Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ENZI ZA AFRICA EVENTS
Msomaji wangu mmoja kaniandikia maneno hayo hapo chini baada ya kusoma makala yangu niliyomtaja Prof. Hamza Njozi:
"Makala ya Prof.Hamza Njozi katika jarida la Africa Events ilihusu nini?
Sikujua kama Prof.Njozi alikuwa akiandika katika Africa Events, ingependeza kama ungetuletea makala zake.
Pia ikiwezekana tuletee picha za jarida la Africa Events, naamini wapo wasomaji wako hawajawahi kuliona jarida hilo."
Nami nimemjibu:
JK,
Makala za Prof. Hamza Njozi sina kwa hivi sasa kwani ni miaka mingi imepita.
Toleo hili la Rais Mwinyi yuko kwenye meli inayopigwa mabomu ilikuwa ni ''lead story'' yangu na sababu yake ni kuwa Ahmed Saleh Yahya wakati huo akiwa mhariri wa Africa Events alikuja Dar es Salaam na tukawa na mazungumzo kuhusu matatizo aliyokuwa anapata Rais Mwinyi kutoka vyombo vya habari Tanzania pamoja na magazeti ya chama chake akiwa Mwenyekiti na gazeti la serikali akiwa ndiye Rais.
Rais Mwinyi akishambuliwa sana na magazeti.
Ahmed Yahya akaniuliza hii iinawezekana vipi?
Mimi nikamueleza kwa nini inakuwa hivyo.
Siasa za Tanzani ni za aina yake kwa watu fulani.
Hapo tuko katika hoteli moja maarufu inaitwa Chef Pride iko Chagga Street na ndiyo ilikuwa kijiwe changu nikija Dar kutoka Tanga.
Basi niko hapo na Sheikh Ahmed tunashusha chai, kababu na sambusa.
Mimi Ahmed Yahya aliponipigia simu kuniambia kuwa yuko mjini na ananiomba tunywe chai pamoja nikajua lipo jambo.
Waamerika wana msemo, ''There is no free lunch in America.''
Ukiona mtu kakualika anakununulia chakula jua utalipa kwa njia nyingine.
Nasema haya kunogesha barza.
Nimekula sana biriani za marehemu Ahmed Yahya London bure na hakunituma kazi.
Sheikh Ahmed akaniomba niandike makala moja kama njia ya kumsaidia mzee wetu.
Ndiyo nikaandika hiyo makala na wakati huo Africa Events walikuwa wameacha kuchapa makala zangu kwa muda mrefu.
Makala hii walichapa kama makala ya ''Special Correspondent.''
Hiki ni kisa kingine Insha Allah iko siku ikipatikana fursa nitakieleza.
Kilichonifurahisha mimi katika toleo hili ni hiyo, ''caricuture'' ya Rais Mwinyi yuko juu ya chombo kinataka kuzama baada ya kupigwa bomu na kushika moto.
Hili Africa Events ndilo gazeti langu lililonitoa ukumbi na nikafahamika.

Share
=AZX2lsA5FjUg_As9lS84E1InZ4BaloGhoksJI1_MG2TCczcQdnqzJPhoHfiimgarSubzp3R2rIGjeX-mgoKLJqxn0z6Tv_Z9VV6NyK1v2TUgrpTPms3seRwJnVZ0tUxe63U&tn=%3C%3C%2CP-R']