EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

Nimesoma post za Muheshimiwa Zitto.

Kwa kweli huenda huyu kijana akawa Obama wetu siku za usoni!

Kwanza nakubaliana naye kabisa kwamba taifa letu linahitaji composition ya national assembly ... kuwa ruling part from 60%-70% na opposition 40%-30%... Hii ndiyo imekuwa hoja yangu milele regardless chama kitakachotawa kinaitwa shetani au malaika.

Kitila utakumbuka haya ndio niliyokueleza siku hile pale Dar es Salaam tulivyokutana kwa moja baridi moja moto.

Tena kwa kufanya mambo yawe matamu zaidi kusiwe na chama ambacho kinaweza unda serikali chenyewe... iwe lazima kitafute mshirika... e.g... chama chochote individually kisiwe na wabunge ambao ni zaidi ya 45% ya wabunge wote. Au kura za urais zaidi ya 50%

with the above composition we shall have health democracy which can bring change to our beloved nation.

Other than that maigizo tu!
 
Hivi is these for real ama changa la macho maana hii serikali yetu siyo ya kuwaamini hata kidogo!
 
hawatoleta chochote.. the only thing that is gonna happen is them being tried and convicted as per the evidence, which in this case is substantial in the sense that the plot was successful and the only thing left to be determined is the level of their involvment, if any... Due to the nature of the said crimes, it is in all likelihood that there is a good amount of documentary evidence implicating the suspects, considering the fact that they authorized the payments in collusion with kina-jettu&co. So lazima watafungwa tuu.

As a lawyer i'm certain that they will have a hard time raising doubt as to their guilt.. The likely defence is probably that 'They did not collude with the criminals and that they were unaware of the forgery' if they can raise that defence to a substantial level then wanaweza get away. But the public policy considerations make that unlikely too.. maybe a few of them will but not all under any circumstances..
 
Kinyambiss kati ya wote watakaofikishwa mahakamani, kesi ya hawa wanne ndiyo ya kuiangalia kwa ukaribu zaidi...
 
Dhamana ni haki ya kila Raia. Kama sheria zikitumika bila woga, haki itatendeka tu na watakaothibitika kuwa ni wakosaji watafungwa. Uchungu tulionao usitufanye tukikuke misingi ya Haki za Raia. Dhamana ni Haki na acha wapate kama wakitimiza masharti

Dhamana ni haki ya raia kwenye haki haki ya raia. Sheria zilishapindwa toka siku wameanza kubembelezwa kurudisha hela kwanza na kwa msingi huo haki ni vigumu kuamini itatendeka. Uchungu ni kweli tunao na tunajua wazi walioathirika kwa namna moja ama nyingine na vitendo vya hawa wezi (wengine kufa kwa kukosa dawa) - wao je hawakuwa na haki ? Wangapi wameswekwa rumande kwa kukosa dhamana, je wao hawana haki ? Kwa nini dhamana ihusishwe na nusu ya fedha walizokwiba, na si hujuma walioifanyia taifa na watu wake ? Hela za dhamana zinatoka wapi kama sio hizo hizo za wizi ambazo hakuna shaka zimezaa faida hata mara tatu. Kwa nini kiasi cha dhamana kisijumuishe na riba. Hapana Mh. Zitto hapa hamna cha haki wala sheria.
 
EPA yamnasa kigogo wa CCM

Akosa dhamana, yuko rumande

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima
Nov. 7, 2008


IDADI ya watuhumiwa wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezidi kuongezeka, baada ya jana watuhumiwa wengine watatu, akiwemo kigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajab Shabani Maranda, kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Mbali ya Maranda, ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha mkoani Kigoma, wengine waliofikishwa mahakamani jana ni mfanyabiashara maarufu wa mkoani Kilimanjaro na Arusha, ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Njanke Enterprises Ltd, Japhet Lema na Farijala Shabani Hussein.
Press nayo inaonyesha kuridhika na hatua za serikali dhidi ya "vigogo."

Tanzania Daima linadhani linafanya kazi nzuri hapa kwa kuonyesha kwamba vigogo wa CCM nao walikuwemo kwenye ufisadi, lakini wanavyo i-cover story, mwananchi ambaye hayuko well-informed anaweza kuamini kwamba 1) huyu mtu kweli ni "kigogo" 2) Serikali inafanya kazi nzuri ya kukamata pia vigogo 3) vigogo wakweli -the Mgonja's and Mramba's of the world - hawakuhusika.

Crummy press!
 
EPA yakumba vigogo BoT
Shadrack Sagati na Mariam Mogella
Daily News; Friday,November 07, 2008 @19:01

Wafanyakazi wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ijumaa walifikishwa mahakamani wakituhumiwa kushirikiana na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wanaodaiwa kuchota mabilioni ya fedha katika benki hiyo kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Wafanyakazi hao ni Mkuu wa Idara ya Madeni ya Biashara, Iman David Mwakyosa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni Ester Mary Komu na makaimu Katibu wa Benki wawili ambao ni Bosco Ndimbo Kimela na Sofia Joseph Lakila.

Kupandishwa kizimbani kwa watuhumiwa hao ijumaa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kunafanya idadi ya watu ambao wameshafikishwa mahakamani kufikia 17. Katika kesi ya kwanza, Mwakyosa, Komu na Kimela walishitakiwa kwa kuitia serikali hasara baada ya kuzembea na kusababisha wizi wa Sh milioni 207.8, mali ya BoT.

Washitakiwa hao ambao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja, wanadaiwa kuzembea na kusababisha wizi wa fedha hizo uliofanywa na Shaban Maranda. Katika kesi hiyo, Maranda ndiye anayetuhumiwa kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kisha kuiba kiasi hicho cha fedha kwa kutumia kampuni yake ya Lashhas Tanzania Ltd.

Alisomewa mashitaka hayo juzi ikidaiwa kuwa alidanganya kuwa Kampuni ya General Marketing Ltd ya Japan ilimruhusu alipwe deni hilo. Ijumaa vigogo hao wa BoT waliunganishwa katika kesi hiyo. Hakimu Mwankeja alitoa masharti ya dhamana yanayowataka washitakiwa wote waweke kiasi cha Sh milioni 104, hawaruhusiwi kusafiri nje ya Dar es Salaam. Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Novemba 20.

Kesi nyingine, Komu, Mwakosya na Sofia wanadaiwa kuzembea na kusababisha wizi wa Sh bilioni 2. 3 uliofanywa na Maranda anadaiwa kushirikiana na Farijala Hussein. Kesi hiyo ambayo iko mbele ya Hakimu Mkazi Warialwende Lema, inadaiwa vigogo hao wa BoT wakiwa na dhamana ya kulinda mali za benki hiyo walizembea kwa makusudi na kusababisha wizi huo kutokea.

Maranda na Farijala wanadaiwa kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kisha kuiba kiasi hicho cha fedha wakitumia kampuni ya Money Planners & Consultant. Waliiba fedha hizo baada ya kudanganya kuwa kampuni yao ilipewa mamlaka ya kulipwa fedha hizo na kampuni ya B. Glancel Ltd ya Ujerumani. Wote walikana mashitaka hayo na kesi hiyo itaenda mahakamani hapo Novemba 13 kwa ajili ya kutajwa.

Wakati huohuo, washitakiwa Godfrey Mosha na Davies Kamungu ambao wanashitakiwa katika kesi mbili za kuiba Sh zaidi ya bilioni mbili, ijumaa walipata dhamana. Washitakiwa hao wanadaiwa kufanya wizi huo kwa kutumia Kampuni ya Changanyikeni Resident Complex Ltd. Walipewa dhamana hiyo na Hakimu Lema. Wenzao watatu Bahati Mahenge, Manase Mwakale na Eddah Mwakale wanaendelea kusota rumande kutokana na kutotimiza masharti ya dhamana.
 
Press nayo inaonyesha kuridhika na hatua za serikali dhidi ya "vigogo."

Tanzania Daima linadhani linafanya kazi nzuri hapa kwa kuonyesha kwamba vigogo wa CCM nao walikuwemo kwenye ufisadi, lakini wanavyo i-cover story, mwananchi ambaye hayuko well-informed anaweza kuamini kwamba 1) huyu mtu kweli ni "kigogo" 2) Serikali inafanya kazi nzuri ya kukamata vigogo pia 3) vigogo wakweli -the Mgonja's and Mramba's of the world - hawakuhusika.

Crummy press!

Kuhani, waandishi wetu wakati mwingine huweka ushakibiki mbele kuliko ethics za journalism, shinda nyingine wengi ni maripota rather than waandishi, nadhani huyo ripota hajui kigogo ni yupi!
 
Jumla ya watuhumiwa 17 wakamatwa wizi wa mabilioni ya EPA
* DPP asema hakuna maneno, ni vitendo tu
Na Pauline Richard na Ramadhan Semtawa


MTEGO wa ufisadi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umeendelea kunasa watuhumiwa, na safari hii umewazoa wafanyakazi wanne wa benki hiyo ambao wamefikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma hizo.

Kwa idadai hiyo sasa watuhumiwa wa ufisadi huo waliokamatwa na kupandishwa kizimbani wanafikia 17.

Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani jana walitakiwa kujibu madai ya kuisababishia BoT hasara ya zaidi Sh2.2 bilioni za EPA.

Mwendesha Mashtaka wa serikali, Wakili wa Boniface Makulilo aliwataja watuhumiwa waliofikishwa mahakamani hapo kuwa ni Esther Leon ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Madai ya Biashara, Iman Mwakosya na Sophia Joseph ambao ni Wakuu wa Idara ya Madeni ya Biashara katika Benki hiyo.

Watuhumiwa hao wameunganishwa na mtuhumiwa Rajabu Malanda ambaye juzi alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Anyimilile Mwaseba na jana alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Warialwande Lema wa mahakama hiyo kwa kesi hiyo.

Katika kesi hiyo, Malanda alisomewa mashtaka sita na wafanyakazi wa BoT walisomewa shtaka moja la kuwa wazembe wakiwa kazini na kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Malanda alidaiwa kughushi hati bandia ya usajili iliyokuwa inaonyesha imetolewa na usajili wa Kampuni ya Manner Planner Consultant na kujipatia zaidi ya Sh2.2 bilioni.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa Novemba 29, 2005 Malanda aliwasilisha hati ya uongo katika Benki ya Biashara (Commercial Bank of Africa) iliyokuwa inaonyesha kuwa wao ni wamiliki wa Kampuni ya Manner Planner

Mtuhumiwa baada ya kuwasilisha hati hiyo inadaiwa alihamishia deni hilo katika Kamapuni ya B Grancers Company Limited ya Ujerumani na Kampuni ya Monner Planner ya Tanzania, baada ya kuonyesha hati hiyo, iliyokuwa imesainiwa na Jonas Banji na Fundi Kitunda kwa madai kuwa wao ni wakurugenzi wa kampuni hizo.

Katika shtaka jingine inadaiwa Novemba2, 2005 mshtakiwa Malanda na Farijala Husein waliwasilisha hati ya uongo ya Kampuni ya BG Monner ambayo ilikuwa inaonyesha kuwa imesainiwa na Mkurugenzi wa Makampuni na kuiwasilisha BoT.

Baada ya kuwasilisha hati hiyo BoT, watuhumiwa hao walijipatia zaidi ya Sh2.2 bilioni mali ya BoT.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Desemba 7 mwaka 2005 watumishi hao wanadaiwa kufanya uzembe na kusababisha hasara kwa mamlaka maalumu ya Benki hiyo wakiwa kama wakurugenzi wa idara ya madai wa BoT.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana kuhusika na tuhuma hizo na mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13 mwaka huu watakaposomewa maelezo ya awali, baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Watumishi hao wa BoT wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh450 milioni na kwamba hawatatakiwa kusafiri nje ya Dar es Salaam pamoja kuwasilisha pasipoti zao za kusafiria mahakamani hapo.

Wakati moto huo ukiwawakia watuhumiwa hao huku wakidaiwa kutoroka, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mmoja baada ya mwingine.

Kauli ya DCI ambaye kurugenzi yake ndiyo yenye mamlaka ya kukamata wahalifu baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutoa kibali, imetolewa wakati Watanzania wakitaka kuona watuhumiwa wote wa fedha za EPA zaidi ya Sh 133 bilioni wanakamatwa.

Hadi jana mchana, mmoja wa watuhumiwa ambaye amesomewa mashtaka bila kuwepo mahakamani kwa madai yuko nje ya nchi, Mwesiga Lukaza alikuwa bado hajakamatwa.

Akizungumzia mtuhumiwa huyo na mchakato wa kuwakamata wahusika, Manumba, alisema ni suala la wakati tu kwani hakuna mtu atakayepona.

Mwesiga na ndugu yake Johnson Lukaza, wote wanakabiliwa na makosa sita, ambayo ni pamoja na kughushi nyaraka kwa kutumia Kampuni ya Kernel Limited of Tanzania na Marubeni Corporation ya Japan na kujipatia mabilioni ya fedha.

Hata hivyo, ni Jonhson ndiye aliyefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka hayo huku Mwesiga akiwa bado kupatikana akidaiwa kwamba yuko nje ya nchi.

Akizungumzia zaidi hilo, Kamishna Manumba alisema; "Sipendi kusema sana kwani yupo kiongozi wetu ambaye ni DPP (Eliazer Feleshi), lakini ninachoweza kusema ni kwamba, ni suala la wakati tu, hakuna mtu atapona," alionya Kamishna Manumba na kuongeza:

"Kama mnavyoona tunawapeleka watu kwa ‘phase’ (awamu), lakini DPP ndiye anayefahamu zaidi nani atapaswa kwenda lini, sisi kazi yetu ni kuwakamata tu."

DPP Feleshi alipoulizwa kuhusu mchakato wa kuwafikisha mahakamani, alisema kinachofanywa na ofisi yake sasa kinaonekana mahakamani kila siku na huko ndiko utakaojulikana ukweli.

DPP Feleshi kama alivyo Kamishna Manumba, ambao wote huwa na ushirikiano mzuri na vyombo vya habari, alisema ameona sasa azungumze kwa vitendo si maneno.

"Sasa hivi kila kitu kinafahamika mahakamani, maana sipendi kuzungumza maneno mengi zaidi ya yale yanayojiri mahakamani kila siku, ni vitendo tu si maneno," alifafanua DPP Feleshi.

Alisema, huu si wakati wa kutoa maneno mengi nje ya mahakama, kwa sababu mchakato huo sasa unafanyika kortini, ambako mambo yote hujibainisha.

Kauli za vigogo hao wa wawili kutoka upande wa mashtaka na polisi, zimetolewa wakati kila siku kuna watu wapya wanakamatwa kwa tuhuma za ufisadi wa EPA na kupelekwa mahakamani.

Maelezo hayo ya DCI na DPP yanazidi kuwaweka watuhumiwa wa EPA katika wakati mgumu, wakiwemo wale waliorejesha zaidi ya Sh69 bilioni ambao wanadhani wamesamehewa.

Kauli hizo pia zinazidi kuwaweka mafisadi wa EPA katika hali tete, kutokana na duru za kiserikali kuonyesha kwamba fedha zilizorejeshwa huenda zikawa kidhibiti cha kukamata watu hao kwa urahisi kwamba walihusika na ufisadi.

"Si kwamba wamekwisha, bado mzee, mambo taratibu, mchakato unaendelea na wananchi wataona, serikali imejipanga vizuri katika hili," kilisema chanzo hicho.

Ufisadi ambao umebainika katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, unahusu Sh90.3 bilioni ambazo ziliibwa na makampuni 13 kwa kutumia nyaraka za kughushi.

Pia unahusu Sh42.6 bilioni zilizolipwa kwa makampuni tisa, katika mazingira yenye utata huku taarifa nyingine za wizi huo zikiwa nje ya nchi, hali iliyomfanya Rais kuongeza muda wa uchunguzi kutoka Agosti hadi Oktoba 31.

Source: Mwananchi
 
Kuhani, waandishi wetu wakati mwingine huweka ushakibiki mbele kuliko ethics za journalism, shinda nyingine wengi ni maripota rather than waandishi, nadhani huyo ripota hajui kigogo ni yupi!

Mbali ya ushabiki, either hawajui kuchagua vichwa vya habari au wanaweka makusudi kichwa habari wanachoona kitavutia watu kununua gazeti. Lakini gazeti la Tanzania Daima linanunuliwa sana, hawana sababu yoyote ya msingi ya kuweka vichwa vya habari vya kuwadanganya wananchi, Hivi Wahariri kazi yao ni nini? Mhariri wa Habari ama hata Mhariri Mkuu wa Tanzania Daima hawezi akarekebisha kichwa cha habari pale kinapoonekana hakitoshelezi?
 
Oyaaa wakuu. Lukaza tayari yupo nje kwa dhamana!

Watu wajanja, wameacha kurudisha ili ziwasaidie kwenye kesi.

Nakumbuka JK alisema kuwa jamaa wanajikaza tu ila wamemalizwa kiaina. Sasa naanza kuona Mchezo unaochezwa hapa. Kama Johson alirudisha hela mpaka akashindwa kurudisha amepata wapi hizo za kujidhamini???????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mwenye akili afikirie mara mbili.

..........FP je unakumbuka Makubo style............na Sembe Chapa Jogoo?.......this time...labda JK mwenyewe aamue kula shubiri........lakini kwa ushahidi uliopo haponi mtu........
 
innocent until proven guilty.....
Ndio maana bail ni haki. Na kama wana wakili mzuri anaweza aka question iyo bail amount iliyowekwa, maana inakuwa sawa na kuwanyima bail. The amount is too high, assuming they are innocent they wouldnt have that much

Mrembo karibu sana jamvini.

Hapo juu Mrembo kweli umeniacha hoi...Hii lazima ni style ya cat walk hiyo maana warembo mambo hayo mnayajuwa zaidi.

Kweli Mrembo tunaweza ku assume kwamba watuhumiwa wako innocent na wamesingiziwa kuwa walichukuwa pesa hizo za EPA.

Hata hivyo mrembo naomba nikukumbushe kuwa uwezekano huo ni finyu sana kwani ushahidi uko wazi na kama ni kusingiziwa basi hawajasingiziwa...Tofauti inaweza kuwa kwenye technicalities tu..Lakini kama ni makosa wamefanya.

Pia amount ya bail kuwa juu inawezekena kushushwa kama unavyodai endapo utaendelea ku assume kuwa pesa zilitochotwa ni ndogo sana.
 
Kama Johson alirudisha hela mpaka akashindwa kurudisha amepata wapi hizo za kujidhamini???????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! !!!!!!!!!!

Mwenye akili afikirie mara mbili.

Mkuu heshima yako, ni kwamba familia ya Lukaza, wanazo hela hata kabla huyu bwana mdogo hajaingia ufisadi, ndio maana ndugu zake ambao nimeongea nao sana wiki hii wanasema hawaelewi nini hasa kilichompeleka huko BOT,

Baba yake alikuwa kibopa toka enzi za awamu ya kwanza, ndugu zake wote ni vibopa longtime, tena wote wake kwa waume, ni yeye tu aliyezidisha tamaa na sasa amechafua sana jina la baba yake na la familia yake kwa ujumla, bila sababu ya msingi wakati wao ni watu wa pesa siku zote, hiyo dhamana ambayo ni ndogo sana wka ndugu zake anaweza kua amelipiwa na sister wake mmoja tu na sio ndugu zake wote, I mean mnyonge mnyongeni lakini haki apewe.

Bwana mdogo aliichokoza serikali yeye mwenyewe, pale aliposhusha Range kwenye ndege ya British Airways, akimuiga Joemaro, hakujua kua huyu ni mkwe wa mkapa!

Tuliambiwa watuhumiwa wa EPA hawataenda mahakamani kwa sababu rais anawaogopa hawa, maana aliiba nao hela za kampeni, sasa hawa wako kizimbani, dhamana ni haki ya kila mwananchi kulingana na makosa yake kisheria, tayari tumeshaambwia kwamba hili ni kundi la kwanza tu, baadye linakuja na lingine la wakubwa, wallahi kuna mtu mzima hapa yupo hatarini, maana according to the dataz hata kesi wa wakulu wa Kiwira ipo tayari na pending.

Dawa ni kuvuta popcorn na kuiachia sheria ichukue mkondo wake.
 
Tumeambiwa kuwa KAGODA imerudisha 37 bn mpaka sasa. Hajapelekwa mtu wa kagoda mahakaman mpaka sasa. Nimeambiwa kuwa Manji ndio karudisha pesa za KAGODA. Tunafuatilia zaidi.

Mpaka sasa hatua ya kuwapeleka mahakani waliopelekwa ni ya kuupongezwa sana. Lakini tusibweteke, bado kazi ni kubwa sana. Lazima kuhakikisha kuwa suala kama hili halitokei tena nchini kwetu. Ukweli wa EPA na Uchaguzi mkuu wa 2005 ni lazima ujulikane ili isitokee chama kingine chochote cha siasa kujaribu kutumia fedha za Umma kwa minajili ya kufadhili uchaguzi.

Kuna mengi ya kujifunza kutokana na sakata hili la EPA. Tunaenda vizuri sana. Press imefanya kazi nzuri sana. Wanasiasa tumefanya kazi nzuri sana. DPP kaanza vizuri. Rais, japo amechelewa mno, amefanya vizuri. Kauli ya kutomwingilia DPP ni kauli ya kiuongozi na itamfanya DPP awe huru zaidi katika kazi yake. Rais amefanya vizuri.

Hapa ndipo nafasi ya upinzani inapoonekana. Nafasi ya vyombo vya habari inapoonekana. Kuna haja kubwa sana kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao vyama vya upinzani vinakuwa na angalau theluthi ya wabunge. Hapa nina maana hata CCM ikishindwa uchaguzi ujao, iwe na angalau theluthi ya wabunge ili CHADEMA nayo isibweteke

Thanks Zitto,

ila kumsifia DPP wakati serikali haijashinda kesi hapo BIG NO.......Inawezekana kaona wanakesi ya kujibu ili mahakama iwasafishe....Kuwa makini hapa...
 
Mkuu Field Marshall ES, nakuaminia kwa data lakini kwenye hilo la Kina Lukaza uko nje mno ya ukweli.

Ni kijana mwenzetu na mimi binafsi sababu namfahamu toka miaka ya 80, namwombea yeye na familia heri na baraka na apate unafuu na kuepuka jail time. Ni mawazo binafsi tu.
 
Mkuu hawa wote mpaka wamefika hapo tayari ni wezi ushahidi upo wazi kabisa.
Hawana hata haki ya kujitetea ni wezi kabisa hao.Kuwapa nafasi ndo kuharibu ushahidi wa kesi yao utaona kesi hii inaweza ikasomwa hata miaka 30 ijayo nyie mtaona tu.Baadae mshitakiwa anakufa kesi inafutwa.

...mkuu polepole na tusiharibu taratibu za demokrasi yetu kwa emotions zetu,fair trial kwa raia wote ndani ya jamhuri ndio maana ya uhuru,acha wajitetee,wapewe lawyer wa kuwatetea na dhamana ambayo ni reasonable,hakuna haja ya kukomoana lazima taratibu zifuatwe no matter what happened ili kulinda haki ya kila mtu!
 
Mkuu Field Marshall ES, nakuaminia kwa data lakini kwenye hilo la Kina Lukaza uko nje mno ya ukweli.

Ni kijana mwenzetu na mimi binafsi sababu namfahamu toka miaka ya 80, namwombea yeye na familia heri na baraka na apate unafuu na kuepuka jail time. Ni mawazo binafsi tu.

Labda kama wako wawili, lakini ninayemjua familia yake iilikuwa inaishi Upanga, dada yake ambaye ameolewa na mshijaki wangu mmoja wa primary school anamiliki kampuni kubwa sana ya Tele/Communications pale jengo la CRDB, na kaka yake mwingine anamiliki kampuni kubwa sana ya kupeleka watalii mbugani kule Arusha na nikiwa majuu nimemsaidia sana kuwaelekeza watalii kwake, I mean a I can go on and on, unless tunawawaongelea Lukaza wawili tofauti!

Hizi sio dataz, ila ni ukweli wa kawaida tu wa familia ninayoifahamu na ndio maana nimekua kwenye communication nao wiki hii nzima, that is all sikusema hizi ni dataz, lakini unakaribishwa sana ila tu yasiwe yale yale maana tayari naona harufu!

Thanxs!
 
Labda kama wako wawili, lakini ninayemjua familia yake iilikuwa inaishi Upanga, dada yake ambaye ameolewa na mshijaki wangu mmoja wa primary school anamiliki kampuni kubwa sana ya Tele/Communications pale jengo la CRDB, na kaka yake mwingine anamiliki kampuni kubwa sana ya kupeleka watalii mbugani kule Arusha na nikiwa majuu nimemsaidaia sana kuwaelekeza watalii kwake, I mean a I can go on and on, unless tunawawaongelea Lukaza wawili tofauti!

Hizi sio dataz, ila ni ukweli wa kawaida tu wa familia ninayoifahamu, that is all sikusema hizi ni dataz, lakini unakaribishwa sana ila tu yasiewe yale yale!

Thanxs!

Mkuu sasa umejileta wala sikuachii huyo kaka yake mkubwa anaitwa Emanuel Makubo na yeye ndiye aliyemfundisha huo ufisadi
Huyu makuba waliibaga pamoja na Chavda wakati ule
Hamna cha kuwasifia ukoo wao wote wezi tuu Johnson mwenyewe keshafungwa Mwanza Kwa wizi
Hamna lolote zaidi ya kujikuza tuu si unajua mabwenga walivyo
 
Back
Top Bottom