bado wanajipanga msimu huu..sioni uwezekano wa wao kuwa mabingwa.
 
Hart with a string of A-game saves. duh ni noma.
 
Hart anastahili kuwa kipa # 1 wa England.
 
City hawa wachezaji iliowasajili sidhani kama wataiweza EPL, mhh..
 
Mtanange umefikia nusu, bado milango haitaki kufunguka. Lets wait for the 2nd half.
 

Teams letter that begins with "W" are going to struggle this season and possibly three of them relegated (West Brom West Ham Wigan Wolves )
 
Naona kumekucha n the wait is over.sawa sawa kabisa tutaendeleza jadi ya kutambiana kama kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…