Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
NALIA NGWENA huwa nashangazwa sana na wachambuzi wa kibongo wanaojiita wanaharakati na uchambuzi wao umejikita juu ya Simba sc na Yanga Sc utadhani hii nchi Kuna timu mbili tu ndiyo zinacheza.

Kuna bwana mdogo kaandika kwenye mitandao anaituhumu TFF kuwa imewadhurumu haki Yao hawajalipwa lakini wachambuzi MAANDAZI wapo kimya tu.

Mbona Suala la Feisal salum Wachambuzi mliongea sana na harambee ya kumchangia mlipitisha bakuli??

Wachambuzi wa Kitanzania mnachambua football gani na mnaangalia/mnapigania harakati gani ili mpira ukue??

Hao watoto wa Under 15 ndiyo taifa la kesho Sasa Kama wanafanyiwa Madudu Kama haya na wakaamua kuachana na mpira mnadhani kuwa tutapata wapi wakina John Bocco, Mbwana Samata N.k??

Maoni Yangu: Enyi wachambuzi wa Mpira ACHENI kupaza sauti kwa Simba SC na Yanga Sc tu, Pazeni sauti juu ya haki na kudhurumiwa kwa watoto/wadogo zetu kwani ndiyo wachezaji wetu wa baadae lakini tukikaa kimya kizazi Cha football kitakufa kwa Tamaa za watu wachache.

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili la michezo na mtandao wetu Pendwa Jamii forum kuwaambia @cloudsfm @efmradio vipindi vya michezo na redio zingine kuwa acheni kuangalia Simba na Yanga tu Pazeni sauti juu ya huu uhuni na dhuruma kwa watoto wadogo.
 
Walichokifanya TFF siyo haki.

Na uzuri nimemuona na kumsikia Wallace Karia akiliongelea jambo hilo kwa kutoa sababu ambazo hazijajitosheleza.

Mfano anasema eti waliwanyang'anya jezi hao watoto kwa sababu hizo jezi zimetengenezwa kwa gharama kubwa!! Kweli ndiyo sababu yenye mashiko hii kutolewa na rais wa shirikisho!!

Halafu sababu ya kutowapa mgao wa fedha walizopewa kwenye hayo mashindano baada ya kuwa washindi wa 2, 3, nk ni kwa sababu mdhamini (Motsepe) alitaka zitumike kujengea miundombinu!!! Sawa!!

Sasa imekuwaje washindwe kuwapa hata posho hao watoto? Je, hawakustahili kupewa chochote, isipokuwa chakula na malazi waliyopata wakati wa mashindano, na nauli tu ya shilingi elfu 20-50 ya kurejea makwao?

Yaani rais Wallace Karia anataka kutuambia Shirikisho halikuwa na fedha ya motisha kwa hao watoto ili na wenyewe wapate moyo wa kulipambania Taifa lao wakati mwingine?

Je, Karia anataka kutuambia hata maafisa wake na benchi la ufundi walioambatana na hao watoto kwenye hayo mashindano, walilipwa nauli tu za kurejea majumbani kwao!!

This is unfair!! Na cha kuhuzunisha, wakati anajibu hizi tuhuma; alijikita zaidi kwenye zile kauli zake zilizo zoeleka za nyodo, dharau na kejeli. Huwa hapendi mawazo mbadala! Hapendi kukosolewa!! Huyu jamaa anatakiwa kubadilika.
 
MKUU YAANI HAO JAMAA NI JANJA JANJA KWELI
 
Mtoto wa chini ya miaka 15 anataka kulipwa?
Sidhani hata kama sheria za FIFA zinaruhusu hii.
Tangu lini kuichezea team ya Taifa ilikuwa ni kuhusu malipo.
Kwamba wamepokonywa Jezi? Au wamerudisha jezi. Waliambiwa hizo jezi ni mali yao?
Kuna vitu vya kulalamika, ila sio hili la kutaka kuanza kuwalipa watoto wa miaka 15 wakilichezea Taifa.
 
Msomali ni Mjinga sana.....

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Hivi nikikuuliza TFF ina shida ya jezi kiasi cha kuzing'ang'ania hizo jezi zilizotumika kwenye hayo mashindano? Jibu litakiwa ni ndiyo, au hapana?

Halafu tukija kwa hao watoto; ndiyo kusema hawastahili posho na motisha kwa sababu tu ya umri wao?

Mbona wale watoto wa timu ya Taifa la Zanzibar walipewa zawadi ya mamilioni ya fedha kama motisha baada ya kuchukua ubingwa wa CECAFA!!
 
Hili binafsi hata mimi limenishangaza mtoto wa miaka 15 bado ni mdogo sana hata interest na hela huwa hawana kiivo huwa wanapenda kucheza mpira na kufurahi hayo mambo ya pesa nadhani kuna vijeba kwenye timu wanawashawishi vibaya madogo

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hivi nikikuuliza TFF ina shida ya jezi kiasi cha kuzing'ang'ania hizo jezi zilizotumika kwenye hayo mashindano? Jibu litakiwa ni ndiyo, au hapana?
Kuzing'ang'ania unamaanisha nini?
Uliwahi kuuliza hata Timu za wakubwa kama huwa wanaondoka na jezi?
Unanilimit nanmna ya kufikiri? Kwamba jibu liwe ndio au hapana?
Kwani watu mkiskia timu ya Taifa mnaelewa nini kwani? Pahala pa kwenda Kugawana posho na Kucheza ili uondoke na Jezi?
Halafu tukija kwa hao watoto; ndiyo kusema hawastahili posho na motisha kwa sababu tu ya umri wao?

Mbona wale watoto wa timu ya Taifa la Zanzibar walipewa zawadi ya mamilioni ya fedha kama motisha baada ya kuchukua ubingwa wa CECAFA!!

Ukiona mtu yoyote anampa motisha ya Fedha mtoto jua anashida pahala.
Miaka 15 anadai hela? Sijawahi skia hii.......
 
KAMA HAWALIPWI HIYO ELFU 20 WALIWAPA YA NINI?

HII NCHI HUWEZI KUCHUKUA VIJANA WA WATU/WATOTO WA WATU WAKALIWAKILISHE TAIFA HALAFU WEWE UNAPATA PESA KUPITIA WAO UNAWAACHA KWENYE MATAA HILO HALIPO MZEE.
 
Wako katika mahesabu ya walaji
 
Kama watoto hawalipwi, sasa hiyo zawadi ilitoka ili iweje. Walipwe viongozi
 
Walipeni watoto pesa zao mnajiabisha sana
 
hivi Karia na vibaraka wake wanaweza kwenda kwenye function yoyote wasilipane posho? mbona wanatumikisha watoto wa watu kama watumwa! so sad!
 
Kwani hawana wazazi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…