Mangi Meno
JF-Expert Member
- Jun 26, 2024
- 292
- 895
Sijasoma huu ushuzi wako kwani Biblia inasema Mpumbavu husema moyoni mwake kuwa hakuna Mungu. U mpunbavu tu dogo na huna ujuacho humu duniani.Huyo Mungu hajawahi kuwepo na wala hayupo kujiongelea na kujitetea mwenyewe.
Mnahangaika sana kutetea kitu ambacho hakipo na wala hakijawahi kuwepo kujidhihirisha chenyewe na kujitetea.
Sasa wewe unataka watu waendelee kuamini fiction stories za uwepo wa huyo Mungu?
People ain't fool anymore, The age of believing is over. We are in the age of knowing.
Wewe endelea kuamini Matango pori yako uliyo aminishwa kuhusu huyo Mungu.
Hususani wewe ndio jishetani jenyewe.Na kwanini awe mweusi hii dharau, kwamba sisi weusi ndio mashetani? π€£π€£π€£
Pia amesema kwenye mbingu ya tatu upande wa kaskazini kulikuwa na moto ambapo ndani ya huo moto watu walikuwa wakichomwa, sasa wanachomwa kwann wakati tulikubaliana kiama bado hvy watu wametengwa mahali kusubiri hy hukumu ya moto πNa sehemu inayounguza yenye moto mkali na muda huo huo kuna barafu kali.!! π
Sasa barafu si inayeyuka sababu ya moto??!
Jamani hivi vitabu vina mauongo mengi.
Au Enoko alikuwa kwenye njozi?
Sijasoma huu ushuzi wako kwani Biblia inasema Mpumbavu husema moyoni mwake kuwa hakuna Mungu.
Hujui hata kuandika.U mpunbavu β
tu dogo na huna ujuacho humu duniani.
Naona unatumia nguvu kweli kutulazimisha tupinge uwepo wa Mungu. Pole hutupati ng'ooooooHujui hata kuandika.
Rudi chekechea kajifunze kuandika kwanza.
Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani ulivyo Bogus.
Tabularasa.
una amini dunia sababu unaiona.π€π€π€
Myth
Kwanza, aliwaona je wakati ni giza ?Kwanza kulikuwa na giza kubwa, giza ambalo duniani hakuna lakini pia akawaona malaika wakiwa wameningβinizwa kwa staili ya kunyongwa, kufungwa na minyororo huku wakitazamwa na wengine waliokuwa wamesimama.
Hapa ngoja nikwambie kitu kimoja. Hao malaika hawakuwa kama hawa tunaowasoma sehemu mbalimbali, hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika. Yaani pamoja na kunyongwa huko, hawakuwa wamekufa.
Hii inapinga sayansi au ni kwasababu sio duniani,π€Moto haukuwa ukiyeyusha barafu zile, watu walipigwa na vitu vyote hivyo viwili kwa wakati mmoja.
π€Kitabu cha enoko kina ukweli ndo maana kilifutwa.
Nimesoma biblia kidogo ila hichi kitabu kinaenda kinyume na biblia kabisa kwa upande wanguSEHEMU YA 02
Enoko anaendelea kusema kwamba malaika wale wawili wakamchukua na kumpeleka kwenye mbingu ya pili na huko akakutana na haya mambo.
Kwanza kulikuwa na giza kubwa, giza ambalo duniani hakuna lakini pia akawaona malaika wakiwa wameningβinizwa kwa staili ya kunyongwa, kufungwa na minyororo huku wakitazamwa na wengine waliokuwa wamesimama.
Hapa ngoja nikwambie kitu kimoja. Hao malaika hawakuwa kama hawa tunaowasoma sehemu mbalimbali, hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika. Yaani pamoja na kunyongwa huko, hawakuwa wamekufa.
Enoko akauliza hawa ni akina nani? Akajibiwa kwamba ni baadhi ya wale malaika waliotaka kupambana na Mungu, wamechukuliwa na kuningβinizwa hapo wakisubiri hukumu siku ya mwisho.
Okay! Sasa hapa mimi kama Nyemo najiuliza kitu. Hawa malaika wataonekana tena mbingu ya tano, na wengine watatu walishushwa duniani. Swali ninalojiuliza ni moja. Kwa nini Mungu aliamua wengine kuwaacha mbinguni wakiteseka na wengine kuwashusha duniani? Ngoja tuendelee kwanza.
Wengine walikuwa wakimwambia Enoko: βMtu wa Mungu, tuombee kwa Mungu atusamehe!β
Enoko akawa anawajibu: βMimi ni nani mpaka niwaombee? Ni binadamu, nisiyekuwa na lolote lile. Kama nikiwaombea ninyi, nani ataniombea mimi?β
Baada ya hapo malaika hao wakamchukua na kumpeleka mbingu ya tatu. Huko akakutana na sehemu iliyotawaliwa na miti mingi mizuri iliyokuwa inamea matunda mazuri, ni kama bustani kubwa sana. Ilipendeza machoni mwake, ilikuwa ni sehemu ambayo ilimvutia kila alipokuwa akiiangalia.
Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na mti mkubwa wa uhai, ni kama ule ambao uliwekwa kwenye bustani ya Eden ambapo kama Adam na Hawa wangekula hakika wasingekufa.
Mti huo ulikuwa na muonekano wa tofauti na miti yetu ya duniani. Ulikuwa kama umetengenezwa kwa mafuta yanayoteleza lakini pia ulionekana kuwa na muonekano wa dhahabu.
Mti huo ulikuwa na uwezo wa kuotesha kila aina ya tunda unalolijua wewe na usilolijua katika maisha yako. Pia katika bustani hiyo kulikuwa na mito, si ya maji, bali ilikuwa ni ya asali na maziwa.
Na pia kulikuwa na mingine ambayo ilikuwa inatiririsha mafuta na mvinyo (wine). Ukiachana na hiyo, pia kulikuwa na malaika mia tatu ambao walikuwa wanaitunza bustani hiyo kubwa huku wakiimba kila wakati.
Kwa namna walivyokuwa wakiimba, Enoko anasema hakuwahi kuona ama kusikia mtu duniani akiimba kama hivyo.
Hiyo ndiyo sehemu ambayo watakatifu watakwenda na kuishi. Yaani kama wewe unatenda mema duniani, utakwenda kuishi kwenye bustani hiyo milele na milele.
Baada ya hapo, malaika wale wakamchukua na kumpeleka upande wa Kaskazini mwa mbingu ile ya tatu. Sasa huko ndipo wale wasiokuwa watakatifu walipokuwa wanahifadhiwa, ndipo jehanamu ilipo.
Enoko anasema alipopelekwa huko, aliogopa kwa kuwa ilionekana kuwa sehemu iliyojaa mateso makubwa ambayo hakuwahi kuyaona. Mwanga pekee uliokuwa ukipatikana ni wa moto ambao ulikuwa unaunguza kila kilicho humo.
Pia kulikuwa na mto, huu haukuwa wa maji bali mto wa moto. Kulikuwa na moto kila kona. Ila mbali na moto huo, pia kulikuwa na barafu kila sehemu. Yaani kulikuwa na mateso ya aina mbili ambayo watu walikuwa wakiyapata. Ya kuunguzwa sana na moto lakini pia ya kupigwa na baridi kali kiasi cha kuganda kabisa.
Moto haukuwa ukiyeyusha barafu zile, watu walipigwa na vitu vyote hivyo viwili kwa wakati mmoja. Watu walikuwa wakilia kwa majuto lakini pia walilia kwa sababu ya kiu kali waliyokuwanayo.
Pia kulikuwa na malaika asiyekuwa na huruma hata kidogo, aliyeogopwa, mwenye hasira na alishika silaha kubwa kwa ajili ya kuwatesea watu.
Enoko akasema: βHii sehemu imejaa mateso makubwa mnoβ na malaika akamwambia: βHii ni sehemu ya watu waliotenda maovu duniani, watu ambao hawakumuheshimu Mungu sehemu ya wachawi, waovu, wabakaji, wala rushwa, matapeli na wengineo.β
Baada ya kuyaona hayo yote, malaika wale wakanichukua na kunipeleka mbingu ya nne.
Itaendelea kesho.
Kuna sehemu nimekulazimisha upinge uwepo wa huyo mungu?Naona unatumia nguvu kweli kutulazimisha tupinge uwepo wa Mungu. Pole hutupati ng'oooooo
ππ Ni pre seasonPia amesema kwenye mbingu ya tatu upande wa kaskazini kulikuwa na moto ambapo ndani ya huo moto watu walikuwa wakichomwa, sasa wanachomwa kwann wakati tulikubaliana kiama bado hvy watu wametengwa mahali kusubiri hy hukumu ya moto π
Nasikia uvivu kukujibu mtu mwenyewe ushajiita wa hovyo.!!Hususani wewe ndio jishetani jenyewe.
Hizi hadithi km zile tulizokuwa tunadanganywa tukiwa watoto, mama akienda kujifungia tunaambiwa kaenda kununua mtoto baharini.!!Pia amesema kwenye mbingu ya tatu upande wa kaskazini kulikuwa na moto ambapo ndani ya huo moto watu walikuwa wakichomwa, sasa wanachomwa kwann wakati tulikubaliana kiama bado hvy watu wametengwa mahali kusubiri hy hukumu ya moto π
Ukiangalia kwa jicho la ndani, uwezekano mkubwa ni kwamba hata Mussa naye pia hakufa bali alichukuliwa akiwa mzima na Mungu mwenyewe, huku Mungu akiwa na sababu zake maalumu za kuwaambia Waisrael kuwa "Mussa mtumishi wangu amekufa"Ukisoma kwenye Biblia, ni watu wawili tu ndiyo ambao hawakuwahi kuonja mauti, nao ni Nabii Eliya na Enoko. Mungu hakutaka kuwaua, aliwatwaa na kuwapeleka mbinguni.
Kwamba Mungu aliwadanganya watu wake??Ukiangalia kwa jicho la ndani, uwezekano mkubwa ni kwamba hata Mussa naye pia hakufa bali alichukuliwa akiwa mzima na Mungu mwenyewe, huku Mungu akiwa na sababu zake maalumu za kuwaambia Waisrael kuwa "Mussa mtumishi wangu amekufa"
Ndiyo maana pale kilimani walipokuwa wapo na Yesu, Petro aliwaona Musa na Eliya