ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Mtangazaji huyu wa TBC1 Enock Bwigane yaonyesha ni kijana mchapakazi anayeipenda kazi yake vyema na staili ya utangazaji wake wa taarifa za michezo ni kama ya watangazaji waandamizi akina Juma Mkamia. Hata hivyo, jambo moja ambalo pengine anaweza kuwa tofauti na watangazaji wengine hasa kwenye habari ni ile staili yake ya kuikazia macho "screen", kujiinamishainamisha, kujitikisa tikisa na kuzungushazungusha shingo kushoto na kulia kana kwamba hawezi kuona kwa kwa urahisi kila anachokisoma akiwa studio... kama si mikogo, .labda maandishi yanakuwa mbali na analazimika kuyafuatilia kutoka kwa kuyakazia macho...
Otherwise, yupo juu Kijana!!!