Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Friends:
This is for you. Please register as early as possible, limited number of seats available. you will get to know more about this kind of Business (Forex Trading). Attached advert has more information.
Free Online Forex Trading Seminar
When: Friday, November 28, 2008:
Time: 05:00 pm-07:00 pm.
Speaker: From Nairobi
Where: Azania Front (Underground Hall)
Register: Mramba Nkalangango (mrambagsn@hotmail.com)
Kuhusu familia hizo kuwa na pesa kabla ya EPA hilo linawezekana...Kwa mfano Njake alikuwa na pesa kabla ya EPA.
Mkuu samahani,
Lema aka Njake aka 7Up ni mtu wa 'shughuli' siku nyingi. Alikuwa na pesa ndio, za uharamia wa kila aina ya biashara. Ameanza hizi kazi za uchafu siku nyingi ndio maana sikushangaa nilipomwona ametajwa kwenye hili. Ila nimeona picha yake kweli wakati ukuta...amezeeka sasa
Watuhumiwa EPA wafikia 20 kortini
Halima Mlacha
Daily News; Monday,November 10, 2008 @20:01
Wafanyabiashara watatu jumatatu walifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kujibu tuhuma za kujipatia mabilioni ya fedha kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na hivyo kufanya idadi ya watuhumiwa kufikia 20.
Mbali na wafanyabiashara mbalimbali, watuhumiwa wengine waliopandishwa kizimbani hadi sasa, wamo wafanyakazi wanne wa BoT. Akisoma mashtaka dhidi ya washtakiwa wawili ambao ni Ajay Somani na Jai Somani mbele ya Hakimu Mkazi wa Kisutu Victoria Nongwa, Wakili Mwandamizi wa Serikali Fredrick Nakulilo, alidai watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa matatu.
Alidai katika kosa la kwanza wote wawili walikula njama ya wizi wakiwa na watu wengine ambao hawajafahamika ya kuiibia BoT, na kwamba Septemba 2, 2005, waliiba Sh bilioni 5.9 mali ya benki hiyo.
Pia mnadaiwa kujipatia ingizo la fedha kwenye akaunti zenu, na Septemba 2, 2005 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya mlijipatia kutoka BoT ingizo la fedha shilingi bilioni 5.9 kwa kujifanya Kampuni ya Liquidity Services Ltd imepasiwa deni lenye kiasi hicho kutoka Kampuni ya Society Alsacience De Construction De Mashines Textiles, alidai Nakulilo.
Alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba upande wa mashtaka hauna pingamizi la dhamana iwapo washtakiwa watatimiza masharti yake. Hakimu Nongwa, alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa hao kuwa dhamana ya kosa zima ni fedha taslimu Sh bilioni 2.9, hivyo kila mshitakiwa atatakiwa atoe nusu yake ambayo ni Sh bilioni 1.4 au mali isiyohamishika yenye thamani ya fedha hizo.
Pia alisema pamoja na fedha hizo, washitakiwa hao wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja, ambao ni waajiriwa katika taasisi zinazotambulika na hawatakiwi kutoka nje ya Dar es Salaam na walitakiwa kukabidhi hati za kusafiria. Washtakiwa wote wawili walikana makosa hayo na kurudishwa tena rumande hadi pale watakapotimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena Novemba 25, mwaka huu.
Aidha, mbele ya Hakimu Mkazi Euphemia Mingi, mfanyabiashara Mwesiga Lukaza, alipandishwa kizimbani akiunganishwa na mshtakiwa mwingine Johnson Lukaza, ambaye alishapandishwa kizimbani juzi, kujibu mashtaka ya kujipatia mabilioni ya fedha za EPA.
Akisoma maelezo ya mshtakiwa huyo, Wakili wa Serikali Bwisalo Maganga, alidai mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, kuiba na kujiingizia katika akaunti kiasi cha Sh bilioni 6.3 mali ya BoT. Alidai Septemba 2, 2005 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na lengo la kurubuni alijipatia kiasi hicho cha fedha kwa kudanganya kuwa Kampuni ya Kernel Ltd imehamishiwa deni kutoka Kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan.
Hakimu Mingi alisema dhamana ya kosa hilo ni Sh bilioni 3.1 hivyo mshtakiwa huyo na mwenzake Johnson kila mmoja atatakiwa kutoa fedha taslim Sh bilioni moja na wadhamini wawili wa kuaminika. Mshtakiwa huyo alikana makosa yote na alirudishwa rumande hadi pale atakapokamilisha masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena Novemba 18, mwaka huu.
Watuhumiwa ambao tayari wamefikishwa mahakamani ni Farijala Hussein, Rajab Maranda, Japhet Lema, Bahati Mahenge, Davis Kamungu, Godfrey Mosha, Manase Mwakale na Eddah Mwakale, Devendra Vinodbhai Patel, Amit Nandy, Ketan Chohan, Jayantkumar Chandubahi Patel na Johnson Lukaza.
Wengine ni wafanyakazi wa BoT ambao ni Mkuu wa Idara ya Madeni ya Biashara, Iman David Mwakyosa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni, Ester Mary Komu na makaimu Katibu wa benki wawili ambao ni Bosco Ndimbo Kimela na Sofia Joseph Lakila.
Kati ya watuhumiwa hao, ni wawili tu ambao wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana hiyo ambao ni Godfrey Mosha na Davis Kamungu. Washitakiwa wengine licha ya dhamana zao kuwa wazi, wanaendelea kusota rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti.
Kati ya watuhumiwa hao, ni wawili tu ambao wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana hiyo ambao ni Godfrey Mosha na Davis Kamungu. Washitakiwa wengine licha ya dhamana zao kuwa wazi, wanaendelea kusota rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti.
Jamani tusilale..lalelale.... nahisi kama hile ari ya kufuatilia hii kashfa inapungua kadiri watuhumiwa wanavyozidi kufikishwa mahakamani! Naona mijadara inaanza kuwa ni myepesi! Bado makampuni 12 (thenashara), na kwahiyo ninashauri ule MOTO tulionzanao kujadili hili suala usizimike....
Kwa maana tukiridhika na ufikishwaji wa watuhumiwa mahakamani itakuwa ni sawa sawa na kumbembeleza mtoto aache kulia kwa kumpa pipi! Inawezekana kulia kwake si pipi bali ana minyoo!
No wonder this njake guy has littered the ms - ars highway with gas stations..... Lile ghorofa kule njiro halitakalika vizuri sasa.
hotels and camp sites, tours, kiwanda cha maji ya kunywa, you name all. Ati ameokoka anasali kwenye makanisa ya kiroho!!!!!
Habari ndo hiyo!!! Tusubiri.