Kwa bahati mbaya sana na mimi nilisikiliza Clouds jioni, na hii ni kutokana na kulazimishwa na jamaa nililiyekuwa naye kwenye gari na nikaona si mbaya ngoja nimpe anachotaka. Ule upuuzi alioongea Kibonde, kama ningekuwa mimi ndo Joseph Kusaga basi leo jamaa angekuwa anapewa onyo kali na kupelekwa training ya utangazaji na uandishi wa habari.
Jamaa alikuwa anajifanya anatoa uchambuzi wa kisiasa hasa masuala ya bunge huku yeye mwenyewe akikiri kuwa hajui mambo yafuatayo;
1. Bunge la sasa linatarajiwa kuwa na wabunge wangapi
2. Idadi ya viti maalumu vya CCM na vile vya upinzani
3. Taratibu zinazofuatwa katika kuchagua spika
4. Mchakato uliofuatwa na CCM mpaka kufikia kumpitisha Anna Makinda
5. Vigezo vilivyotumika na CCM kumuengua spika Sitta, huku Kibonde akimdhihaki kama ni mtu aliyekuwa mzigo kwa chama chake
Sasa najiuliza kama alikuwa anajua kwamba anakuja kuchambua masuala ya bunge na uchaguzi wa spika, kwa nini hakujiandaa na kuwa na relevant information?
Nilishikwa na butwaa pale ambapo bogus mwingine Gadner G Habash aliposema kwamba Jaji Mkuu wa Tanzania ni mwanamke!! Na aliendelea kusisitiza hivyo mpaka msikilizaji mmoja alipomtumia sms na kumwambia kuwa Jaji mkuu ni mwanaume.
I was totally pissed off!! Nikajiuliza hivi Kibonde anaweza nini? Kuchambua michezi pia hajui, namshauri atafute training zitakazo msaidia kuondoa ujinga alionao.
Labda tatizo linaweza kuwa Kibonde hajui kama hajui!!