Kwanini nchi isizuie wananchi wake kwenda kuwa house maid huko nchi za kiarabu?
Na ikiwa wamekubali kupeleka watumwa huko badi waweke sharti la mtumwa kuwasiliana na ubalozi angalau mara moja kwa mwezi kumsikiliza, kama mazingira ya kazi ni mazuri, na treatment kwa ujumla, na iwe tayari kumsaidia kurudi nyumbani muda wowote kama mazingira ya kazi hayamridhishi kwa namna yoyote ile.
Wengi ninewasikia wakilalamika mitandaoni, baada ya kurudi nyumbani, kenya au Tanzania, kwamba mazingira kule siyo salama kabisa, manyanyaso, na mateso ni mengi.