Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Kuna wakati nilikuwa safarini kule Kigoma, magahaibi mwa Tanzania. Nikiwa kule niijaribu kufuatilia madai ya Mnyika kuhusu kusambaratika kwa Tawi la CHADEMA liitwalo Urusi baada ya Makamba kufanya ziara kule. Mnyika alidai kuwa Makamba aliwanunua baadhi ya vijana wa Ngome hiyo ya CHADEMA ya Urusi pale Mwanga. Pia alidai kuwa Urusi haijasambaratika (ni kweli haijasambaratika bali imezaliwa 'Urusi yenye nguvu').
Nilipododosa kwa baadhi ya wenyeji wa Mwanga ambao si wana CHADEMA walinithibitishia kuwa baadhi vijana wa CHADEMA wa Urusi walipewa shilingi milioni 15 ili wajiunge na CCM ili kuiua Urusi. Tukio lile lilisababisha mgawanyiko kwa Vijana wa urusi na mgao ulichukuliwa na vijana 3 tu.
Katika habari zile wapasha habari waliniambia kuwa zile fedha hazikuwa za Makamba wala CCM bali zilitolewa na kada mmoja wa CCM mkoani Kigoma anayeitwa Rajab Maranda na wakaendelea kusema kuwa Maranda ambaye ni mfanyabiashara maarufu na Alwatan pale Kigoma mjini ni mmoja wa Watuhumiwa wa pesa za EPA. Wakati ule zilikuwa ni tetesi na pengine ningeleta hapa ningeambiwa huo ni udaku au nithibitishe.
Baada ya Wtuhumiwa wa EPA kufikishwa mahakamani, Rajab Maranda akiwa mmojawapo nimeamini madai ya Mnyika na kuwa ni kweli Kada huyo wa CCM alijichotea pesa za EPA, na ni pesa hizo hizo ambazo Mkamba alizitumia kuwahnga vijana wa ngome ya CHADEMA wa Urusi ili kuisambaratisha CHADEMA Kigoma. Ukweli ni kuwa CCM haiwezi kuepuka tuhuma kuwa ilitumia pesa za EPA kwenye harakati zake za kisiasa hapa nchini.