Enzi hizo Pepe Kalle na Hidaya Khamis Masawe

"Nimepoteza mpenzi wangu nchini Tanzania[emoji443]"
 
Ila alikuwa kifaa, angekuwa bado yuko hai ningemtafuta
 
Mwaka 1991 Pepe Kalle na bendi yake ya Empire Bakuba walikuja Tanzania kutumbuiza mkoani Arusha.

Baada ya kufika Arusha, walikodi teksi iliyokuwa ikiendeshwa na mwanamke aitwaye Hidaya Khamis Massawe. Wakiwa ndani ya teksi walianza kuongea kwa lugha ya Lingala wakimsifu dereva teksi kwa jinsi alivyokuwa mzuri. Hata hivyo, Hidaya (dereva teksi)

alikuwa anafahamu lingala kutokana na shughuli zake za kibiashara huko RD Congo. Pepe Kalle alishtuka sana baada ya kumsikia Hidaya akizungumza kwa lugha ya Lingala. Baada ya kumaliza shoo yao jijini Arusha, Pepe Kalle aliahidi kuwa atarejea Tanzania kwa Hidaya.

Mwaka uliofuata wa 1992, Pepe Kalle kweli alirudi Tanzania Arusha na kutunga wimbo wa Hidaya.

Mume wa Hidaya Mzee Massawe, baada ya kujua kuwa wimbo wa Hidaya alitungiwa mkewe aliamua kuachana naye na kumuacha siku hiyo hiyo.

Hidaya khamis masawe alifariki mwaka 2021 Arusha mtaa wa Kaloleni.

View attachment 2922833
Iv hakuachaga watoto pepekale
 
Uyo mume nae fala,
Unaruhusu vp mkeo afanye udreva taxi?
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
uko makazini wanawake zetu Wana mabwana zao.
Kuna mwana hapa anatafuna wife wa mchizi kinoma noma na ukiangalia ni kama mwana hapa ndo ana masaa mengi na manzi about 10 hours daily ukiondoa jumamosi na Jumapili!
 
Mwaka 1991 Pepe Kalle na bendi yake ya Empire Bakuba walikuja Tanzania kutumbuiza mkoani Arusha.

Baada ya kufika Arusha, walikodi teksi iliyokuwa ikiendeshwa na mwanamke aitwaye Hidaya Khamis Massawe. Wakiwa ndani ya teksi walianza kuongea kwa lugha ya Lingala wakimsifu dereva teksi kwa jinsi alivyokuwa mzuri. Hata hivyo, Hidaya (dereva teksi)

alikuwa anafahamu lingala kutokana na shughuli zake za kibiashara huko RD Congo. Pepe Kalle alishtuka sana baada ya kumsikia Hidaya akizungumza kwa lugha ya Lingala. Baada ya kumaliza shoo yao jijini Arusha, Pepe Kalle aliahidi kuwa atarejea Tanzania kwa Hidaya.

Mwaka uliofuata wa 1992, Pepe Kalle kweli alirudi Tanzania Arusha na kutunga wimbo wa Hidaya.

Mume wa Hidaya Mzee Massawe, baada ya kujua kuwa wimbo wa Hidaya alitungiwa mkewe aliamua kuachana naye na kumuacha siku hiyo hiyo.

Hidaya khamis masawe alifariki mwaka 2021 Arusha mtaa wa Kaloleni.

View attachment 2922833
Pepe alikuwa anakula mzigo ama ini wazee?
 
Back
Top Bottom