Enzi hizo utotoni

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Nakumbuka tulikuwa tunaruka fensi ya hospitali kwenda kuokota mipira iliyotumika (catheter) maarufu kama tekenya, mipira hiyo ilitumika kutengenezea manati ambayo inavutika sana na kulenga umbali mrefu. Mipira hiyo ni taka hatarishi lakini hatukuwahi kuugua,

Manati yenye mipira ya dunlop nani anaikumbuka?

Manati ikiuua ndege damu ya ndege unaipaka kwenye kipago nani anakumbuka?

Kutega ndege kwa kutumia ulimbo ( wirembo) nani anakumbuka?

Kutengeneza mawe ya kwenye manati kwa kutumia udongo wa mfinyazi (mbiringe) nani anazikumbuka?

Nani anaijua hii kitu hapo chini

Hebu toa experience yako hapa enzi hizo utotoni

 
Mpira wa miguu maarufu kama tango master enzi hizo ukiwa unauzwa Tsh elfu kumi na tano pia kulikuwa na tubeless nani anaikumbuka?
 
Kombolela mnaenda kujifichia jikoni ili mdokoe sukari guru ya mama mmoja hivi alikuwa anauza shule ni breakfast.
 
Kwa historia hii utakuwa umekulia maeneo ya mkoa wa pwani au morogoro umeenda mbali basi Lindi ama mtwara. Lakini hasa hayo maneno ni ya Pwani.
 
Kwa
Inaelekea wewe unaogopa kugegedana tu, yaani raha yote ya kugegedana wewe huitaki eti unataka kurudi kuwa mtoto? Baba yako anajuwa haya. angalia asije kukupa laana, maana yeye nataka wajukuu sasa acheze nao.
N kombolela mbona walikuwa wanagegedana frsh tuu mzeeh baba. Tna kama ukisikia michezo ya kibaba na kimama af usikie watoto wanalilia kuwa baba au mama hapo jua tayari kuna jambo kati yao.πŸ˜‚πŸ˜‚

Hutoto raha saan asikudanganye mtu
 
We mwamba sio mtabora kweli wewe?
 
Kwa

N kombolela mbona walikuwa wanagegedana frsh tuu mzeeh baba. Tna kama ukisikia michezo ya kibaba na kimama af usikie watoto wanalilia kuwa baba au mama hapo jua tayari kuna jambo kati yao.πŸ˜‚πŸ˜‚

Hutoto raha saan asikudanganye mtu
Sitaki kurudi huko, nawaachia nyie mie niendelee kuwachapa mademu mtakao niachia.
 
Enzi za utoto nimekumbuka tulikuwa tunapika mchanga..Kama tunapika wali...πŸ˜‚πŸ˜‚
Mtu mzima mmoja akatuambia tutachomwa Moto siku ya kiama tukaachaga kuupika mchanga.
 
Kuiba maandazi na kuyaficha kwenye kwapa kisha ukifika nje unakula na wenzako!
πŸ˜€πŸ˜€
 
Hayo mawe ya kupiga manati sisi tuliyaita "mbulugwa" na kile kingozi kinachocover jiwe au mbulugwa sisi tulikiita "kikova"
 
Mpira wa miguu maarufu kama tango master enzi hizo ukiwa unauzwa Tsh elfu kumi na tano pia kulikuwa na tubeless nani anaikumbuka?
Tubeless si ni lile lenye maupele pele sieti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…