Epidural Anesthesia: njia ya kisasa kujifungua bila maumivu

Epidural Anesthesia: njia ya kisasa kujifungua bila maumivu

kwa hiyo wanaozaa kwa operation hawawapendi watoto wao?
Operation ni muhimu kuokoa maisha yako au mtoto. Ila epidural ni hitaji lisilo la msingi kwa mama wala mtoto
 
Epidural ni gharama kubwa sana?

Wapi huko ambako epidural ni gharama?

Maana sijawahi kusikia ni gharama sana...but then again circles zangu ni tofauti na za wengi humu....so maybe, just maybe.....

Nimeskia mikocheni hospital ni 5M. Hii hela kwa mtanzania wa chini kama mimi ni kubwa sana.
 
Kuna mambo hayaelewi kisawasawa kuhusu epidural analgesia
1: Epidural analgesia haiondoi maumivu yote ya kujifungua ila inayapunguza tu. Huwezi kujifungua huku unaangalia TV au unasoma gazeti kama ilaivyo elezwa hapo juu.
2: Indication ya epidural anagesia sio kwa ajili ya kupunguza maumivu tu, ila pia hutumika kusaidia kulainisha na kufungua njia ya uzazi iwapo progress ya labour iko slow.

Kila kitu katika medicine kina indications, contraindication, benefits and side effects. Epidural analgesia ikiwa indicated properly ni njia nzuri ya kumuwezasha mama kujifunga kwa usalama.

Swala la gharama sio major concern kwenye epidural analgesia. The major concern is presence of a skilled anaesthetist. Dawa zinayotumika ni dawa za kawaida za ganzi. catheter zake pia ni za kawaida. Cha msingi ni kupata mtu anayeweza kuapply correctly.
 
Nimeskia mikocheni hospital ni 5M. Hii hela kwa mtanzania wa chini kama mimi ni kubwa sana.

Hakuna sababu ya epidural analgesia kuwa sh. mil 5. Kuna uwezekano mkubwa kuwa hii taarifa sio sahihi. jaribu kutafuta taarifa sahihi.
 
Hakuna sababu ya epidural analgesia kuwa sh. mil 5. Kuna uwezekano mkubwa kuwa hii taarifa sio sahihi. jaribu kutafuta taarifa sahihi.

Unajua sielewi kabisa kwa nini hiyo procedure iwe ghali hivyo, kama yanayosemwa ni kweli.

Manake huko kwingine hata wasio na private insurance hupewa hiyo option ya epidural.
 
Unajua sielewi kabisa kwa nini hiyo procedure iwe ghali hivyo, kama yanayosemwa ni kweli.

Manake huko kwingine hata wasio na private insurance hupewa hiyo option ya epidural.

nadhani kwa sababu bongo haijazoeleka ndo maana inaonekana a big deal
 
Hata kama haijazoeleka haiwezi kuwa mil 5.

Dawa inayotumika kwenye epidural ni the same na dawa inayotumika kumchoma ganzi mtu anyeng´oa jino. Kwahiyo kinachooingezeka kwenye epidural ni ile catherter tu. Catherter inatengenezwa na plastic na inaingizwa kwa sindsano ya kawaida. Kwanini iwe gharama kiasi hicho? The procedure itself takes less than 20 min to perform.

Kama ni kweli inalipiwa pesa hizo maana yake ni kwamba hospitali inacapitalise kwenye ujinga wa wateja wake.

So far ninachoamini ni kwamba hawa wanaosema ni shilingi mil. 5 hawana taarifa sahihi.
 
Vitabu vya dini vimebainisha kwamba mwanamke atazaa kwa uchungu,sasa hiyo njia ya kuondoa uchungu sidhani kama ni sahihi,ndio uchungu unauma sana ila hakyna raha kama kujifungua kwa uchungu,hata upasuaji mimi sipendi,nautaka uchungu wenyewe,maana ya kuitwa mama ni.lazima uwe umepitia labor pain atii duuuuu
 
mwanangu ntampenda tu sababu kubeba tumbo nayo si kazi ndogo. nashkuru kama imefika kairuki tutaifata huko huko kwa kweli:israel:
 
I once read in a magazine about epidural years back,sijawahi tu kusikia live mtu kaipitia nijue kama ina usalama,mwee usije kuwa reluctant kupush ukaumiza katoto kako jamani...
Mwenye eksipiriensi atuambie
 
:israel: :israel: :israel: gfsonwin, Fixed Point, Kaunga, Mwa J, KUJENI MSHANGAE!
hii nilishawahi kuisikia zamani, kama miaka 6 imepita. Nikajiuliza maswali mengi sana kuhusu hicho kinachifanya mtu asisikie maumivu.
Wakati bado naendelea kushangaa nikaenda conference moja ambapo mama mmoja wa ki-dutch alikuwa anatusimulia jinsi alivyojifungua twins kwa maumivu makali sana. alimwomba sana daktari wake ampe hiyo epidural lakini alikataa kata kata kuwa hana imani na hiyo kitu. na akamwambia uchungu wa kuzaa huwa hauui, atapona tu watoto wakishatoka.
 
...........Mimi hii kitu nina uzoefu nayo, nilipofika labor tu niliambiwa nipewe epidural.
Niliwakatalia, nikasema mimi nataka kuzaa kwa uchungu, tena uzazi wangu wa kwanza
nataka nisikie uchungu. Sasa uchungu ulivyokuja, weweeeee!! Bahati Mbaya mtoto aligoma kutoka,
hivyo nikaa na uchungu for almost 10 hrs, ile uchungu unakuja, unatoka. Baadaye uchungu ulivyochanganya
na mtoto hatoki, weeeeeee!! Nilihitaji mwenyewe epidural!! Niliwaambia nichomeni tu epidural.

Baada ya kupewa epidural tu, sikusikia uchungu hata kidogo. na Tv nilitazama!! Chezea epidural!!

Hata hivyo mwanangu bado aligoma kutoka, after 18 hrs ya labor... nikaishia emergency C-section.
Nikija kuzaa tena, lazima nipewe epidural. Ya nini kupata uchungu mkali vile na wakati kuna option ya kutopata uchungu. Ukipata mtaalamu mzuri haina tatizo lolote.
 
hii nilishawahi kuisikia zamani, kama miaka 6 imepita. Nikajiuliza maswali mengi sana kuhusu hicho kinachifanya mtu asisikie maumivu.
Wakati bado naendelea kushangaa nikaenda conference moja ambapo mama mmoja wa ki-dutch alikuwa anatusimulia jinsi alivyojifungua twins kwa maumivu makali sana. alimwomba sana daktari wake ampe hiyo epidural lakini alikataa kata kata kuwa hana imani na hiyo kitu. na akamwambia uchungu wa kuzaa huwa hauui, atapona tu watoto wakishatoka.
mwe nimebaki najishangalia, ila kwa africa nadhani hakuna bado wataalam, mmhhh wacha tukomae na uchungu mwe! miss u mah! Fixed Point
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom