EPA na mambo yake

EPA na mambo yake

Samahani Ndg;

Umesikia wapi hii kauli?
MKUU UMETUTOKA??????
 
Hivyo vijifisadi vilivyokamatwa vinashikilia uchumi gani. Watu wanaoshikilia uchumi wa hapa ni wafadhili na wakichoshwa na usanii wetu wakakataa kutupa pesa zao ndio kweli nchi itayumba na kwenda mrama. Hayo maneno ni ya kisanii watanzania si mambwege tena. Hao mafisadi wengi wanavijibiashara vya binafsi na wala biashara zao zilikuwa hazina faida ndio sababu wakawa wezi na wengi vijihela vyao vimefichwa dubhai au nchi za kihuni .na wameshanunua vijiapatmenti kwenye vinchi kama maurisius, dhubai,malta,Sausi etc. Uchumi gani utayum ba??????? labda wa mafisadi.
 
Mbona tumesema kila siku kuwa hapa tunachezewa mchezo wa karunguyeye na mazingaombwe ya mauza uza. Hosea hana tena udhu na kwa hiyo hawezi kushiriki vita ya kupambana na ufisadi. Alitakiwa ajiuzulu kuhusiana na suala la Richmond (sina shaka kabisa hapa aliopokea uchache wa nguvu) na pia keshatajwa kwenye kashifa nyingine kibao. Hiyo tu ilitosha kumwondolea hadhi ya kutoa kauli yoyote kuhusu mafisadi. Sasa anazidi kutia chumvi kwenye kidonda kwa kuzidisha kauli za kutuzuga na kutuamshia ghadhabu tena. Nadhani sasa wahusika wametumiwa ujumbe (messege sent) kuwa yeye (Hosea) hawezekani na hawawezi kufanya kitu.

Tuanze kuwasuta wabunge wetu watueleze kama lile azimio la bunge limeshafutwa au la. Baada ya hapo tunaweza kuanza kutafuta mbinu za kuhakikisha anaachia ofisi ya umma badala ya kuendeleza upuuzi wake huku akitumia kodi zetu!
 
Unajua huyo jamaa wa TAKUKURU hamjamuelewa yeye ameuambia umma wa Watanzania na ulimwengu kwa ujumla kuwa, kazi yake aliyopewa na muungwana imemshinda. Na hivyo atafutwe mwingine kwani naye pia ni sehemu ya ufisadi au jamani hamjamuelewa Hosea?
 
Mkuu kilbark,

Dr. Hoseah siyo kwamba kazi haiwezi,Tatizo la nchi hii linaongozwa kisiasa na hauwezi kuanza kukurupuka kuwashtaki watu bila ya kumuuliza Mkulu wa nchi.

Ngoja nikupe mfano wa suala la EPA,Baada ya Kugundulika Pesa za EPA zimeliwa mkulu aliogopa moja kwa moja kuwachulia hatua wale wezi wakaweka siasa na kujaribu kuhadaa wataznaia kwamba hao ni watu wazito na utakumbuka hata mzee mkaramba alishwahi kulizungumza hili bungeni.

Mathalani DPP kapewa Zigo zito sana ambalo lilimsihindwa muungwana na DPP alikuwa na moja kuchagua kufuata anachokiamini au kuacha waje wahukumiwe na Rais na yeye alichagua njia iliyo bora na Sahihi.

Nakumbuka kipindi chetu enzi za Mwalimu ilikuwa siyo RAhisi watu wa namna hii kupona,ulikuwa ukighundulika tu unawekwa ndani na mammbo mengine yanafuatwa.

Kwa upande mwingie watu wa EPA ni wazito sababu wanamilipi pesa nyingi katika Uchumi na kuwagusa inabidi uende kwa njia sahihi na kwa uangalifu Mkubwa sana,ila naamna DPP na kwa misimamo yake basi atawafikisha mahakamani mara moja.Nakumbuka niliwahi kuzungumza naye punde kabla ya kuteuliwa na rais kuwa DPP alinieleza msiamo wake kwamba wasomi kama sisi tunahitaji kuleta madailiko ya utendaji katika serikali yetu na alinishauri hata mimi nikipata nafasi ya utezi nisifanye kazi kwa uoga.

Nina Imani na DPP na hata Dr. Hoseah,Uzoefu wake katika idara ya Usalama wa taifa itasaidia sana kufanya maamuzi ambayo hayatathiri mwenendo wa serikali na nchi yetu kiujumla.

Tuwe Wavumilivu
 
-TUKIWASHITAKI WOTE UCHUMI WA NCHI UTAYUMBA
Wanandugu maneno haya yamentisha si kidogo bali ni kwa hali ya tahadhar kwa kusikia maneno kama haya toka kwa mtu mkubwa kama huyu
kwamba mafisadi wameshika nchi hii so ni vigumu kuwafkisha wote !!!
JF NAOMBA TUSHAURIANE KWA HILI!!!!
kwangu mimi nahisi uchumi umeshayumba kama yeye binafsi hosea mshitakiwa na mshiriki halisi wa EPA ,bado ndie kinara namba moja kuchunguza fisadi wenzake!!!
pili ....tuwaachie wenyewe

Huyu Hosea naye nadhani ni Fisadi tu. Anataka kutuaminisha kuwa Uchumi wetu umeshikwa na Mafisadi, na kuna ukweli lakini nani ameruhusu hili? Kama uchumi wetu umeshikwa na maisadi ni afadhali tu washitakiwe wote na uporomoke ili tuanze upya maana serikali yetu pia imeshikwa na mafisadi na kwa hiyo haiwezi kuwa huru. Ijikombe, wakati ni sasa!
 
Prof. Ndulu was working for the world Bank when the EPA scandal happened. He was called back home from Washington to work as Deputy governer and later he was appointed as governor. I do not know why Dr. Slaa does not bother to equip himself with facts before making such accusations.
 
Date::11/12/2008
Hosea: Tukiwashtaki watuhumiwa wote wa ufisadi, nchi itayumba

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akizungumza jambo na waandishi wa habari ....
Exuper Kachenje

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, amesema kuwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi kwa pamoja kunaweza kusababisha nchi kuyumba.

Hoseah alisema hayo katika siku ambayo hakukuwa na mtuhumiwa yeyote katika sakata la wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) aliyefikishwa mahakamani baada ya wafanyabiashara 20 kupandishwa mfululizo kizimbani kuanzia Jumatano iliyopita hadi juzi.

Akitoa mada kwenye semina iliyohusisha vyuo vikuu tisa nchini iliyofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini, mkurugenzi huyo wa Takukuru alisema: "Tukiwapeleka wote mara moja mahakamani, nchi inaweza 'ikaparalyse' (ikapooza) ni lazima kuwe na 'stability' (kutoyumba), tufanye kwa kuwa ni sahihi," alisema Hoseah.

Akitoa mada katika semina hiyo iliyowahusisha wajumbe wa kamati za maadili kutoka vyuo hivyo, Hoseah alieleza kuwa, mapambano dhidi ya rushwa kubwa yanapaswa kufanyika kukiwa na utashi wenye nguvu wa kisiasa, mikakati sahihi ya kiuchumi pamoja na kuzuia rushwa.

Alisema kuwa watuhumiwa wa rushwa kubwa wana nguvu kutokana na fedha nyingi wanazomiliki, kiasi cha kuweza kuhatarisha usalama wa watu wengine kwa kutumia vibaya fedha zao.

Dk Hoseah ni kigogo wa tatu kuzungumzia uwezo wa mafisadi na hatari ya kuwashughulikia bila ya umakini baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kulieleza bunge kuwa, kushughulikia watu wenye uwezo wa kifedha ni kazi ngumu, kama ilivyoelezwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Ali Hassan Mwinyi kuwa mafisadi ni hatari.

Watuhumiwa katika kashfa hiyo ya EPA wanadaiwa kuchota fedha hizo katika kipindi cha mwaka 2005/06 wakisingizia kupewa au kulipa madeni na makampuni ya nje yaliyokuwa yakiidai serikali. Watuhumiwa hao wanadaiwa kuchota Sh133 bilioni.

Pamoja na kilio cha wananchi kuwa wote waliochota fedha hizo wapandishwe kizimbani, Rais Jakaya Kikwete alitoa maagizo kuwa wale ambao wangeshindwa kurejesha fedha walizochota kabla ya Oktoba 31, ndio waliotakiwa kufikishwa mahakamani.

Na watuhumiwa hao 20 waliofikishwa mahakamani hadi sasa wamekuwa wakipandishwa kizimbani kwa nyakati tofauti na wengi wameshtakiwa kwa makosa tofauti, wakipandishwa mmoja mmoja na wakati mwingine kuunganishwa na wenzao na kwa mahakimu tofauti.

Akitoa mada yake jana, Dk Hosea alisema Takukuru peke yake haiwezi kumaliza tatizo la rushwa nchini bila kuwepo ushirikiano kutoka kwa taasisi za elimu, mashirika mbalimbali na wananchi.

Aliongeza kuwa, mapambano dhidi ya rushwa, kubwa na ndogo yanapaswa kuwashirikisha wananchi wote, huku akielezea Watanzania kuwa ni waoga kutokana na kukosa ufahamu wa masuala mbalimbali yanayowahusu.

Hoseah alisema kuwa katika mapambano ya rushwa ni vema kuzuia rushwa na kwamba uadilifu ndiyo njia bora ya kulitokomeza tatizo hilo.

Alisema moja ya kasoro za Tanzania ni kuwa na taasisi nyingi dhaifu, zisizo na uwezo zinazofanya kazi zake bila ya uwazi, hali aliyoielezea kuwa inakaribisha rushwa.

"Moja ya kasoro za Tanzania ni kuwa na taasisi dhaifu, zisizo na uwazi... lazima tufanye kazi kuzipa nguvu kwa kurejesha maadili," alisema Hoseah.

Aliongeza kuwa, ndani ya serikali pia uadilifu upo chini na kueleza kuwa kuwa kutokana na hali hiyo ni vema wananchi wakaacha kulalamika badala yake kutafuta ufumbuzi wa tatizo kwa kushiriki kurejesha maadili na kupambana na rushwa.

Alisema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakilalamikia tatizo la rushwa huku wakishinikiza Takukuru ichukue hatua bila wao kushiriki katika mapambano hayo ambayo alisema kuwa ni ya kila mmoja.

Mkurugenzi huyo wa Takukuru alisema kuwa katika kutilia maanani umuhimu wa kuongeza jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa nchini, wameanzisha mkakati maalumu wenye lengo la kurejesha uadilifu nchini.

"Tunataka kurejesha maadili, lengo ni kuzuia rushwa, jukumu letu ni kuwawezesha watu wafahamu na kushiriki katika mapambano hayo," alisema.

Kwenye Mahakama ya Kisutu, hali jana ilikuwa shwari baada ya siku nne za purukushani za kupandisha kizimbani watuhumiwa hao 20, ambao kati yao ni wawili tu waliopata dhamana kutokana na mahakama kuweka masharti magumu, anaripoti James Magai na Paulina Richard.

Hadi majira ya alasiri jana, hakuna mtuhumiwa hata mmoja mpya kwenye kesi hiyo ambaye alikuwa amefikishwa mahakamani hapo.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Charles Kenyela, aliwaambia waandishi wa habari kuwa hadi mchana huo hakuwa na taarifa za kuwepo kwa watuhumiwa wengine ambao wangepandishwa kizimbani.

Mpaka sasa ni wamiliki wa kampuni 10 tu kati ya 22 zinazodaiwa kuchota fedha hizo ambao walikuwa wameshafikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akiwemo mfanyabiashara maarufu mwenye asili ya Kiasia, Jayatkumar Chantubhai Patel, ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Jeetu Patel.

Tofauti na siku nyingine jana hali ilionekana kuwa tulivu mahakamani hapo huku kukiwa na pilikapilika chache za baadhi ya ndugu wa watuhumiwa katika kashfa hiyo ya EPA ambao walikuwa wakishughulikia dhamana za watuhumiwa hao.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Elieza Feleshi, hakutaka kuwaambia waandishi kama kuna watuhumiwa zaidi ambao wangefikishwa mahakamani jana na badala yake alisema aulizwe msemaji wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Hata hivyo, msemaji huyo, Omega Ngole alijibu kwa ufupi kuwa hawawezi kusema ni lini watuhumiwa wanapelekwa mahakamani na badala yake taratibu zinapokamilika na DPP kujiridhisha, wahusika hufikishwa mahakamani.

"Hivyo ninachoweza kukuambia ni kwamba, tumwache DPP afanye kazi, kama kuna watu wa kuwapeleka mahakamani akishajiridhisha atawapeleka," alisema Ngoe.

Wamiliki wa makampuni waliofikishwa mahakamani mpaka sasa ni Johnson na Mwesiga wanaomiliki kampuni ya Kernel, Ketan Chohan, Jeetu Patel na Amit Nandy (Bina Resort na Itoh), Bahati Mahenge, Manase Mwakale, Davis Kamungu, Godfrey Mosha na Edah Nkoma Mwakale (Changanyike Residential Compelex Ltd)

Wengine ni Rajabu Farijala, Japhet Lema na Rajabu Malanda (Mibale Farm), Rajabu Farijala na Rajabu Malanda (Money Planner), Japhet Lema (Njake Enterprises) na Ajay Somani na Jay Somani (Liquidity Services).

Wengine ni Jeetu Patel na ndugu zake wanaomiliki kampuni za Bencon International Ltd, Maltan Mining Ltd na Navy Cut Tobacco (T) Ltd.

Source: Mwananch
 
“Hivyo ninachoweza kukuambia ni kwamba, tumwache DPP afanye kazi, kama kuna watu wa kuwapeleka mahakamani akishajiridhisha atawapeleka,” alisema Ngoe.

Source: Mwananchi
 
Thats the way Alasiri operates

Kabisaaa.. na wanajua soko lao liko wapi...wanakuja na vichwa vya habari vye lugha za mtaani ili kuwakamata watu kiulaini lakini wenye akili zao wanajua hakuna habari nzito hapo

au kwa vile linatokaga mchana watu wameshachoka?
 
Soo la EPA: Gavana Ndullu atajwa!

2008-11-11 17:19:44
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Wakati watuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA, wanazidi kuongezeka, sakata hilo limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa madai mapya yanayomhusisha gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu.

Katika madai hayo, inaelezwa kuwa Profesa Ndullu aliyenyaka nafasi hiyo baada ya gavana aliyekuwepo, Dk. Daud Balali ambaye sasa ni marehemu kutimuliwa kazi, hakustahili kushikilia nafasi hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa Balali aliyeboronga hadi mapesa hayo yakabebwa kiulaini.

Aliyeibua madai hayo ni Mbunge wa jimbo la Karatu, Dk. Wilbroad Slaa.

``Binafsi nilishangaa kuona Prof. Ndullu akipandishwa cheo na kuwa gavana mpya... ikumbukwe kuwa mapendekezo ya kampuni iliyokagua na kubaini wizi huo wa pesa za EPA
( Ernst & Young), yalitaka safu nzima ya uongozi wa BoT ibadilishwe,`` akadai Dk. Slaa.

Akadai kuwa kwa vile Prof. Ndullu alikuwa miongoni mwa safu hiyo, hakupaswa kupewa ugavana.

Sambamba na hilo, Dk. Slaa amedai kuwa bado hajaridhishwa na watu walioburuzwa mahakamani kwa kile alichodai kuwa, anaamini wapo vigogo wanaostahili kuunganishwa na watuhumiwa hao katika kesi zinazowakabili.

Akadai kuwa kwa anavyoamini yeye, wafanyakazi wa BoT walioshitakiwa katika kesi hiyo hadi sasa, ni baadhi tu ya watuhumiwa wa sakata hilo, kwani vigogo wa kweli walioidhisha fedha hizo hadi zikaweza kuchotwa kwa kiwango kilichotajwa bado hawajaguswa.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amesema licha ya baadhi ya watumishi wa BoT kuburuzwa kortini, bado Serikali inapaswa kutoa maelezo ya kina juu ya sababu za kutomhoji gavana wa awali, Dk. Daudi Balali kuhusiana na wizi huo wa EPA.

``Nadhani maelezo ya Ballali yalihitajika sana…yeye ndiye alikuwa na ufunguo wa mambo yote, hivyo Serikali iueleze umma ni kwa nini haikumhoji,`` akasisitiza Dk. Slaa.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, ametaka watu waliorudisha fedha za EPA nao wafikishwe mahakamani.

Akasema taaluma ya sheria aliyofundishwa na ile anayoendelea kuwafundisha wasomi wa Watanzania na pia katiba ya nchi, inaeleza kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.

Akasema kwa mtaji huo, haoni sababu ya kuwaacha watuhumiwa waliorejesha fedha za EPA bila kuwaburuza kortini.

``Kutowafikisha mahakamani wale waliorudisha fedha ni ubaguzi wa wazi mbele ya sheria. Kwa vile mimi ni mwalimu wa sheria, sivumilii kuona hali hiyo,`` akasema Dk. Mvungi.

Hadi kufikia jana, watuhumiwa 20 wa kesi ya EPA walikuwa tayari wameshaburuzwa kortini na kusomewa mashtaka ya kuhusika na wizi wa pesa hizo za EPA kabla ya kutupwa rumande, huku wawili pekee wakipata dhamana ambao ni Davies Kamungu na Godfrey Mosha.

Miongoni mwa walioburuzwa kortini ni maafisa wanne wa Benki Kuu (BoT) ambao ni Mkuu wa Idara ya Madeni, Imani Mwakosya, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni , Esther Komu, Kaimu Mwanasheria, Bosco Kimela na Mwanasheria wa Benki hiyo, Sofia Joseph.

Wengine ambao wameshaburuzwa kortini na kutupwa rumande ni Jayantkumar Chandubhai Patel a.k.a Jeetu Patel, Devendra K. Vinodbhai Patel, Amit Nandy, Kehan Chohan na Johnson Lukaza, Eddah Mwakale, Manase Mwakale na Bahati Mahenge.

Waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni Mwesiga Lukaza, Jai Chohotalal Somani na Ajay Suryakant Somani.

SOURCE: Alasiri

Mheshimiwa Dr. Slaa,

Labda ututengenezee timeline ya suala la EPA vinginevyo naona kumhusisha prof. Ndullu
ni makosa kwasababu timeline inakataa.

Nijuavyo mimi prof. Ndullu alichaguliwa kuwa naibu Gavana baada au siku chache kabla ya Dr. Ballali kukimbilia USA. Kama ninavyojua mimi ni sahihi, basi, yeye hakuwepo BOT wakati hizo pesa zinachotwa.

Anayejua tarehe kamili ambayo prof. Ndulu aliteuliwa kuwa naibu gavana naomba atufahamishe.
 
Mbali na kwamba kauli za viongozi wetu wengi wa serikali CCM hazina kichwa wala miguu hapa Hosea amesema ukweli ambao kila mtu anaujua kwani ni wazi kua Mafisadi(WEZI) Namba moja ni vigogo au waliokua vigogo wa serikali na CCM chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya tatu Mkapa na awamu ya Nne Kikwete.Hao wanaofikishwa mahakamani ni watu waliotumiwa kupitishia fedha hizo.Kweli kama vigogo hao wa serikali na CCM pamoja na Rais wakifikishwa mahakamani nchi itayumba bora nchi iyumbe kwa hao watu kufikishwa mahakamani na liwe funzo kwa wengine kuliko kuendelea na maigizo na mazingaobwe.Kwa upande mwingine kauli ya Hosea kama mtaalamu inatia mashaka kwanza baada ya kutangaza nguvu za mafisadi na kuonesha woga wako utaweza kupambana nao vipi?Hii naifananisha na mkuu wa majeshi kumtangazia adui wake silaha gani alizonazo,askari wangapi na mbinu atakazozitumia katika vita dhidi ya adui wake!Pili ni vigezo vipi vilivyotumiwa kuchagua kundi lipi lifikishwe mwanzo mahakamani?TUMECHOKA NA MAZINGAOMBWE MUNGU IBARIKI TANZANIA.Advocate Jasha
 
Kiongozi mkuu wa PCCB anapoongea maneno kama hayo kweli inasikitisha sana.

Yaani leo hii tunaogopa kuwashughulikia majambazi kwasababu tu wana pesa?
 
MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, amesema kuwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi kwa pamoja kunaweza kusababisha nchi kuyumba.

Hoseah alisema hayo katika siku ambayo hakukuwa na mtuhumiwa yeyote katika sakata la wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) aliyefikishwa mahakamani baada ya wafanyabiashara 20 kupandishwa mfululizo kizimbani kuanzia Jumatano iliyopita hadi juzi.

Akitoa mada kwenye semina iliyohusisha vyuo vikuu tisa nchini iliyofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini, mkurugenzi huyo wa Takukuru alisema: "Tukiwapeleka wote mara moja mahakamani, nchi inaweza 'ikaparalyse' (ikapooza) ni lazima kuwe na 'stability' (kutoyumba), tufanye kwa kuwa ni sahihi," alisema Hoseah.

Akitoa mada katika semina hiyo iliyowahusisha wajumbe wa kamati za maadili kutoka vyuo hivyo, Hoseah alieleza kuwa, mapambano dhidi ya rushwa kubwa yanapaswa kufanyika kukiwa na utashi wenye nguvu wa kisiasa, mikakati sahihi ya kiuchumi pamoja na kuzuia rushwa.

Alisema kuwa watuhumiwa wa rushwa kubwa wana nguvu kutokana na fedha nyingi wanazomiliki, kiasi cha kuweza kuhatarisha usalama wa watu wengine kwa kutumia vibaya fedha zao.

Dk Hoseah ni kigogo wa tatu kuzungumzia uwezo wa mafisadi na hatari ya kuwashughulikia bila ya umakini baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kulieleza bunge kuwa, kushughulikia watu wenye uwezo wa kifedha ni kazi ngumu, kama ilivyoelezwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Ali Hassan Mwinyi kuwa mafisadi ni hatari.

Watuhumiwa katika kashfa hiyo ya EPA wanadaiwa kuchota fedha hizo katika kipindi cha mwaka 2005/06 wakisingizia kupewa au kulipa madeni na makampuni ya nje yaliyokuwa yakiidai serikali. Watuhumiwa hao wanadaiwa kuchota Sh133 bilioni.

Pamoja na kilio cha wananchi kuwa wote waliochota fedha hizo wapandishwe kizimbani, Rais Jakaya Kikwete alitoa maagizo kuwa wale ambao wangeshindwa kurejesha fedha walizochota kabla ya Oktoba 31, ndio waliotakiwa kufikishwa mahakamani.

Na watuhumiwa hao 20 waliofikishwa mahakamani hadi sasa wamekuwa wakipandishwa kizimbani kwa nyakati tofauti na wengi wameshtakiwa kwa makosa tofauti, wakipandishwa mmoja mmoja na wakati mwingine kuunganishwa na wenzao na kwa mahakimu tofauti.

Akitoa mada yake jana, Dk Hosea alisema Takukuru peke yake haiwezi kumaliza tatizo la rushwa nchini bila kuwepo ushirikiano kutoka kwa taasisi za elimu, mashirika mbalimbali na wananchi.

Aliongeza kuwa, mapambano dhidi ya rushwa, kubwa na ndogo yanapaswa kuwashirikisha wananchi wote, huku akielezea Watanzania kuwa ni waoga kutokana na kukosa ufahamu wa masuala mbalimbali yanayowahusu.

Hoseah alisema kuwa katika mapambano ya rushwa ni vema kuzuia rushwa na kwamba uadilifu ndiyo njia bora ya kulitokomeza tatizo hilo.

Alisema moja ya kasoro za Tanzania ni kuwa na taasisi nyingi dhaifu, zisizo na uwezo zinazofanya kazi zake bila ya uwazi, hali aliyoielezea kuwa inakaribisha rushwa.

"Moja ya kasoro za Tanzania ni kuwa na taasisi dhaifu, zisizo na uwazi... lazima tufanye kazi kuzipa nguvu kwa kurejesha maadili," alisema Hoseah.

Aliongeza kuwa, ndani ya serikali pia uadilifu upo chini na kueleza kuwa kuwa kutokana na hali hiyo ni vema wananchi wakaacha kulalamika badala yake kutafuta ufumbuzi wa tatizo kwa kushiriki kurejesha maadili na kupambana na rushwa.

Alisema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakilalamikia tatizo la rushwa huku wakishinikiza Takukuru ichukue hatua bila wao kushiriki katika mapambano hayo ambayo alisema kuwa ni ya kila mmoja.

Mkurugenzi huyo wa Takukuru alisema kuwa katika kutilia maanani umuhimu wa kuongeza jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa nchini, wameanzisha mkakati maalumu wenye lengo la kurejesha uadilifu nchini.

"Tunataka kurejesha maadili, lengo ni kuzuia rushwa, jukumu letu ni kuwawezesha watu wafahamu na kushiriki katika mapambano hayo," alisema.

Kwenye Mahakama ya Kisutu, hali jana ilikuwa shwari baada ya siku nne za purukushani za kupandisha kizimbani watuhumiwa hao 20, ambao kati yao ni wawili tu waliopata dhamana kutokana na mahakama kuweka masharti magumu, anaripoti James Magai na Paulina Richard.

Hadi majira ya alasiri jana, hakuna mtuhumiwa hata mmoja mpya kwenye kesi hiyo ambaye alikuwa amefikishwa mahakamani hapo.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Charles Kenyela, aliwaambia waandishi wa habari kuwa hadi mchana huo hakuwa na taarifa za kuwepo kwa watuhumiwa wengine ambao wangepandishwa kizimbani.

Mpaka sasa ni wamiliki wa kampuni 10 tu kati ya 22 zinazodaiwa kuchota fedha hizo ambao walikuwa wameshafikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akiwemo mfanyabiashara maarufu mwenye asili ya Kiasia, Jayatkumar Chantubhai Patel, ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Jeetu Patel.

Tofauti na siku nyingine jana hali ilionekana kuwa tulivu mahakamani hapo huku kukiwa na pilikapilika chache za baadhi ya ndugu wa watuhumiwa katika kashfa hiyo ya EPA ambao walikuwa wakishughulikia dhamana za watuhumiwa hao.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Elieza Feleshi, hakutaka kuwaambia waandishi kama kuna watuhumiwa zaidi ambao wangefikishwa mahakamani jana na badala yake alisema aulizwe msemaji wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Hata hivyo, msemaji huyo, Omega Ngole alijibu kwa ufupi kuwa hawawezi kusema ni lini watuhumiwa wanapelekwa mahakamani na badala yake taratibu zinapokamilika na DPP kujiridhisha, wahusika hufikishwa mahakamani.

“Hivyo ninachoweza kukuambia ni kwamba, tumwache DPP afanye kazi, kama kuna watu wa kuwapeleka mahakamani akishajiridhisha atawapeleka,” alisema Ngoe.

Wamiliki wa makampuni waliofikishwa mahakamani mpaka sasa ni Johnson na Mwesiga wanaomiliki kampuni ya Kernel, Ketan Chohan, Jeetu Patel na Amit Nandy (Bina Resort na Itoh), Bahati Mahenge, Manase Mwakale, Davis Kamungu, Godfrey Mosha na Edah Nkoma Mwakale (Changanyike Residential Compelex Ltd)

Wengine ni Rajabu Farijala, Japhet Lema na Rajabu Malanda (Mibale Farm), Rajabu Farijala na Rajabu Malanda (Money Planner), Japhet Lema (Njake Enterprises) na Ajay Somani na Jay Somani (Liquidity Services).

Wengine ni Jeetu Patel na ndugu zake wanaomiliki kampuni za Bencon International Ltd, Maltan Mining Ltd na Navy Cut Tobacco (T) Ltd.

Duh,hawa mafisadi wanatisha !!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jamani wakati umefika wa kuacha uonevu na kupendelea watu, Hivi hawa waliopewa jukumu la kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wausika wote wa wizi wa fedha za Benki Kuu (BOT) watawakamata lini wausika wakuu? mbona vigogo wengi tu tunawajua wanausika na wizi huo lakini bado awajakamatwa au mbaka na wao wafe kama mwenzao.
 
Kiongozi mkuu wa PCCB anapoongea maneno kama hayo kweli inasikitisha sana.

Yaani leo hii tunaogopa kuwashughulikia majambazi kwasababu tu wana pesa?

Thats too low according to his rank
Mbona mwalimu alianzisha na kuliesimamia Azimia La Arusha na watu wengi sana walitaifishiwa mali zao na nchi ikaenda
Bora tukubalian hawa guardian to Tanzanian future are bunch of cowards
 
Back
Top Bottom