Enyi wanawake wa Tanzania nani aliwaloga kuhusu michezo ya kuwekeana pesa?

Enyi wanawake wa Tanzania nani aliwaloga kuhusu michezo ya kuwekeana pesa?

Ujumbe umefika

Nipo hapa na kijumbe mkusanya pesa yeye anasema michezo ni mizuri inategemea na lengo au kiasi anachopewa mtu na wachangiaji kama wachangiaji wote hawana tatizo. Mchezo utakua na faida

ila wapo wanaochezesha mchezo kitapeli au kwa ubabaishaji ktk michango ndio shida
 
Hii sasa imevuka mipaka. Migogoro na ugomvi ni wa kutosha baada ya kudhulumiana pesa. Michezo ni mingi mno. Kuna hadi michezo ya vyombo. Michezo karibu yote haifuati sheria wala utaratibu unaoeleweka. Mbaya zaidi utakuta vikundi vingine ni vya ONLINE.

Wewe mwanamke wa Tanzania nakuamuru achana na huo upuuzi unaoitwa mchezo. Kama huna nidhamu ya pesa usidhani michezo itakusaidia. Hiyo hela unayotunza kila siku kwa kijumbe si uongezee mtaji wako wa biashara? Wengi wenu mmekuwa Low Profile ili mpate hela za mchezo. Kuna ambao mnacheza michezo ya hela nyingi ndo mmekuwa hatarini zaidi.

Kama unataka kutunza pesa zako nenda benki iliyoko karibu nawe watakushauri namna sahihi na salama ya kuhifadhi pesa zako. Wanaume wanaoshiriki michezo pia waache huo upuuzi.
Umesema kweli. Wengine wanaishia kuuza utu wao ili wachangie ama waishi baada kuwa wamepeleka hizo fedha kwa kijumbe 😀
 
Siyo michezo yote ni mibaya, Mimi pia mchezo wa hela inapita kwa kijumbe siutaki! Mchezo mzuri ni ule ambao mna group la what's up na mtu mwenye zamu ya kupokea anaweka no ya simu/acc ya bank yake na kila mmoja anamtumia...... inasaidia sana kutokudhulumiana nk

Msituone wamama hatuna akili hii michezo inasaidia kukusanya Ada za watoto,kodi na hata wengine tunajenga kwa njia hii kikubwa ni uaminifu na nidhamu, zaidi muwe mnajuana mna shughuli za halali kama mnafanya kazi au biashara muhimu ni uhakika wa kulipa hasa ukiwa umeshakula za wenzio.
Hauko salama.
 
Na hatutaki ushauri🤣🤣🤣
Benki ili watukate kodi, wale kwa urefu wa kamba!! Akuuuuuuuu!
Ulizia account zisizo na Makato mfano mm nilikua na malengo yangu nikafungua nmb wallet hakika ilinisaidia
 
Attachments

  • IMG_20241004_202653_123.jpg
    IMG_20241004_202653_123.jpg
    383.3 KB · Views: 6
Hii sasa imevuka mipaka. Migogoro na ugomvi ni wa kutosha baada ya kudhulumiana pesa. Michezo ni mingi mno. Kuna hadi michezo ya vyombo. Michezo karibu yote haifuati sheria wala utaratibu unaoeleweka. Mbaya zaidi utakuta vikundi vingine ni vya ONLINE.

Wewe mwanamke wa Tanzania nakuamuru achana na huo upuuzi unaoitwa mchezo. Kama huna nidhamu ya pesa usidhani michezo itakusaidia. Hiyo hela unayotunza kila siku kwa kijumbe si uongezee mtaji wako wa biashara? Wengi wenu mmekuwa Low Profile ili mpate hela za mchezo. Kuna ambao mnacheza michezo ya hela nyingi ndo mmekuwa hatarini zaidi.

Kama unataka kutunza pesa zako nenda benki iliyoko karibu nawe watakushauri namna sahihi na salama ya kuhifadhi pesa zako. Wanaume wanaoshiriki michezo pia waache huo upuuzi.elf 10.
Halafu tunaoumia ni sisi wanaume, kutwa kuombwa pesa za mchezo , huwa nasikia hasira sana kuombwa pesa za michezo.., maana wakati wa kuvunja hivyo vikoba wala hushirikishwi, ila kwenye kuweka sasa..
Bank na wenyewe makato yao mie nacheza mwenyewe😂😂 kila siku nahakukisha niketupia katika simu yangu
 
Halafu tunaoumia ni sisi wanaume, kutwa kuombwa pesa za mchezo , huwa nasikia hasira sana kuombwa pesa za michezo.., maana wakati wa kuvunja hivyo vikoba wala hushirikishwi, ila kwenye kuweka sasa..
,😂😂😂😂 Uwe unauliza uliza siku ya kuvunja kikoba
 
Back
Top Bottom