Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

Mtoto sio mali ya nchi we kenge ndo maana mtu ana uhuru wa kubadili uraia, hata mchezaji ana uhuru wa kukataa kuchezea timv ya taifa lake, halazimishwi, halafu tunaongelea maslahi hapa, hao watoto kuna kitu wameingiza, ambacho kimsingia walitakiwa wanufaike nacho,
ETI PESA ZIMEENDA KUJENGA MIUNDO MBINU.
 
Watu wanapiga Kelele tu hapa, Chini ya miaka 15 ( Miaka 14 na siku kadhaa kushuka chini)
Mtoto wa miaka 14 anadai hela? Afu anasema familia Inamtegemea.
Akirudi hana Kitu watamshangaa.....
Huyo ni wa U 15 kweli?

Wabongo ni watu wa malalamiko na Kuendeshwa na Mihemko.
Umasikini upo kwenye damu huo na hata ukifanikiwa huwa hautoki watoto watoke nje ya Nchi harafu uwape 15,000 unaona sawa upo sawa kweli kichwani mwako? Haya watoto hutaki kuwapa pesa umewafanyia nini kama burudani yao ?
 
Hapa tunakubaliana ila sio kijana wa miaka 14 kupigia hesabu ya kugawana pesa wakishinda team ya Taifa.
shida yako hufikirii nje ya box, posho/kulipwa ni suala mtambuka, ndo maana nchi za wenzetu mtoto akiwa na kipaji kinacholipwa anatafutiwa manager au mzazi ndo anakuwa msimamizi wake, nchi za watu huwez mtumia mtu burebure tu kwa kisingizio et bado mtoto.
 
Umasikini upo kwenye damu huo na hata ukifanikiwa huwa hautoki watoto watoke nje ya Nchi harafu uwape 15,000 unaona sawa upo sawa kweli kichwani mwako? Haya watoto hutaki kuwapa pesa umewafanyia nini kama burudani yao ?
Hapa unamzungumzia nani ?
Mimi au hao watoto sikuelewi?
 
we ndo unayeelewa mambo siyo, mnatumia vipaji vya watoto wa watu kupanua matumbo yenu na wake zenu, kwa nn msingepeleka watoto wenu kucheza.
Unaweza ukawatukana hawa vima yaani utengeze shule kwa ajili ya kujitafutia pesa kupitia watoto harafu anakuja Kima mmoja anawatetea Wezi wenzie...
 
NALIA NGWENA huwa nashangazwa sana na wachambuzi wa kibongo wanaojiita wanaharakati na uchambuzi wao umejikita juu ya Simba sc na Yanga Sc utadhani hii nchi Kuna timu mbili tu ndiyo zinacheza.

Kuna bwana mdogo kaandika kwenye mitandao anaituhumu TFF kuwa imewadhurumu haki Yao hawajalipwa lakini wachambuzi MAANDAZI wapo kimya tu.

Mbona Suala la Feisal salum Wachambuzi mliongea sana na harambee ya kumchangia mlipitisha bakuli??

Wachambuzi wa Kitanzania mnachambua football gani na mnaangalia/mnapigania harakati gani ili mpira ukue??

Hao watoto wa Under 15 ndiyo taifa la kesho Sasa Kama wanafanyiwa Madudu Kama haya na wakaamua kuachana na mpira mnadhani kuwa tutapata wapi wakina John Bocco, Mbwana Samata N.k??

Maoni Yangu: Enyi wachambuzi wa Mpira ACHENI kupaza sauti kwa Simba SC na Yanga Sc tu, Pazeni sauti juu ya haki na kudhurumiwa kwa watoto/wadogo zetu kwani ndiyo wachezaji wetu wa baadae lakini tukikaa kimya kizazi Cha football kitakufa kwa Tamaa za watu wachache.

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili la michezo na mtandao wetu Pendwa Jamii forum kuwaambia @cloudsfm @efmradio vipindi vya michezo na redio zingine kuwa acheni kuangalia Simba na Yanga tu Pazeni sauti juu ya huu uhuni na dhuruma kwa watoto wadogo.
Watakuwa wamekula mgao. Mwandishi wa habari ukimpa 10,000 tu umemteka.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
labda miundombinu ya matumbo ya viongozi wa tff maana kila aliye pale ana tumbo kama gunia, yaani unasubiria zawadi ndo ukajengee miundo mbinu? yule msomali si binadamu wallah.
Msomali arudishwe kwao Somalia kwa kweli,, WATANZANIA hawawezi kuwa na Akili za kikatili kiasi hiki...

Eti jezi nayo inajengewa miundo mbinu ...

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Mtoto wa chini ya miaka 15 anataka kulipwa?
Sidhani hata kama sheria za FIFA zinaruhusu hii.
Tangu lini kuichezea team ya Taifa ilikuwa ni kuhusu malipo.
Kwamba wamepokonywa Jezi? Au wamerudisha jezi. Waliambiwa hizo jezi ni mali yao?
Kuna vitu vya kulalamika, ila sio hili la kutaka kuanza kuwalipa watoto wa miaka 15 wakilichezea Taifa.
We mbwa, hivi mpira ni juhudi binafsi au mbio za mwenge ambazo kila mmoja anashiriki?

Kama ni juhudi binafsi, kwanini mtu asipewe motisha?

Timu ya taifa ya wakubwa hawalipwi? Au kwa sababu wanawezabkudai na kugoma.

Hao watoto hata ulaya wanawapa motisha. Iko namna ya kuwalipa.

Kumbuka nao wana majukumu yao katika familia zao. Wanahitaji mahitaji ya shule nk.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
We mbwa, hivi mpira ni juhudi binafsi au mbio za mwenge ambazo kila mmoja anashiriki?

Kama ni juhudi binafsi, kwanini mtu asipewe motisha?

Timu ya taifa ya wakubwa hawalipwi? Au kwa sababu wanawezabkudai na kugoma.

Hao watoto hata ulaya wanawapa motisha. Iko namna ya kuwalipa.

Kumbuka nao wana majukumu yao katika familia zao. Wanahitaji mahitaji ya shule nk.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Sio Tu ni motisha Bali ni zawadi zingatia neno ZAWADI
 
Back
Top Bottom