EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

Kuna wakati nilikuwa safarini kule Kigoma, magahaibi mwa Tanzania. Nikiwa kule niijaribu kufuatilia madai ya Mnyika kuhusu kusambaratika kwa Tawi la CHADEMA liitwalo Urusi baada ya Makamba kufanya ziara kule. Mnyika alidai kuwa Makamba aliwanunua baadhi ya vijana wa Ngome hiyo ya CHADEMA ya Urusi pale Mwanga. Pia alidai kuwa Urusi haijasambaratika (ni kweli haijasambaratika bali imezaliwa 'Urusi yenye nguvu').

Nilipododosa kwa baadhi ya wenyeji wa Mwanga ambao si wana CHADEMA walinithibitishia kuwa baadhi vijana wa CHADEMA wa Urusi walipewa shilingi milioni 15 ili wajiunge na CCM ili kuiua Urusi. Tukio lile lilisababisha mgawanyiko kwa Vijana wa urusi na mgao ulichukuliwa na vijana 3 tu.

Katika habari zile wapasha habari waliniambia kuwa zile fedha hazikuwa za Makamba wala CCM bali zilitolewa na kada mmoja wa CCM mkoani Kigoma anayeitwa Rajab Maranda na wakaendelea kusema kuwa Maranda ambaye ni mfanyabiashara maarufu na Alwatan pale Kigoma mjini ni mmoja wa Watuhumiwa wa pesa za EPA. Wakati ule zilikuwa ni tetesi na pengine ningeleta hapa ningeambiwa huo ni udaku au nithibitishe.

Baada ya Wtuhumiwa wa EPA kufikishwa mahakamani, Rajab Maranda akiwa mmojawapo nimeamini madai ya Mnyika na kuwa ni kweli Kada huyo wa CCM alijichotea pesa za EPA, na ni pesa hizo hizo ambazo Mkamba alizitumia kuwahnga vijana wa ngome ya CHADEMA wa Urusi ili kuisambaratisha CHADEMA Kigoma. Ukweli ni kuwa CCM haiwezi kuepuka tuhuma kuwa ilitumia pesa za EPA kwenye harakati zake za kisiasa hapa nchini.
 
Janja yake kwisha gundua. Anajua kuwa Desemba inakaribia na ataulizwa kuhusiana na zile kesi kumi kubwa za rushwa ambazo yeye mwenyewe alisema kuwa ndilo lengo la taasisi yake kwa mwaka. hadi sasa hajafikisha mahakamani hata kesi moja na anaanza kujitetea kabla hajaulizwa.
tafadhali Hoseah, tafuta utetezi mwingine, janja hii tumeshaibaini. Na kwa hakika hatutaki utetezi, tunachotaka ni wewe kutimiza ahadi yako kuwa taasisi yako itahakikisha inafikisha kesi kumi kubwa za rushwa kila mwaka. Mwaka unakwisha na tunazitaka kesi kumi kubwa za rushwa. kama umeshindwa kutimiza malengo ambayo ulijiwekea mwenyewe, ni vema ukaachia ngazi, ndio ustaarabu
 
-TUKIWASHITAKI WOTE UCHUMI WA NCHI UTAYUMBA
Wanandugu maneno haya yamentisha si kidogo bali ni kwa hali ya tahadhar kwa kusikia maneno kama haya toka kwa mtu mkubwa kama huyu
kwamba mafisadi wameshika nchi hii so ni vigumu kuwafkisha wote !!!
JF NAOMBA TUSHAURIANE KWA HILI!!!!
kwangu mimi nahisi uchumi umeshayumba kama yeye binafsi hosea mshitakiwa na mshiriki halisi wa EPA ,bado ndie kinara namba moja kuchunguza fisadi wenzake!!!
pili ....tuwaachie wenyewe

Huyo Hosea yeye mwenyewe ni fisadi na kamati ya Mwakyembe ilipendekeza aondolewe TAKUKURU inashangaza mpaka hii leo bado anapeta na kutoa kauli ambazo Watanzania hatuwezi kuzikubali hata kidogo. Kikwete inabidi amfukuze kazi haraka sana na pia kumtaka atoe hiyo list ya mafisadi walioshikilia uchumi wa Tanzania.
 
hao CHADEMA walipokea zanini lol... wastemanz

Hata wao sisiem waliwahi kutuambia tukipewa tupokee lakini siku ya mwisho ya kupiga kura tuongee na karatasi na kalamu yetu tu. kama walitoa 15m kwa watu watatu basi labda wana kura 3 tu, lakini daima Urusi ni CHADEMA,,,,,
 
imeshindwa kabisa kupata habari kuhusu mahabusu ambayo hawa jamaa wa EPA scandal wanashindia.

Wana JF kwa mwenye habari aiweke hapa.
1. Iko wapi?
2. Ikoje?
3. AOB

Thanks
 
Haitayumba ila inayumba kwa kwa sababu ya walovyoiba na tukiwafunga wote tutafanya kazi kwa true level tuliyonayo na itakuwa na manufaa zaidi kwa GDP kwani walipa kodi wataongezeka kwa kuwa hawa waliomo wengi ni wakwepa kodi na wezi kwa pamoja. Tunaondoa tabaka flani au siyo?
 
Mkuu kilbark,

Dr. Hoseah siyo kwamba kazi haiwezi,Tatizo la nchi hii linaongozwa kisiasa na hauwezi kuanza kukurupuka kuwashtaki watu bila ya kumuuliza Mkulu wa nchi.

Ngoja nikupe mfano wa suala la EPA,Baada ya Kugundulika Pesa za EPA zimeliwa mkulu aliogopa moja kwa moja kuwachulia hatua wale wezi wakaweka siasa na kujaribu kuhadaa wataznaia kwamba hao ni watu wazito na utakumbuka hata mzee mkaramba alishwahi kulizungumza hili bungeni.

Mathalani DPP kapewa Zigo zito sana ambalo lilimsihindwa muungwana na DPP alikuwa na moja kuchagua kufuata anachokiamini au kuacha waje wahukumiwe na Rais na yeye alichagua njia iliyo bora na Sahihi.

Nakumbuka kipindi chetu enzi za Mwalimu ilikuwa siyo RAhisi watu wa namna hii kupona,ulikuwa ukighundulika tu unawekwa ndani na mammbo mengine yanafuatwa.

Kwa upande mwingie watu wa EPA ni wazito sababu wanamilipi pesa nyingi katika Uchumi na kuwagusa inabidi uende kwa njia sahihi na kwa uangalifu Mkubwa sana,ila naamna DPP na kwa misimamo yake basi atawafikisha mahakamani mara moja.Nakumbuka niliwahi kuzungumza naye punde kabla ya kuteuliwa na rais kuwa DPP alinieleza msiamo wake kwamba wasomi kama sisi tunahitaji kuleta madailiko ya utendaji katika serikali yetu na alinishauri hata mimi nikipata nafasi ya utezi nisifanye kazi kwa uoga.

Nina Imani na DPP na hata Dr. Hoseah,Uzoefu wake katika idara ya Usalama wa taifa itasaidia sana kufanya maamuzi ambayo hayatathiri mwenendo wa serikali na nchi yetu kiujumla.

Tuwe Wavumilivu

Nazidi kuwa na wasi wasi! Kwanza siamini kinachoendelea na unaposema tuwe wavumilivu ni kama unanipa nusu kaputi hivi!!
 
SEGEREA aka SEGA DANCE!!....kwa mujibu wa sheria, ila mmmh isije kuwa jamaa wanalala Landmark Hotel Ubungo, halafu asubuhi wanaamkia mahakamani...Dar es Salaam hakuna linaloshindikana ukiwa na pesa!
 
Tuache uzushi jamani, hawa mahabusu wako rumande aliko Zombe, yaani Keko labda kama huko Keko ndani kuna Hilton special kwa ajili yao, hebu turuhusu mkono wa sheria ufanye kazi yake sasa maana tulisema hawatashikwa hata siku moja, tukaambiwa Lukaza yupo Dubai, na blah! blah!,

Sasa kesi inaunguruma bado tu tunazidisha maneno yasiyokuwa na ukweli ili kuendeleza tu hizi conspiracy theories, hebu tutulie wakuu tuangalie kesi walizonazo, kama kweli kuna a strong kesi, au ni hadithi tu maana tukumbuke kuwa na wao watuhumiwa wana haki ya kujitetea mahakamani, sasa wasije wakaachiliwa tukaanza kutafutana kumbe hakukuwa na kesi anyways ilikuwa ni a political ploy!.

Kama Zombe yuko Rumande, hakuna mwingine wa kuwekwa nje ya huko.
 
Hivyo vijifisadi vilivyokamatwa vinashikilia uchumi gani. Watu wanaoshikilia uchumi wa hapa ni wafadhili na wakichoshwa na usanii wetu wakakataa kutupa pesa zao ndio kweli nchi itayumba na kwenda mrama. Hayo maneno ni ya kisanii watanzania si mambwege tena. Hao mafisadi wengi wanavijibiashara vya binafsi na wala biashara zao zilikuwa hazina faida ndio sababu wakawa wezi na wengi vijihela vyao vimefichwa dubhai au nchi za kihuni .na wameshanunua vijiapatmenti kwenye vinchi kama maurisius, dhubai,malta,Sausi etc. Uchumi gani utayum ba??????? labda wa mafisadi.

Wajinga nakubaliana na wewe na kwa kuongezea ni kuwa kama ni kweli wanavyodai kuwa wameshikilia uchumi...Then tuna haki ya kuwaambia wauachie kwasababu sidhani kama uchumi wenyewe ni mzuri hapo bongo..Kwa maana hiyo ni kwamba wanataka waendelee kuuharibu uchumi kama ambavyo wameshafanya....Pointi ya kushikilia uchumi haina mantiki kabisa....Kama kuujenga uchumi ndio kuwalinda mafisadi wanaoushikilia...Then hii ni mpya kwangu.
 
Wajinga nakubaliana na wewe na kwa kuongezea ni kuwa kama ni kweli wanavyodai kuwa wameshikilia uchumi...Then tuna haki ya kuwaambia wauachie kwasababu sidhani kama uchumi wenyewe ni mzuri hapo bongo..Kwa maana hiyo ni kwamba wanataka waendelee kuuharibu uchumi kama ambavyo wameshafanya....Pointi ya kushikilia uchumi haina mantiki kabisa....Kama kuujenga uchumi ndio kuwalinda mafisadi wanaoushikilia...Then hii ni mpya kwangu.


Kumbe anataka kusema uchumi wa nchi uko mikononi mwa jitu patel et al? Au kama wanavyojiita mafia wa atanzania? Disturbing a lot them minds aah!

They are non tax payers as they evade a tax and swindle fedha za umma.

Ni sawa kama uchumi wa tanzania ni wa kifisadi na kama pia aina ya siasa tulojichagulia basi iandikwe katiba yake ili tujue mustakabali wa watu wa chini katiba hiyo ita-take vipi care.

Au kama katiba ya sasa inatoa uamuzi huo kupitia mahakama basi ni sawa au kama hosea ni mahakama aseme ni sheria ipi inamruhusu na ni mahakama gani imekaa kutoa uamuzi huo haswa ukizingatia kuwa kesi za namna hii ni kesi kwa mafisadi kutoka kwa watanzania wote.

It is a thinking of a shame!!!
 
Heshima mbele wakuu.... pamoja na kwamba tunajaribu kuruhusu sheria kufuata mkondo wake na kuacha speculation kama tulivyoshauriwa na wengi, hii kitu nimeisoma kwenye Thisday ya leo (12 Nov 2008) kidogo inanichanganya kichwa.... watu wameshaanza kuua "orginal players".....

Since kuanzia mwanzo watu tulikuwa tupo concerned na hii Kagoda sasa naona kweli kama habari hii ina ukweli (manake inazidi ku conceal names and identities) inanifanya kidogo nianze kuamini kwenye conspiracy theories so far presented in this topic!

Haya, ngoja tuzidi kuangalia na kutega masikio, ila wajue kuwa waTz tumeshaamka sio mambo ya mwaka 47 tena.... Aluta Continua!!

In Kagoda, dead men tell no tales

TWO business tycoons linked to the external payment arrears (EPA) account scandal through the infamous Kagoda Agriculture Limited company are reportedly blaming the theft of more than 40bn/- from the Bank of Tanzania to a dead man, in an elaborate ploy to avoid criminal charges.

It has now been revealed that a prominent businessman based in Dar es Salaam told EPA investigators that his deceased father was the actual beneficiary of over $30.8m (approx. 40bn/-) fraudulently paid to Kagoda from the key BoT account.

In doing so, the tycoon accepted financial liability and returned all the stolen funds to the government before the October 31, in an attempt to avoid criminal charges.

’’The businessman agreed to pay back the stolen EPA funds, but sought to avoid criminal liability by claiming that it was actually his deceased father who stole the funds,’’ said a source close to the EPA investigation.

He added: ’’He (the business tycoon) claimed he had nothing to do with the Kagoda company, but agreed to return all money purportedly stolen by his dead father. This is, of course, all part of an elaborate trick to try to avoid criminal charges.’’

Sources say the businessman who claimed the Kagoda funds were stolen by his deceased father was actually used to camouflage the involvement of another prominent business tycoon with vast interests, who was the real architect of the looting.

’’Some sort of an agreement was reached between these two businessmen to try and conceal the identity of the man behind the Kagoda company, who is a well-known public figure,’’ said another well-placed source.

Government officials said aides to the businessman who masterminded the massive looting of funds from the BoT through Kagoda had scrambled to surrender billions of shillings to the government on behalf of the shell company to avert the case from going to the courts for prosecution.

In the final few days leading up to the October 31 deadline, aides to the Kagoda businessman were seen carrying suitcases full of cash to a commercial bank located along Samora Avenue as they rushed to return the stolen funds to the government.

’’Actually, the businessman who was used to camouflage the involvement of the Kagoda architect panicked and almost fled the country recently at the prospect of going to jail. He now appears to have somewhat relaxed after all the stolen money was returned to the government by the Kagoda man,’’ said one of our sources.

So far, a total of 20 suspects have been arraigned at the Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar es Salaam in connection with the EPA scandal.

They include business tycoon Jeetu Patel, who faces multiple counts of conspiracy, fraud and theft charges in the EPA scam in four separate criminal cases before the court.

Jeetu Patel has reportedly already returned more than 35bn/- to the government from the EPA account, but was still unable to avoid criminal charges.

However, the powerful forces behind the Kagoda company who are known to be well-connected individuals, remain conspicuously missing from all the high profile action in the court.

’’It is true that this businessman?s father died abroad ?. However, the real beneficiary of the Kagoda funds is trying to use a dead man to avoid criminal charges,’’ said another source familiar with the so-called ?dead-man? ploy.

He added: ’’After all, investigators cannot question a corpse, can they?’’

Source: Thisday
 
Thisday wamuelezea Manji wa Kagoda, he he he heee.
 
Msiwaonee wahindi peke yao ? Dunia nzima inalitazama soo hili kwa undani kabisa na matokeo yake,hivyo kuonekana sura nyingi za wahusika ni za wahindi na makampuni yao hivi jamaa zetu hawahusiki ?
 
Ndugu wa watuhumiwa EPA walia na dhamana
Pauline Richard

BAADHI ya ndugu na jamaa wa wafanyabiashara wanaotuhumiwa wa wizi wa Sh133 bilioni zinazodaiwa kuchotwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania wameitupia lawama Ofisi ya Uhakiki wa hati miliki za majengo kwa kushindwa kuwapa hati miliki za nyumba zao ili waweze kutimiza masharti ya dhamana kwa ndugu zao.


Wakizungumza na Gazeti hiyo jana, ndugu hao walisema kuwa ofisi hiyo imekuwa kikazo kikubwa kwa ndugu zao kuendelea kusota rumande. Mpaka sasa ni watuhumiwa wawili kati ya 20 waliotimiza masharti ya dhamana.


Ndugu hao walidai kuwa siku ya kwanza baada ya ndugu zao kufikishwa mahakamani hapo walikwenda katika ofisi hiyo iliyopo katika jengo la Wizara ya Ardhi, lakini wakakuta ofisi hiyo imefungwa hivyo kukwamisha zoezi la kuwadhamini ndugu zao.


Mpaka sasa watuhumiwa 20, kati yao wakiwamo watatu ni wafanyakazi wa BoT wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mbele ya mahakimu tofauti. Kati ya hao watuhumiwa wawili tu ndiyo waliotimiza masharti ya dhamana na tayari wako nje.


Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi waka wakati tofuati kuanzia wiki iliyipita na kuwekewa masharti magumu ya dhamana ambayo wengi wao wameshindwa kutimiza.


Wtu hao ambao sasa wako mahabusu wanashitakiwa kwa tuhuma mbalimbali zinazohusiana na upotevu wa mabilioni ya shilingia EPA ikiwamo kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu na uzembe katika kusimia taratibu za utoaji fedha BoT.


Karibu maofisa wote wa BoT wameshtakiwa kushiriki katika kashfa hiyo kutokana na uzembe wao katika kusimamia na kudhibiti mwenendo wa fedha kupitia nyadhifa nyadhifa zao. Watuhumiwa hao walikamatwa na kufikishwa mahakamani ili kutekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyotoa wakati akilihutubia Bunge la bajeti mwishoni mwa Agosti mwaka huu, kwamba atakayeshindwa kurejesha fedha anazotuhumiwa kupora ifikapo Oktoba 31, afikishwe mahakmi mara moja.


Wakati hao wakifikishwa mahakamani, baadhi ya wananchi wamesema wanaendelea kusubiri kuwaona watu maarufu wanatinga kortini, kwani wanaamini kwamba waliofikishwa ni mafisadi wadogo.
 
Back
Top Bottom