Enzi zetu za shule

Umenikumbusha mbali sana, nilisoma Mwakaleli miaka ya 1995 (A Level) kuna mwalimu mmoja alikuwa mtaalamu wa Biology O - Level, hivyo vijana walimuita AMOEBA (Amiba) kwa jinsi alikuwa mtaalamu wa somo hilo lakini pia alivyokuwa rough.
 
wakati nasoma Songea Girls kuna mwalimu alikuwa na shingo fupi sana huyo tulikuwa tunamwita "tumchinjie wapi"
 
Mwalimu wetu wa Kiswahili form two alikuwa ndo kwaanza anatoka kozi; Topic yake ya kwanza ilikuwa ni Mofimu! Basi mpaka namaliza shule aliitwa mofimu!
 
Dah! kweli hii imenikumbusha mbali hata mimi, maana enzi hizo kwa wale waliosoma shule moja ya vipaji kaskazini mwa Tz wanaweza kuwakumbuka hawa.....
1. Mswahili (R.I.P) ------ Huyu ticha alikua mwalimu wa nidhamu alikua na vijisharubu hv na alikua akikubamba na soo tu neno la kwanza kumtoka ni "mswahili..."
2. Chifu ------- Huyu ni ticha mmoja wa kimasai alikua anapenda sana kuita watu chifu kwa mfano "chifu nitakukata vigongo" maana yake nitakupa stick. Jamaa alikua na misifa sana sijui kama hadi leo yupo.

3. Machakura (R.I.P) ----- machakura linatokana na neno chakula huyu ticha alikua ni Mkurya
4. Amanda ----- Jina hili lilitokana na tangazo la sabuni ya Amanda...nakumbuka huyu ticha alikua anafunisha geography
na wengineo wengi tu km Dudubaya, Rucockroach(Rumende)
 
Sijaona wadau wa Mzumbe Academic Village aka MAVI mpo kwenye JF?
Mara ya kwanza kutua Moro Mji kasoro bahari nilipendezwa sana na mazingira yake..ila nilipotua kwenye magofu ya mzumbe nikajua huku starehe yetu ni kitabu tuuu..Nawakumbuka sana mateacher kama
Anthony Wibonele aka Mkhomboti au alikuwa akijiita Tanzania One Physics (TOP) ..RIP
Msabila..(RIP) huyu nae alikuwa si haba kwenye Chemistry vijana walikuwa wanachezea mabanda tu kwenye NECTA...
Sifa moja ya wibonele alikuwa anafundisha Number na physics ilikuwa burudani tosha kwenye vipindi vyake..

Bila kumsahau Mkuu mwenye enzi hizo Thomas Dedemtula Msuka....
Wanamzumbe wanaweza kumalizia wimbo wa shule huu( ambao ulikuwa ukiimbwa J5 siku ya Ukaguzi wa Headmaster)
...Shule yetu Mzumbe sekondariiii ..Yasifika kote Tanzaniaa
..Malezi ya mzumbe..Elimu ya mzumbe....
( beti zimenipotea hapo..)
 
kuna mwalimu wangu mmoja wa primary tulimwita KENUA kutokana na tabia yake ya kukagua meno, so akikufikia anakwambia kenua, from there onwards ndo likawa jina lake
 
umenikumbusha mbali sanaaaa.
 
kijenge primary school kulikuwa na mwalimu anaitwa HAITOSHI.
Kila alipokuwa anaingia darasani akisalimiwa anasema haitoshi ,hivyo wanafunzi marudia kumsalimia anasema haitoshi kwa hiyo mnarudia tena na tena alikuwa anaitwa Mwl.Mujwauzi ni miqaka kibao cjui leo hii yuko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…