Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Tangu lini Serikali yetu ikaanza kujali Afya za Watoto kuliko viwango vizuri vya ufaulu? Hii haijawahi kutokea na haitakaa itokee, tuache siasa kwenye mambo ya msingi, tusiue sisimizi kwa rungu, tutafute solution ambazo hazitawaweka kwenye wakati mgumu walimu wetu (maana watoto wakifeli serikali hii hii huwa inawaangushia zigo wao utafikiri waliofaulu na waliofeli kwenye shule na darasa moja walikuwa wanasoma madarasa tofauti kumbe ni darasa moja).
Sababu kubwa ya watoto kuumia migongo ni hizi 2:
1. Serikali kuongeza masomo(hasa shule za msingi). Enzi zetu tulikuwa na masomo 5 tuu(Kiswahili,English,Sayansi, Hisabati na Stadi za Kazi), wakati sasa kuna masomo 10+.
2. Walimu kulazimisha watoto wanunue counter books badala ya zile daftari nyepesi. Enzi zetu shule ya msingi hakuna aliyekuwa anatumia counter books, hata sekondari ilikuwa siyo lazima kutumia counter books. Mimi mpaka leo nina daftari zangu za sekondari ambazo nyingi ni zile nyepesi, counter books ni chache sana.
3. Walimu kulazimisha wanafunzi kubeba daftari zote waendapo shule badala ya kubeba zile tuu ambazo ratiba ya masomo inaonesha. Unakuta siku hiyo kuna vipindi 4 lakini mtoto analazimishwa abebe counter books zote 10 badala ya 4 tuu.
Hivyo naisihi Serikali na walimu wetu waache siasa kwenye elimu na watafute solution bila kutingisha status quo iliyopo, elimu yetu bila masomo ya muda wa ziada ni ngumu sana watoto wetu kupasua.
Mbona mnawapa homework kama hamtaki wasome muda wa ziada? Kama ni hivo basi pigeni na marufuku walimu kutoa homework, maana zinawatesa sana watoto wanashindwa kupumzika na kuwa na afya njema, si mnajali sana afya bwana!!!
Na nyie madaktari mna vitu vingi sana upande wenu ambavyo vinawashinda, acheni kuhangaika na mambo ya elimu. Ama hamtaki nawanetu wasome kwa bidii wawe madaktari kama nyie?
Huu ushauri wenu utafutieni njia sahihi ikiwemo kuiambia serikali na walimu wapige marufuku counter books maana ndizo zinazoua migongo ya hao watoto mnaojifanya mnawajali sana.