Ephata Nanyaro: Kuhusu future ya CHADEMA na hoja za wanaohama chama kuitafuta ‘future’

Nanyaro nikiona wapinzani mnazungumza kushiriki uchaguzi na kushinda bila kudai tume huru ya uchaguzi, naona kama utani fulani hivi. Yaani cdm sasa hivi inatakiwa kila anayesimama kuongea lazima atamke uhitaji wa tume huru ya uchaguzi. Bila hilo vuguvugu sioni lolote jipya.
 
Binafsi sijaona HOJA inayoleta tumaini na kuonyesha hiyo FUTURE.
Kubwa ulilozungumzia hapo ni;
wanachadema kuhamia CCM.
Sababu za wao kuhamia.
Na kwamba pamoja na kuhama huko hawataiathiri CDM...!!!
Hujaonyesha mwelekeo mpya wa CDM, Malengo na Mikakati matokeo au Tathmini.

Labda nikukumbushe tu athari ya kuhama;
Uanachama ndio mtaji wa chama kwa maana ya ushawishi na kampeni,rasilimali fedha, na hatimae KURA. sote ni mashahidi wanaCCM walipohamia CDM 2015 tuliona kura za urais ubunge udiwani na mameya waliongezeka CDM, bila kusahau RUZUKU.
Hujaeleza CDM wamejipangaje.

SABABU ulizorota ni kwamba hawaendi ccm kwa mapenzi bali kwa "hasira,hofu,mashaka,wasiwasi na uchu wa madaraka,hawajui itikadi"

Unachotuambia ni kwamba wanaohama wanahasira, ya nini, na nani kwa faida ya nani na wako kiasi gani..

Kwamba wanaohama wana HOFU,MASHAKA na WASIWASI; Upi, kwa nini..na nani!?

Kwamba wanaohama wana UCHU WA MADARAKA, inaamana wamekata tamaa kupata madaraka kupitia CDM..!??

Japo hawaamini ktk itikadi ya CCM kikubwa hapa ni kura zao

Kifupi sababu zako ulizotoa zinathibitisha tu kwamba CDM mmepoteza tayari..!!

Kama matokeo ya 2015 yaliwatoa jasho na damu basi 2020 itawagharimu MOYO, MAINI NA MAPAFU.

Acheni kujipa matumaini yasiyokuwemo na badala yake jiulizeni kwa nini watu wanahama na sio kutafuta visingizio
 
msemaji Ukweli njoo usome uzi hali wa Chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…