Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Siku hizi watu hawawezi kabisa kutunza siri. Kila mtu anataka aonekane anajua kitu fulani kuhusu mtu fulani. Anaona akikisema au kukishea na wengine anaona kama amekuwacool au anapata sifa. Mwambie mtu ishu ndogo tu kesho utashangaa kila mtu anajua. Haiwezekani kabisa kuwa na maongezi kama zamani, kila mtu mpashukuna. Hakuna faragha kabisa. Hakuna wasiri tena. Kila mtu anataka kuwa wa kwanza kusema/kujua jambo fulani kuhusu fulani.
Wanaume siyo kama wa zamani. Siku hizi ni bora ya wanawake, wanaume hawawezi kabisa kutunza siri. Ushahidi unaonyesha kwa Tz wanaume ni wengi sana Istagram kuliko wanawake.
Ubaya wa watu kujua-jua mambo yako ni nini? Watu wengi watatumia taarifa hizo kukukwamisha/kukuattack. Nimeshuhudia hilo mara nyingi sana. Kuna hadi waliopoteza kazi.
Nini cha kufanya. Linda na ficha mambo yako kadri uwezavyo. Hao unaowaamini sana ndiyo wasambazaji wa taarifa zako. Hata kama una jambo zuri vipi, ishu ambayo unafikiri ukimwambia mtu wako wa karibu atafurahia, usimwambie bila kufikiri kwa kina madhara yake.
Kingine; watu wengi wanafikiri kuwa siri zina expire. Unamwambia mtu ishu fulani. Yeye anafikiri kuwa baada ya muda inakuwa imeexpire hivyo anaweza kuisambaza.
Kuwa makini, linda faragha yako. Watu wasio na ustaarabu ni wengi sana.