Ephata Nanyaro: Kuhusu future ya CHADEMA na hoja za wanaohama chama kuitafuta ‘future’

Ephata Nanyaro: Kuhusu future ya CHADEMA na hoja za wanaohama chama kuitafuta ‘future’

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Kuhusu future ya CHADEMA

Kuna watu waoga wanaosema hawaoni future wakiwa CHADEMA hivo wamehamia ccm!
Naomba nitumie fursa hii kueleza yafuatayo.Binafsi nimekuwa CHADEMA tangu enzi zie ambazo mikutano ilikuwa inafanyikia stend au sokoni kwa kuwa Stend au sokoni huwa kuna watu tu na lazima watasikiza.Nikachaguliwa kuwa diwani 2010 wakati Arusha ilikuwa na kata 19 CHADEMA tukashinda kata 9 TLP 1 na ccm 10,Jimbo likawa chini ya CHADEMA hivo kufanya idadi kuwa sawa nje ya wabunge wa viti maalum na madiwani wa viti maalum

CCM walitumia dola kuchakachua uchaguzi wa Meya,hali iliyofanya tuanze harakati za viwango vipya kumpinga Meya wa kichina,kwa miaka mine hatukushiriki vikao vya Halmashauri wala kuchukua posho jambo lililofanya Makao Makuu kutulipa fedha kufidia zile ambazo hatukuingia vikaoni.Baadhi yetu tulisimama Imara hadi mwisho licha ya changamoto mbalimbali hatukuyumba.2015 tulipata madiwani 24 kati ya kata 25 yaani ccm walikuwa na diwani mmoja tu aliyechaguliwa na wanachi.Kuna kata ambazo kura za ccm zilikuwa za aibu kuu,mfano Levolosi mgombea wa ccm alipata kura 122 wakati mimi nilipata kura 3998

Kuna watu wamechaguliwa mwaka 2015 baada ya kazi kubwa ambayo tuliifanya,kwa gharama ya jasho na damu zetu,
Moja ya ahadi wanayopewa ni kuwa watachaguliwa tena kuwa madiwani yaani kwao udiwani ni swala la Kufa na kupona (a metter of grieve concern) hawa wamekuwa brainwashed na kwao madaraka ni kila kitu wamehamia ccm ili warejeshwe kwenye udiwani,hawajui kuwa tangu zamani za Pontio Plato hatukuwahi kushinda kwa hisani/ruhusa ya ccm,tulishinda kwa kutumia Peoples Power.Kama 2010 na 2015 tulitumia peoples power kushinda tutashinda tena 2020 kwa kutumia nguvu ya umma

Habari njema ni kuwa hawa wahamiaji kutoka Upienzani kwenda ccm ni Wahamiaji haramu ambao wanaenda kumalizia uhai mdogo wa ccm uliobaki,hawaendi ccm kwa mapenzi bali kwa hasira,hofu,mashaka,wasiwasi na uchu wa madaraka,hawajui itikadi na kwao sio swala la maana bali madaraka

Ikiwa ishara ya kipimo cha uimara au kukubalika ccm ni idadi ya wahamiaji basic cm ni mahututi kuliko vile tulifikiri mwanzo.Kwamba chama ambacho kiko madarakani tangu 1978 leo kimeishiwa wanachama wenye sifa za udiwani au ubunge au uwakilishi hadi waporwe wapinzani,ni kielelezo cha kuwa kimekufa!

Kielelezo cha nguvu yetu ni kiwango cha nguvu kubwa inayotumiwa na dola dhidi yetu,kama tungekuwa hatuna future basi dola ingeacha kupambana na chama kisichokuwa na future..kwa kuwa future yetu ni kubwa na maono yetu ni makubwa kuliko wao ni lazima wawe na wasiwasi wa kiwango cha kukimbia hata wasipokimbizwa
Mimi naona future kubwa ndani ya CHADEMA!Naona mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli kwa Taifa letu

Tusiogope
Tusirudi Nyuma
Hisitoria itaandikwa na Washindi
We have God we have the power

Nanyaro EJ
Mwenyekiti Wilaya
 
Umeandika haya kwa sababu siasa za upinzani; intelligent ones are full of doubts while the stupid ones are full of confidence
 
Huyu ndiye anafaa kupambana na Mrisho Gambo kwenye ubunge siyo Lema.

Lema akagombee Hai!
 
Mtamjua vizuri October!
FB_IMG_1580040189342.jpg

Wewe kapuku mtozeni na mama Samia nani ana akili ?
 
CHADEMA mng'oeni kwanza Mbowe uenyekiti mambo mengine yatakwenda sawa .

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Back
Top Bottom