The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Katika kile kinachoweza kuwa muujiza wa kuokoa na kuboresha maisha ya maelfu ya watu duniani, chanjo ya mRNA ya Urusi iitwayo Enteromix imeonesha ufanisi wa asilimia 100 na usalama katika majaribio ya kitabibu. Hii inaweza kuleta matumaini makubwa katika kupambana na saratani sugu na hata kuizuia.
“Chanjo ya saratani ya Urusi, Enteromix, sasa ipo tayari kwa matumizi ya kitabibu,” imetangaza Wakala wa Shirikisho la Tiba na Baiolojia (FMBA).
Mkuu wa FMBA, Veronica Skvortsova, amesema chanjo hiyo ya mRNA imekamilisha kwa mafanikio majaribio ya kabla ya kitabibu, ikithibitisha usalama wake na ufanisi wa hali ya juu. Chanjo imeonesha matokeo makubwa katika kupunguza ukubwa wa uvimbe na kupunguza kasi ya ukuaji wake, na pia imeonekana kuwa salama kwa matumizi ya mara kwa mara.
Skvortsova aliongeza kuwa chanjo hii itatumika kulingana na mgonjwa, ikibuniwa kulingana na RNA ya mtu husika. Aina ya kwanza ya chanjo itatumika kutibu saratani ya utumbo mpana (colorectal cancer), huku toleo jingine likiwa linaandaliwa kwa ajili ya glioblastoma (aina ya saratani ya ubongo) na baadhi ya saratani za ngozi (melanoma), kulingana na taarifa zilizochapishwa na shirika la habari la Sputnik kwenye mtandao wa X.
Enteromix imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa inayofanana na ile iliyotumika kwenye chanjo za COVID-19. Inafanya kazi kwa kufundisha mfumo wa kinga ya mwili kutambua na kuharibu seli za saratani. Pia inatengenezwa mahsusi kwa kila mgonjwa mmoja mmoja.
Cha kuvutia ni kwamba, tofauti na matibabu mengine ya saratani kama vile tiba ya mionzi au dawa za sumu (chemotherapy), hakukuwa na madhara makubwa yaliyoripotiwa, na wagonjwa waliivumilia vizuri chanjo hiyo.
Hapo awali, ilifichuliwa kuwa Urusi ilikuwa imeanza majaribio ya kitabibu ya chanjo mpya ya saratani Enteromix ikihusisha washiriki 48. Dawa hiyo ilibuniwa na Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Tiba ya Mionzi cha Wizara ya Afya ya Urusi kwa kushirikiana na Taasisi ya Baiolojia ya Molekuli ya Engelhardt (EIMB) ya Chuo cha Sayansi cha Urusi (RAS).
Kuanza kwa jaribio hilo kulitangazwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi wa St. Petersburg (SPIEF 2025), uliofanyika kati ya Juni 18 na 21 kaskazini mwa Urusi. Tukio hilo, lililoandaliwa na shirika la Roscongress chini ya ofisi ya Rais wa Urusi, liliangazia maendeleo ya Urusi katika utafiti wa tiba na bioteknolojia.
Kwa mujibu wa ripoti ya MedPath, Enteromix hutumia virusi vinne visivyo na madhara kushambulia na kuharibu uvimbe wa saratani huku pia ikiongeza nguvu za kinga ya mwili kupambana na ugonjwa huo. Baada ya kupita kwenye miaka kadhaa ya majaribio, imeonesha ufanisi wa kupunguza kasi ya ukuaji wa saratani na katika baadhi ya visa kuiondoa kabisa.
Kwa kuwa majaribio sasa yamekamilika, hatua inayosubiriwa ni kibali cha udhibiti. Iwapo itapitishwa, Enteromix inaweza kuwa chanjo ya kwanza ya mRNA dhidi ya saratani inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja, jambo ambalo linaweza kubadilisha namna tunavyokabiliana na saratani — kuizuia, kuitibu na kuisimamia.