Enyi wanawake wa Tanzania nani aliwaloga kuhusu michezo ya kuwekeana pesa?

Enyi wanawake wa Tanzania nani aliwaloga kuhusu michezo ya kuwekeana pesa?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Hii sasa imevuka mipaka. Migogoro na ugomvi ni wa kutosha baada ya kudhulumiana pesa. Michezo ni mingi mno. Kuna hadi michezo ya vyombo. Michezo karibu yote haifuati sheria wala utaratibu unaoeleweka. Mbaya zaidi utakuta vikundi vingine ni vya ONLINE.

Wewe mwanamke wa Tanzania nakuamuru achana na huo upuuzi unaoitwa mchezo. Kama huna nidhamu ya pesa usidhani michezo itakusaidia. Hiyo hela unayotunza kila siku kwa kijumbe si uongezee mtaji wako wa biashara? Wengi wenu mmekuwa Low Profiled Pr○st!tut£s ili mpate hela za mchezo. Kuna ambao mnacheza michezo ya hela nyingi ndo mmekuwa hatarini zaidi.

Kama unataka kutunza pesa zako nenda benki iliyoko karibu nawe watakushauri namna sahihi na salama ya kuhifadhi pesa zako. Wanaume wanaoshiriki michezo pia waache huo upuuzi.
 
Hii sasa imevuka mipaka. Migogoro na ugomvi ni wa kutosha baada ya kudhulumiana pesa. Michezo ni mingi mno. Kuna hadi michezo ya vyombo. Michezo karibu yote haifuati sheria wala utaratibu unaoeleweka. Mbaya zaidi utakuta vikundi vingine ni vya ONLINE...
Pesa zipi ndo ziwekwe benki, kila withdraw unakatwa sh2000 pesa nyingi sanaa bora tuendelee na huo utaratibu wakusaidiana vyombo vya ndani, na benki ni wezi hata kuangalia salio unakatwa 1000, ambao ni nyingi kwa maisha ya nyumbani, bora kuibia na mwizi ninae mjua kuliko kuibiwa na mwizi nisio mjua.
 
Waache Wanawake wajiwekee akiba, maana siku hizi Wanaume tumekuwa wavivu kuhudumia, Wala kununua vitu vya ndani

Unakuta Mume anatoa shilingi elfu 30 anamwambia Mke eti hela ya kutumia wiki mbili 🙌

Bora hiyo michezo inawasaidia
 
Waache Wanawake wajiwekee akiba, maana siku hizi Wanaume tumekuwa wavivu kuhudumia, Wala kununua vitu vya ndani

Unakuta Mume anatoa shilingi elfu 30 anamwambia Mke eti hela ya kutumia wiki mbili 🙌

Bora hiyo michezo inawasaidia
wajiwekee akiba kutoka kwa mwanaume huyo huyo unayemdharau...
 
Siyo michezo yote ni mibaya, Mimi pia mchezo wa hela inapita kwa kijumbe siutaki! Mchezo mzuri ni ule ambao mna group la what's up na mtu mwenye zamu ya kupokea anaweka no ya simu/acc ya bank yake na kila mmoja anamtumia...... inasaidia sana kutokudhulumiana nk

Msituone wamama hatuna akili hii michezo inasaidia kukusanya Ada za watoto,kodi na hata wengine tunajenga kwa njia hii kikubwa ni uaminifu na nidhamu, zaidi muwe mnajuana mna shughuli za halali kama mnafanya kazi au biashara muhimu ni uhakika wa kulipa hasa ukiwa umeshakula za wenzio.
 
Back
Top Bottom