Hahah!! Mazingira tu labda ndio yalisababisha hivyo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Watu simu tumezijua ukubwani kabisa aisee
.comUna miaka mingapi shemu?
Km nakuona vile kwenye bilinge bayoyo..Mi nilikuaga mtaalamu wa kukata viuno,yani tukianza nyimbo zetu za utoto mkataji mauno mkuu ni mimi.
Kuna ule wimbo unamalizikia na maneno ya "okota maganda,peleka uganda yamepanda bei sukuma waaaaa"
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
I miss those moments
Mkuu umenikumbusha sana.Ulikua unaweza nini au kipaji gani?
As for me wakuu,
Nilikua mtaalam sana wa mitego ya ndege. Kuanzia ule mtego wa mpira wa v, unagongelea vijiti vitTu kwenye ardhi inakua kama v hivi halafu katikati unawek pumba au mchele, ukiwa masta zaidi unawek waya kati then unavuta na kuweka kamba. Pia kulikua na mtego wa ungo, vitanzi na ulimbo. Jamaa wangu mmoja bae pia ni prominet member hapa jf yeye alikua ni mtaalam wa kusuka sambi aka chandimu. Yaan kitu kinadunda kama cha kununua, wapi eric kandimba mtaalm wa kusuka kona za magari ya matauri. Yaan mtatengeneza magari yenu vizuri ila lazima muende kwa erick akawasukie kona. I miss them days....
Kweli mkuuHahah!! Mazingira tu labda ndio yalisababisha hivyo
Hizi harakati zako za kutega ndege unanikumbusha jamaa flani kwenye magazeti anaitwa KipepeMkuu umenikumbusha sana.
Nimepitia hiyo kadhia ya kutega ndege kwa mitego hiyo ya V halafu unaweka pumba katikati huku ukiwa imefunga kamba ndefu hadi sehemu uliyojificha ili ndege wasikuone.
Nilikuwa natumia mpira(mkanda wa Baiskeli) au Upinde kutengeneza V ya mtego.
Urimbo nimetumia pia kutega ndege hasa kwenye visima ambayo wanaenda kunywa maji, nilikuwa natafuta mti wenye matawi mengi madogo madogo halafu napaka urimbo kwenye hayo matawi na kuwenda kuweka kwenye sehemu ambayo ndege wanakuja kusimama kabla ya kushuka chini kisimani ili wanywe maji.
Pia tulikuwa tunatega chini pembezoni mwa maji kwa kuweka aina fulani ya magugu magumu marefu mithili ya waya tukiwa tumelipaka urimbo, ndege akiwa anaenda kunywa maji akikanyaga ananaswa na urimbo, akitaka kujiokoa kwa kufurukuta ndio anajinasa zaidi kwenye urimbo hadi hawezi kuruka tena.
Pia nimetumia sana upinde na mshale kuwinda ndege, nimewahi kupiga ndege wengi sana kwa mshale..
Siku moja nilileta kizaa zaa bana na upinde wangu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nilimpiga mwenzangu karibu na jicho(nusura ndani ya jicho).
Tulikuwa na mtindo kuambizana rusha mshale kama utamfikia mwenzako aliyesimama umbali fulani kutoka kwako, sasa mimi nikamwambia jamaa kaa tayari narusha mshale, alikuwa bado hajajiandaa ili ukimfikia aukwepe mimi nikarusha jamaa akaja kushtukia mshale ushafika alipotaka kuukwepa mshale ukampiga karibu na jicho akaanza kutokwa Damu.
Mimi nilihofia sana, ukizingatia Mtingi alikuwa noma(mkali sana) nikawa nawaza kitanuka nikifika home. Ila hakikunuka kivile wazee walikuja kuisolve hiyo kesi ikaisha.
Mimi kuwinda nilikuwa napenda sana hasa kwa kutumia Upinde na Mshale.Hizi harakati zako za kutega ndege unanikumbusha jamaa flani kwenye magazeti anaitwa Kipepe
Hahah!! I wish time could turn back unitag tukawinde wote [emoji23][emoji23][emoji23]Mimi kuwinda nilikuwa napenda sana hasa kwa kutumia Upinde na Mshale.
Nikimpiga ndege najiovunia sana umahiri wa kulenga
Hahahahahaaaaa yaani we acha tu mkuu.Hahah!! I wish time could turn back unitag tukawinde wote [emoji23][emoji23][emoji23]
Hahah!! Mixer na visu kabisa kweli ilikua ni kwele mzeeHahahahahaaaaa yaani we acha tu mkuu.
Halafu siku hizi madogo yametekwa na huu utandawazi ambao umeingia hadi interior, kuwinda hakuna tena kama enzi zetu.
Masula ya upinde hawana habari nayo, wazee ndio wamebaki na pinde na mikuki yao kama silaha za siku zote za jadi.
Enzi zetu ulikuwa ukitembelea nyumbani kwa rafiki yako ukikaribishwa geto unakuta ukuta umejaa Maupinde yamening'inizwa maana ndio ilikuwa staili ya utunzaji.
Mishale(vichwa vyenye ncha kali)(ukienda K/Koo sokoni inaikuta wanauza) tulikuwa tunaitafuta kwa uda na uvumba, mingine tulikuwa tunanunua na mingine tunatengeneza wenyewe kwa kutumia misumari hasa ile ya inchi 6.
Siku ukiwa zamu kwenda kuchunga unatoka ukiwa umebeba upinde wako na mishale yako kadhaa maridadi kabisa ya kila aina, rungu na kisu, huku pembeni una mbwa ambaye unamtumia kufukuza na kukamata ama Sungura au Digidigi msituni.
Kuna wapo walikuwa lazima warudi nakitoweo home jioni.
Hahah!! Mixer na visu kabisa kweli ilikua ni kwele mzee
Aisee!!Mkuu ilikuwa ukiwa porini huna kisu au panga mambo yalikuwa hayaendi.
Kulikuwa na matunda kibao ya kula ambapo mara nyingi itahitajika kisu au panga kupunguza matawi ili uweze kuyachuma.
Pia ukibahatika kupata kitoweo, utatumia kisu kukihalalisha huko huko kabla hakijafa na maumivu ya majeraha ya silaha zetu.
View attachment 761880
Mojawapo ya matunda pendwa ya porini
Hahahahaaaa.Aisee!!
Kweli muda upo kasi sana ndugu yangu
Ata wadogo zako siku hizi hawafanyi tena hivyo zaidi ni Ps na FIFAHahahahaaaa.
Kwa sasa tupo mjini mambo yamebaki historia aisee
Ndio hivyo.Ata wadogo zako siku hizi hawafanyi tena hivyo zaidi ni Ps na FIFA
Duh! Kweli ilikua sio poa mkuuNdio hivyo.
Wao siku hizi wanapanga misele kwa simu, sisi ilikuwa hadi utembee KM kadhaa uendee kwa mshikaji(na unaweza kumkuta au la) na pia mje muende tena sehemu mliyopanga.
Haha yaaaani apo naimbiwa "tunamuomba dada J atuoneshe maringo yaaake bingiri bingir mpaka chini"[emoji23] nakazana sasa kama napewa helaKm nakuona vile kwenye bilinge bayoyo..
Ungekua unakaa mtaani kwetu ningekua nakuja kwenu kukufundisha sarakasiMie nilikuwa fundi wa michezo yote kasoro kuparamia miti na kuruka sarakasi, vilinipitia pembeni kabisa.. Kibaba baaba nilikuwa lazima niwe baba nipate kuwadukunyua watoto wa watu, mpira usiseme nilikuwa fundi, mpaka leo hii na utu uzima wangu.. Nilikuwa so genius mtaa si watoto ama watu wazima walikuwa wakinikubali kichizi, nilikuwa na damu ya kupendwa..
Tatzo langu moja tu nilikuwa mwizi vibaya mnooo[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nashkuru hii tabia nilipofika darasa la 5 hiv nikaiacha, ila nilikuwa mwizi hatar, sijui ningekuwa jambazi la aina gani leo hii, ilifikia hatua mama yangu mzaz alitaka kunichoma mikono yangu moto na nina kialama cha moto mpaka leo mkononi. Kiukweli namshukuru sana mungu kwa kuniongoa.. + vipigo vya mama yangu kipenzi.
Mpaka saivi unajua kulenga ndege?Mimi kuwinda nilikuwa napenda sana hasa kwa kutumia Upinde na Mshale.
Nikimpiga ndege najiovunia sana umahiri wa kulenga