Enzi za UHIMA(CASFETA),UKWATA na TYCS: Ulikua wapi???

Enzi za UHIMA(CASFETA),UKWATA na TYCS: Ulikua wapi???

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Habari hii sio yangu, nimeikuta mahali nikaona tujikumbushe tuliyowahi kuyapitia miaka ileee. Inachekesha lakini inasaidia kutukumbusha kuwa wakati si milele...

Kulikuwa na UHIMA(CASFETA),UKWATA na TYCS wakati tukisoma.Sisi wengine tulio katikati,wakati mwingine tulienda UKWATA sbb ya kuimba Mapambio na nyimbo za kusifu.Kukesha ktk sala na usiku wa kuabudu.Kule TYCS tulisogea wakati wa mikusanyiko na ibada na kwaya ili kukaa kwa ukaribu na mabinti.Ambao tulikuwa tunawaona kwa msimu.

Hawa wazee wa "Maranatha" wa siku ya saba ya Juma nao walikuwa na Umoja wao.Baada ya machweo ya ijumaa huwezi kumuona na kitabu wala daftari la kukopi notisi.Hakika shule ni mahali sahihi kujifunza tamaduni na mila za jamii tofauti za dunia hii.

Huku UHIMA ilikuwa ni full sala na maombi ya kina na tafakuli za biblia.Wale jamaa wa TYCS walikuwa Liberal sana!Huku Disko unawakuta na kanisani wapo.Vurugu za kutoroka usiku kwenda mtaani wapo na kanisani wapo.Hawakujifunga sana kati ya dini na maisha ya ujana na uanafunzi.Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tuliletewa wasichana wa shule jirani kwa ajili ya disco.(Shule yetu ilikuwa boys tupu)

Wengi tulijichanganya kwa ajili ya "kurefresh mind". Kucheza disko mchana kutwa mpaka jioni ya machweo ilikuwa burudani sana.Ilikuwa siku njema ya kusubiliwa na wengi.Wengine hatukuwa wanafiki..Tulisema hadharani jinsi tunavyopenda disko na namna ilivyotupa burudiko la akili.Katika umri wa miaka 17 hadi 20,kukumbatiwa na mtoto wa kike mwenye konzi kifuani...Huku "West Life" wakitumbuiza na kibao chao cha "The Queen of My Heart".Loooh....ilikuwa barabara sana!Hakika nyakati hazirudi nyuma.

Tumesoma wakati huo usiokuwa na simu za mkononi.Haukuwa wakati wa M-Pesa,Tigo Pesa wala Airtel Money.Ni nyakati za EMS na Telegram,wakati wa barua na kadi za love na best wishes.Siku ya disko ndio ilikuwa makutano na yule umpendaye au wakati wa kutuma barua ya "proposal" kwa yule umtamaniye.

Barua yenye karatasi maalumu,zenye nakshi ya makopakopa na background ya maandishi ya kimapenzi.Ziliuzwa shilingi kumi hadi shilingi wakati wa uhitaji.Looh....We can not turn the days and live again in these memorable moments,but we can turn the memories and share the old good moments!

TAMSA ulikuwa ni Umoja wa Wanafunzi wa Kiislamu.Tuliwaita "Wazee wa Feedback",wengi baada ya disko ni kuja bwenini kusikiliza na kuulizia story za kwenye ukumbi wa disko,nini kilitokea na nani alifanya tukio gani.Wengi walipenda kuhudhuria lkn pindi wakionekana kwenye milango ya kumbi za disko walitengwa na jamii ya wenzao ktk umoja wao.

Wao wakabaki kuwa "Wazee wa Feedback" ya kilichotokea disko.Ukitoka tu disko utasikia "Hebu tupe feedback ya huko mtaalamu".Sehemu ya hekaheka za ujana na uanafunzi wao ni kama "ilidhurumiwa" na mifumo ya imani.Siri ya imani na mifumo yake anayo Mungu...

Hawa TYCS tuliwaita wazee wa "Kiasi".Wao kila kitu ni ruksa ili ufanye kwa "Kiasi".Kwamba kila kitu kina umuhimu wake ktk maisha lkn kifanyike kwa kiasi,kama ni disko nenda,ila cheza na kumbatia wakati wa blues kwa kiasi.Chochote kikizidi ni sumu.Hawa ukimkuta disko anaruka majoka kama Small Jobiso,na kwenye "Easter Conference" anahubiri kama kazaliwa ukoo wa masiah.Haya yote ni mafunzo.Mchangamano huu ukibahatika kuuona maishani,basi itakufanya uheshimu kila jambo ktk jamii.Fikra tofauti ndani ya jamii moja.

Siku ya disko kila mtu alichukua viwaro vyake vya nguvu.Kupulizia pafyumu popote unapoikuta inapuliziwa,kiasi unaweza kujikuta unanuka badala ya kunukia.Hii nayo ilikuwa "experience" nzuri ktk maisha.Mahali palipochezwa disko mchana ndipo usiku palipigwa sala za usiku kwa wanafunzi wa dini na umoja tofautitofauti.Mchana disko na usiku ni sala,na maisha yanaendelea.

Ujana maji ya moto.Habari moja ya kiongozi wa UKWATA kupenda disko mpaka kutengwa.Alikuwa kila disko lazima aingie,lkn hii ilikuwa kinyume na misimamo ya UKWATA.Walimpa machaguo...Kati ya disko na UKWATA...Jamaa hakujiuliza,alichagua raha za disko; na wakati wa mahafali hata cheti cha kutambuliwa kuwa member wa UKWATA hakupata.Sasa ni baba wa familia na watoto watatu,ndani ya ndoa takatifu.Kiongozi aliyemvua "uanachama" kwa kosa la kuingia disko ni baba wa watoto wanne ambao kila mmoja ana mama yake.Hakika mambo ya imani yana mafumbo yake.

Wakati mwingine imani na uchumi binafsi wa mtu vina uhusiano.Maana wale waliosema ni kukosoa uumbaji kusuka,kupaka wanja na hata kuweka lipshine,sasa ndio walimu wa kujiremba.Wakati ule hali "mbaya" ya uchumi wao binafsi waliificha ndani ya imani zao.Akiiulizwa kwanini hajirembi kama wenzake,atasema "Wapendwa ktk bwana huwa hatuhangaiki na urembo wa kidunia".Baada ya "boom" la pili mambo huwa tofauti.Hii inatoa funzo.

Mwingine alivaa "kobasi" na suruali za juu ya enka,kwa msimamo wa imani.Warembo wa Chuo wakamfanya aone ule si uvaaji wa kijana barobaro.Hakika nyakati zinabadirika na mengi tunajifunza kadiri ya tunavyokua.Miaka inaenda,umri unasonga,sasa tunakutana mitaani kama kina baba na kina mama wa familia.Wale wajuzi wa imani ndio sasa tunawashauri jinsi ya kupunguza mipango ya kando na kilaji(pombe) ili kuweka msisitizo wa kutunza familia.Hivi haya mambo ni kwanini?

Hivi kuna uhusiano wowote wa "kuyaonja" mambo fulani ya "utineja" na kuachana nayo na wengine "wasiyoyaonja" maisha hayo kukuta wakiyarudia ktk utu uzima?...

HeadMaster wetu(apumzike kwa amani) alisisitiza sana mahudhurio siku ya disko,akasisitiza kuwa tucheze sana mpaka tutoke jasho,na disko likiisha tuwahi bafuni kuoga kabla miili haijapoa,na tulale bila kugusa daftari mpaka kesho.Haikuwezekana kulala baada ya kuoga,muda huo ilikuwa ni wasaa wa kusimuliana yaliyojiri ukumbi wa disko.Wazee wa "Feedback" wakiongoza kwa maswali na udadisi.

Kuelekea mwishoni mwa disko,DJ machachari hufunga na nyimbo mfululizo za "blues".Hapo itapigwa ya kwanza na atatangaza "one more track"...ikisisika sauti hiyo watu huzidi kukumbatia ya mwisho mwisho.DJ mtukutu ataongeza nyingine moja akibandika juu ya pili,huku walimu wa malezi wakiwa tayari kuhakikisha kila mtu anarejea bwenini bila kuchepuka kizani.

Huu wakati hautarudi tena,sioni tena wakati huu ukirudi hata kwa vizazi vyetu.Ulikuwa ni wakati mtiifu na rafiki kwa utineja wetu.Mikono mifukoni mara baada ya disko na kurudi bwenini..Si kwasbb ya baridi watu wanaweka mikono hiyo mifukoni,bali wakati huo hali ya "maungo" inakuwa si hali tena.Sabuni hujuta kwanini ilitengenezwa kwa kuteleza...Looh!!Wakati huu upo wapi?
 
samahani mkuu,ni ''HUIMA'' (Huduma ya Injili Mashuleni) na sio 'uhima'...........
mimi nilkua Tabora miaka ile.walikua na bendi moja matata sana ya gospel ikiongozwa na Abel(nasikia ni mchngaji),dada Vai,Andy katika drums,Silanda katika Bass guitar na wengine wengi.walikua na impact kubwa kwangu na japo nilizungukwa na mazingira ya muziki these guys inspired me a lot..nilijifunza kupiga ala yangu ya kwanza ya muziki(drumms) pale kituoni kwao Furaha Center..miaka ile Wenge Musica wametoa Pentagon...full ku copy midundo ya Titina Alcapone..
Huima was a real deal..sijui tu walishindwa wapi wakapotea
 
samahani mkuu,ni ''HUIMA'' (Huduma ya Injili Mashuleni) na sio 'uhima'...........
mimi nilkua Tabora miaka ile.walikua na bendi moja matata sana ya gospel ikiongozwa na Abel(nasikia ni mchngaji),dada Vai,Andy katika drums,Silanda katika Bass guitar na wengine wengi.walikua na impact kubwa kwangu na japo nilizungukwa na mazingira ya muziki these guys inspired me a lot..nilijifunza kupiga ala yangu ya kwanza ya muziki(drumms) pale kituoni kwao Furaha Center..miaka ile Wenge Musica wametoa Pentagon...full ku copy midundo ya Titina Alcapone..
Huima was a real deal..sijui tu walishindwa wapi wakapotea
Asante kwa marekebisho chief
 
Mi Ni maalimu!Ila nimeuzuria sana haya Mambo ya tycs na ukwata yote nikatika jitiada za kusakata mademu wa kuchakata,hiyo mrumaa girls,usangi girls,kilogaya,kiriki,minja na lomwee,asee kikweli nilizichakata.kuna jamaa alikuwa tozi kinomaa pambaa Kama zote plus misuti,miguo ya kinaijeria basi Wana ilikua ndo chimbo letu la kwenda kugongea phatfarm,fubu,dada,seanjoans au fila.dah ilikuwa noma
 
Back
Top Bottom