r.i.p trial balance wangu wa lugalo secondary iringa alifariki mwishoni mwa miaka ya tisini.
Bunsen burner.......huyu ni mwalimu wangu wa kemia form 1 na alinifanya nilipende somo kwa uhondo na namna alivyokuwa akilitamka jina la hicho kifaa cha maabara.
Sir ambi (sijui kama yupo hai) alikuwa mojawapo wa walimu ogopwa sana enzi hizo. Kutokana na u-seriousness wake watu walimpachika jina la sir
mheshimiwa comrade ...marehemu mwalimu materu ambaye aliwahi kututishia form one enzi hizo kwamba majina yetu yameandikwa kwa penseli kwenye rejista ya shule; hivyo kwake ilikuwa ni rahisi kutufuta! Akikuita lazima akwambie mheshimiwa comrade. Lakini wanafunzi ni wanafunzi; akiwa ni mwalimu wa somo la kilimo alikuwa ndiye msimamizi wetu wa orientation na orienatio enzi hizo ilikuwa ni kulima bustani (waliofika lugalo sekondari iringa wanalifahamu eneo husika linalimwa mboga mboga karibu mwaka mzima) vijana kwa kukwepa kazi tuliandikisha orodha ya majina kwa kuytaumia majina ya wachezaji wa yanga na simba wa enzi hizo! Tih tih ilikuwa patashika wakati wa gwaride la utambuzi mheshimiwa comrade alipokuwa anang'angania kumwadhibu a.k.a abedi mziba ama omari fungo na minziro wake!teh teh teh
headmaster wangu wa kwanza mwl mazengo aliwahi kuja shule kavaa raba enzi hizo zikiwa na jina maarufu la kuchumpa; ikawa soo kwani alimfuma mwanafunzi akiwaambia wenzie "headmaster kavaa la kuchumpa" yeye akatafsiri neno la kuchumpa ni kitu cha wizi! Ilikuwa mshike mshike na bahati mbaya sana alikuwa na kigugumizi!
Namshukuru mungu nilipata bahati ya kupita mikononi mwao pamoja na vituko vyote tulivyovifanya bado wao ndio ndio msingi wa mimi nilivyo sasa
jamani endelezeni safu!