Epicurean paradox ni hoja mbovu ya akina kiranga na wenzie

Epicurean paradox ni hoja mbovu ya akina kiranga na wenzie

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
4,031
Reaction score
6,156
Kama Mungu ana nguvu zote na muweza wa yote kwanini Kuna mabaya duniani kwanini asingefanya dunia iwe ya mema tu?

Vipi kama Mungu angefanya iwe ya mema tu watu kama hao wakauliza kwanini yawepo mema tu huyu Mungu muweza wa yote kwanini haruhusu mabaya ?

Au tuseme kama Mungu angendoa mabaya yote je wanaopenda mabaya nao waondolewe la sivyo mabaya yatabaki na kama ndio huoni anawaonea watu kuchagua wapendayo je Mungu ana udikiteta ?

Kwanini kaacha mema na mabaya lakini Kuna watu wanataka mema tu akina kiranga vipi angeacha mema tu na kuondoa mabaya wale watu wanaopenda mabaya wangeemda wapi

Je sio kumfanya Mungu dikteta?

NB. Hapa tunafocus na philosophy sio vitabu vya dini kwa hiyo usijibunkilingana dini jibu kwa style hiyo, tunataka philo itupe majibu
 
Mtoto wangu wa miaka 11, ananiuliza kama Mungu ameumba anga ya mbali yenye sayari zote pamoja na dunia na viumbe vyake....na kama kila kilichokuwepo maana yake kimeumbwa
Je ni nani alimuumba huyo Mungu?
 
Inasikitisha sana
Mfano ila ni kweli wewe unapenda mademu. Alafu kwa masihara kwa Mungu hii ni dhambi manake si jambo jema je akiondoa mabaya haya manake hata chanzo akiondoe vipi kama wewe hupendi mema ya Huyu Mungu si atakua anakuonea? Uongo?
 
Mtoto wangu wa miaka 11, ananiuliza kama Mungu ameumba anga ya mbali yenye sayari zote pamoja na dunia na viumbe vyake....na kama kila kilichokuwepo maana yake kimeumbwa
Je ni nani alimuumba huyo Mungu?
Acha kutoka kwenye swali jibu hii hoja mafelwe anauza ili APATE hela kwa mfano kuua ni kosa au jambo baya je Mungu akiondoa hiyo tabia mafwele atajisikiaje wakati anaipenda. Angekuwa haipendi asingefanya aliyofanya assume mafelwe ni muuzaji na ndio fantasy yake
 
Free IQ TEST
 
Mtoto wangu wa miaka 11, ananiuliza kama Mungu ameumba anga ya mbali yenye sayari zote pamoja na dunia na viumbe vyake....na kama kila kilichokuwepo maana yake kimeumbwa
Je ni nani alimuumba huyo Mungu?
Wanadamu waliozoea kujenga, kutengeneza na kuunda, siyo jambo rahisi kuelewa ukweli kwamba siyo kila kilichopo lazima kiwe na mwanzo - Mungu hana mwanzo wala mwisho!

Hoja kwamba kila kitu lazima kiwe na mwanzo ni sawa na kulazimisha kanuni fulani moja ya hesabu ikokotoe maswali yoyote bila kujali uanuwai wao.
 
Back
Top Bottom