Ephraim Kibonde Jahazi Show

Ephraim Kibonde Jahazi Show

Wanaelekea pabaya sana na redio yao hiyo,sikuhizi siwapendi kabisa.siku upinzani ikichukua uongozi sijui wataficha wapi sura zao kwa aibu,si wamejionea ya SUGU huko Mbeya mjini,nyuso zimeanza kuwashuka, nawaambia wajirekebishe wasichezee hisia za watu.
 
Kuna tetesi nimesikia kuwa Manji kanunua hisa za kutosha ,na hz ni dalili za mabadiliko ya sera za CLOUDS kuendana na bosi wao kiongozi!
 
namtahadharisha Tambwe kibarua chake kinaweza ota nyasi make huyu KIBONDE n mjinga anapiga jaramba kuwania nafasi hyo.Afu kuonyesha jinsi alivyo mjinga eti n comedian.Babu mzima hovyoo.
 
Kwa bahati mbaya sana na mimi nilisikiliza Clouds jioni, na hii ni kutokana na kulazimishwa na jamaa nililiyekuwa naye kwenye gari na nikaona si mbaya ngoja nimpe anachotaka. Ule upuuzi alioongea Kibonde, kama ningekuwa mimi ndo Joseph Kusaga basi leo jamaa angekuwa anapewa onyo kali na kupelekwa training ya utangazaji na uandishi wa habari.

Jamaa alikuwa anajifanya anatoa uchambuzi wa kisiasa hasa masuala ya bunge huku yeye mwenyewe akikiri kuwa hajui mambo yafuatayo;

1. Bunge la sasa linatarajiwa kuwa na wabunge wangapi
2. Idadi ya viti maalumu vya CCM na vile vya upinzani
3. Taratibu zinazofuatwa katika kuchagua spika
4. Mchakato uliofuatwa na CCM mpaka kufikia kumpitisha Anna Makinda
5. Vigezo vilivyotumika na CCM kumuengua spika Sitta, huku Kibonde akimdhihaki kama ni mtu aliyekuwa mzigo kwa chama chake

Sasa najiuliza kama alikuwa anajua kwamba anakuja kuchambua masuala ya bunge na uchaguzi wa spika, kwa nini hakujiandaa na kuwa na relevant information?

Nilishikwa na butwaa pale ambapo bogus mwingine Gadner G Habash aliposema kwamba Jaji Mkuu wa Tanzania ni mwanamke!! Na aliendelea kusisitiza hivyo mpaka msikilizaji mmoja alipomtumia sms na kumwambia kuwa Jaji mkuu ni mwanaume.

I was totally pissed off!! Nikajiuliza hivi Kibonde anaweza nini? Kuchambua michezi pia hajui, namshauri atafute training zitakazo msaidia kuondoa ujinga alionao.

Labda tatizo linaweza kuwa Kibonde hajui kama hajui!!
 
Kile kituo kimejaza mbuzi manyoya, mawakala wa mafisadi, na genge la waleta mizaha
 
Kibonde as Kibonde hapo Clouds FM anaitoa hiyo media ktk Uburudishaji. Kweli huyo jamaa na G Habashi wake ni vilaza wa kutupa, kilichowaweka pale sijui ni nini.

Personally, I commend the Power Breakfast presentation especially with PJ.
 
Kibonde as Kibonde hapo Clouds FM anaitoa hiyo media ktk Uburudishaji. Kweli huyo jamaa na G Habashi wake ni vilaza wa kutupa, kilichowaweka pale sijui ni nini.

Personally, I commend the Power Breakfast presentation especially with PJ.

huyo gadna arudie kazi ya kuuza duka tu!
 
Hivi nauliza jamani hiyo Clouds FM ni redio ya CCM? Halafu huyu kilaza Kibonde anapata wapi ubavu wa kuongea issues zinazogusa jamii hovyo hovyo namna hii, amenikera sana. Eti obvious Anna Makinda atashinda Uspika na hizo analysis zake mbuzi!! Sijui nimpe adhabu gani huyu?:sad::spider:

Kwani haujui Kibonde ni bwabwa, na ma bwabwa yanaongea ovyo yakiwashwa.
 
lets discuss issues tusiwape umaarufu wasiostahili, tuache kusikiliza kipindi chake tu inatosha
 
Hili ni tatizo la kulelewa huyo gh analelewa na kibonde ni mafisadi wanamleaa,anyway ni njaa tu zinawasumbua mtu mwenye akili timamu hawezi kuongea kwenye media ule upuuzi,naungana na aliyesema kibonde hajua kama hajua
 
we bado una muda wa kumsikiliza huyo...pole sana:tape::tape::tape:

Nashukuru kwa pole yako njema, ila sikumsikiliza kwa hiari yangu, nilipokuwa kwa wakati huo ndio walikuwa wamefungulia Clouds na kwasababu redio haikuwa yangu sikuwa na jinsi zaidi ya kununa!:A S angry: Mbona mwenyewe nilishajipiga marufuku.
 
hIVI HUYO kIBONDE ANAZUNGUMZIA LOLOTE KUHUSU USHINDI WA sUGU?
tHUBUTU!!
 
Hii radio Mwaka 2005 ndio ilisema rais ana sura nzuri. Sasa sijui kwa vigezo vipi!!??
 
Halafu hawa jamaa wa radio, tv na blogs kama Michuzi, Mjengwa hawaangalii upepo, hawajui ndiyo kifo cha ccm kinafika muda sio mrefu, na bado wao wanajifanya kupiga piga mdomo, watakosa pakutokea na upuuzi wao..!
 
Kibonde namfahamu tokea tunasoma naye primary alikuwa monitor mnoko akiandika majina ya wapiga kelele wakati watu wamenyamaza kimya na kuyasubmit wakati watu wanapiga kelele. He's crazy hivyo haniumizi kichwa.
 
kama kweli anasoma ujumbe basi nadhani anatakiwa kujilekebisha ukweli hata mimi nawachukia sana hasa Kibonde anapofanya ushabiki kwenye kitu kinachoitaji umakini.Kunasiku nilikuwa naangalia Clouds TV anakipindi chake nilijaribu kumwangalia sikumwelewa alikuwa anafanya nini.Tukiacha ushabiki nadhani kila kitu kinapendeza kama unapata ushauri kabla ya kukifanya pia angalia watu wanaokupa ushauri maana wanaweza kuwa wanakusifia kwa kuwa wanakujuwa wanaona aibu kukueleza ukweli.Ushauri kwenye kipindi cha TV acha huna unachokifanya,redioni punguza ujuwaji kumbuka wewe nimtoa habari hutakiwi kuonyesha ushabiki wowote kama ninafasi za uongozi utapata maana wanakujuwa.
 
Back
Top Bottom