Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

H
Unajifanya mjuaji kweli ,kuhusu kuchezea timu ya taifa lazima mupewe posho tu hamuwezi kucheza bure hayo tushayaona sana wachezaji wanagoma kuchezea timu ya taifa mfano nigeria,Cameroon nk tena hao waliokigoma ni wachezaji wakubwa wanaocheza ligi za ulaya kwasababu mpira ni ajira kama ilivyo uwaziri,ubunge na ukuu wa mkoa
Hajui chochote huyo boya anaropoka tu humu ndani eti timu ya taifa hutakiw kulipwa!!! Alafu unaweza Kuta ni Kiongozi humo humo tff.
 
Wangepewa hata vifaa vya Michezo na jezi, jezi za mashindano et wamechukua huu ni ufala sasa madogo wangebadilishana jezi na wenzao ingekuaje? Wangeambiwa wazifate?
tff ina watu wa ajabu sana tangia zamani, canavaro alibadilishaga jezi na eto (timu ya taifa) ilikuwa ishu ngumu sana kwake, ikafika mpaka akaambiwa afuate jezi alipo eto au afanye mpango eto atume hyo jezi. Ilibid mpaka waziri aingilie kati kuwa jezi akishakabidhiwa mchezaji ni mali yake, ndo tff wakaufyata.
 
Hili ni andiko bora la mwaka upande wa jamii sports,japo unaonekana unapenda kuonyesha lawama na vidole kwa watu.Ukiacha usimba na Uyanga una kichwa kizuri.
 
Hao wanaosema mtoto wa miaka 15 hatakiwi kupewa pesa, wanalinganisha mitoto yao ( akina Junior) ambayo bado yanafuliwa nguo.
Kwa kijijini mtoto wa miak 15 ameshajenga gheto lake mwenyewe na anaijua pesa nini, wengine wanategemewa na familia, na unaweza kuta anaishi na bibi.
Watoto wapewe haki yao, Karia asilete akili zake za ukada.
 
Hao wanaosema mtoto wa miaka 15 hatakiwi kupewa pesa, wanalinganisha mitoto yao ( akina Junior) ambayo bado yanafuliwa nguo.
Kwa kijijini mtoto wa miak 15 ameshajenga gheto lake mwenyewe na anaijua pesa nini, wengine wanategemewa na familia, na unaweza kuta anaishi na bibi.
Watoto wapewe haki yao, Karia asilete akili zake za ukada.
UPO SAHIHI MKUU [emoji736]
 
NALIA NGWENA huwa nashangazwa sana na wachambuzi wa kibongo wanaojiita wanaharakati na uchambuzi wao umejikita juu ya Simba sc na Yanga Sc utadhani hii nchi Kuna timu mbili tu ndiyo zinacheza.

Kuna bwana mdogo kaandika kwenye mitandao anaituhumu TFF kuwa imewadhurumu haki Yao hawajalipwa lakini wachambuzi MAANDAZI wapo kimya tu.

Mbona Suala la Feisal salum Wachambuzi mliongea sana na harambee ya kumchangia mlipitisha bakuli??

Wachambuzi wa Kitanzania mnachambua football gani na mnaangalia/mnapigania harakati gani ili mpira ukue??

Hao watoto wa Under 15 ndiyo taifa la kesho Sasa Kama wanafanyiwa Madudu Kama haya na wakaamua kuachana na mpira mnadhani kuwa tutapata wapi wakina John Bocco, Mbwana Samata N.k??

Maoni Yangu: Enyi wachambuzi wa Mpira ACHENI kupaza sauti kwa Simba SC na Yanga Sc tu, Pazeni sauti juu ya haki na kudhurumiwa kwa watoto/wadogo zetu kwani ndiyo wachezaji wetu wa baadae lakini tukikaa kimya kizazi Cha football kitakufa kwa Tamaa za watu wachache.

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili la michezo na mtandao wetu Pendwa Jamii forum kuwaambia @cloudsfm @efmradio vipindi vya michezo na redio zingine kuwa acheni kuangalia Simba na Yanga tu Pazeni sauti juu ya huu uhuni na dhuruma kwa watoto wadogo.
Kuna shida mahala kwa hawa wachambuzi wetu, asilimia kubwa wanawaza kuwashambulia simba au yanga na lengo kusaka followers mitandaoni

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Hivi nikikuuliza TFF ina shida ya jezi kiasi cha kuzing'ang'ania hizo jezi zilizotumika kwenye hayo mashindano? Jibu litakiwa ni ndiyo, au hapana?

Halafu tukija kwa hao watoto; ndiyo kusema hawastahili posho na motisha kwa sababu tu ya umri wao?

Mbona wale watoto wa timu ya Taifa la Zanzibar walipewa zawadi ya mamilioni ya fedha kama motisha baada ya kuchukua ubingwa wa CECAFA!!
Karia ni Mwizi

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Mtoto wa chini ya miaka 15 anataka kulipwa?
Sidhani hata kama sheria za FIFA zinaruhusu hii.
Tangu lini kuichezea team ya Taifa ilikuwa ni kuhusu malipo.
Kwamba wamepokonywa Jezi? Au wamerudisha jezi. Waliambiwa hizo jezi ni mali yao?
Kuna vitu vya kulalamika, ila sio hili la kutaka kuanza kuwalipa watoto wa miaka 15 wakilichezea Taifa.
Mkuu unaoneana ni mchoyo na mbinafsi kuliko hebu jaribu kuwa muungwana kidogo
 
Back
Top Bottom